Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,093
- 22,806
Dah.... Maneno yako yamejawa na busara sana ndani yake. Watoto wa siku hizi wanajifanya mapenzi wanayojua ni ya bata tu. Kuchaguana kwaajiri ya swaga za kupost mtandaoni wakijishebedua kwa kubenua midomo kama nyani anakula ubuyu, kubedua tako moja na kupiga picha za kufanana maflana na nguo za vitenge.Mkuu kile kiapo cha siku ya ndoa ...kuishi kwa shida na raha.....moja ya misingi yake ni kama hicho unachokizungumzia.....na sio shida na raha za kulala na njaa tu....kuna wakati mwenzio anaweza ugua akashindwa hata kwenda chooni au bafuni....ni wewe ndio wakumsaidia kwa kila kitu....anajisadia na kuoga kitandani.....je utaacha kumsadia kwa kuogopa harufu! ....ukifanya hivyo utakuwa umevunja kiapo cha ndoa....lakini vile vile kwenye ndoa....mke pia ni mama....na mme ni baba... hivyo kila mtu ni mtoto kwa mwenzie na mzazi wa mwenzie...na siku zote mzazi huwa haoni kinyaaa kwa mtoto wake....haya yote yanawezekana Kama tu mlioana kwa mapenzi ya dhati la sivyo sio rahisi kiivyo.
Wanasahau kuwa ndoa ni zaidi ya hayo, hakuna kitu muhimu katika maisha kumtunza na kumpenda mwenzako kwa hali zote.
Nimefeel sana huo mstari uliposema kuwa MCHUKULIE MTOTO WA MWENZAKO KAMA MTOTO WAKO HALAFU WEWE KUWA KAMA MZAZI KWAKE.
Ukitazama kiuhalisia katika mapenzi usipomchokulia mwenzako kama mtoto wako hautakuwa na huruma nae pale anapokosea kwasababu wazazi huwa wanahuruma sana na watoto wao hata wakosee kosa gani watawapokea kwa mikono miwili. Watawachapa, watawasema ila mwisho wa siku watawapokea tena na kuishi nao kwa upendo na ndio maana watoto ni ngumu sana kuwaacha wazazi nyakati za matatizo au hali ngumu na wakati wa raha huwa nao pia.
The same kwenye mahusiano, mtoto wa mwenzako huyo wazazi wamekukabidhi uishi nae, ana tabia au mwenendo mbaya usimuache akateseke au akataabike mbeleni, muonyeshe upendo kwa kumjali zaidi na kumfunda taratibu. Ni kweli samaki mkunje angali mbichi, ila hata akishakaushwa pia unaweza mnyoosha taratibu akanyooka.
Mwenzako anafanya ulevi unamuacha, anakuwa mvivu unamuacha, hajui kutunza pesa na kufanya maendeleo unamuacha hayo sio maisha, hebu jitume katika kuweka mambo sawa na kumsaidia aache upuuzi kwa juhudi na bidii zote unless awe anakubishia na kukuonyesha hataki huo. Msaada wako.
Pia katika kuwa kama mzazi kwa mwenzako, hilo jambo ni kuhimu sana. Mpenzi wako (girlfriend/mchumba/mke) anapokuwa na shida unampa msaada kwa kujali au unampotezea. Je unahakikisha anapata mahitaji yake. Anapoumwa unakuwapo kwaajiri yake kumhudumia kwa upendo na kumfariji na kumdekeza ajiskie yupo na baba yake au mama yake?! Unapomuona amekata tamaa unampa maneno ya lawama au unamkumbatia na kumbembeleza na kumjaza nguvu kama vile wewe ulivyojazwa nguvu kipindi ukiwa mdogo pale ulipokosa tumaini na kujiamini?! Je siku akiwa na furaha na mood yake haipo sawa unampa attention yako yote au unasema wanawake ukiwaendekeza watakupelekesha au unasema mwanaume msumbufu ana visa sana?!
Je, inapotokea mwenzako anataka kukumbatiwa tu na kuambiwa its okay am here for you, huwa unampa hiyo kitu?!
Upendo unanguvu sana ndio maana kwa nguvu ya upendo makahaba hugeuka kuwa mke mwema mara tu atakapokutana na mtu anaemjali na kumpenda na kumtreate kama mzazi.
Upendo unamfanya mwanaume mvivu kujikuta anabadilika nakuwa mchapa kazi kwa bidii ili kutomdisappoint mtu aliyempenda.....
Kupenda, kupendwa na kupendana ni raha sana pale unapokutana na copy yako. Usikate tamaa na matukio ya ujana, endelea kumtafuta zing wako.
