Wanandoa hii hali imewahikukukuta?

Wanandoa hii hali imewahikukukuta?

Mbona hii ipo wazi, anakupa mzigo mkubwa wa msosi ili upate nguvu za kitandani. Yawezekana performance yako bed ni ndogo ndoo maana anatumia nguvu ya msosi
 
Hata mimi napenda hubby ale haswaa tena mpaka tonge la mwisho,lakini ale ashibe kwa kiasi chake mambo ya kumlazimisha ale mpaka avimbiwe hapana,huyo mkeo ni wale wanawake ambao mume akijamba ndio heshima kwake kuwa umekula umeshiba,sasa ww ukila hata kujamba hujambi anajua hujashiba.................kula mzee umjambie mkeo afurahi.
Samahani, nina swali. Ulishawahi kuvuta bangi?
 
Ndoa zina mengi.

Mimi nimeoa huu mwaka wa 5 na tuna mtoto mmoja. Tatizo: Mke wangu akinitengea chakula anataka nimalize chote hata nikishiba. Nikibakisha tu nyumbani hapakaliki, ataanza kulia usiku kucha na maneno mara kwahiyo mimi sijui kupika, mara mbona mgahawani huwa hubakishi na maneno mengi.

Tatizo mimi si mlaji sana, na nilisha mweleza awe ananitengea kidogo ili nikimaliza aniongezee lakini wapi, huwa anajaza sahani yangu mpaka nasema hiii bagosha huu mlima kilimanjaro nitauweza kweli? Siku zingine najikaza namaliza kwa mbinde ili kuzuia vita lakini sometimes nashindwa.

Sijajua tatizo ni nini, nikibakisha tu naye anazira kula, anaondoka dining namkuta chumbani analia.

Wakuu hili tatizo umewahi kukumbana nalo? ulisovuje?
Muache, oa mwingine!
 
Nahisi kama chakula kina connection na mhaba
 
Inasikitisha sana sababu wamama wengi na hata waume zao hawana elimu ya lishe bora!

Ni ujinga fulani hivi.

Kuna mbaba Mzee aliambiwa na daktari apungue uzito kwa jinsi alivyokuwa anaumwa.

Lakini akifika nyumbani mkewe anamlazimisha ale kama mtoto la sivyo ni ugomvi mkubwa.

Sasa na kajiuliza mwanamke kama Huyo kweli anapenda mumewe awe na maisha marefu au anataka kumuua polepole?
 
hahaha! bro niashalipita mm hlo, we kumkomoa mshawishi muwe mnakula sahan moja hadi mwisho..
Hahahaaa hii nilifanyiwa nilikuwa mvivu mno kula,
Ikaanzishwa system ya kula sahani moja kwanzia hapo nikajifunza kupiga msosi
 
Huyo unatakiwa umkutanishe na Dokta wa Lishe au wataalamu kama Dokta Janabi mkiwa pamoja apate elimu atolowe ujinga kichwani mwake.

Wako wengi sana kwenye jamii waume kwa wanawake.

Kwanza werevu wengine mlo wa usiku wana skip completely

Halafu utake kunishilia chakula aaah wapi yarabi nafsi yangu wewe kama kulia lia tu mwaya !
 
Ndoa zina mengi.

Mimi nimeoa huu mwaka wa 5 na tuna mtoto mmoja. Tatizo: Mke wangu akinitengea chakula anataka nimalize chote hata nikishiba. Nikibakisha tu nyumbani hapakaliki, ataanza kulia usiku kucha na maneno mara kwahiyo mimi sijui kupika, mara mbona mgahawani huwa hubakishi na maneno mengi.

Tatizo mimi si mlaji sana, na nilisha mweleza awe ananitengea kidogo ili nikimaliza aniongezee lakini wapi, huwa anajaza sahani yangu mpaka nasema hiii bagosha huu mlima kilimanjaro nitauweza kweli? Siku zingine najikaza namaliza kwa mbinde ili kuzuia vita lakini sometimes nashindwa.

Sijajua tatizo ni nini, nikibakisha tu naye anazira kula, anaondoka dining namkuta chumbani analia.

Wakuu hili tatizo umewahi kukumbana nalo? ulisovuje?
Mwambie aache kukupakulia,pakua mwenyewe.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mwambie gharama za matibabu ya magonjwa ya presha, kisukari, figo ni kubwa sana na usumbufu wa kukosa raha, muulize kama anaijua bei ya kidonge cha presha na mgonjwa atatakiwa anywe kwa muda gani?!

Huyo atakuwa hajasoma na hana exposure!
 
Halafu kuna wanaume Eti wao kila mlo awapo nyumbani lazima apakuliwe na mkewe la sivyo ugomvi hadi vikao na wanafamilia!

Mapenzi ya kikoloni kabisa mahaba ya kiutumwa!

Mfano Eti mume atengewe maji ya kuoga apelekewe bafuni.

Mimi nawauliza hivi mfano nyumba ina master bed room , ina heater za maji ya moto na baridi kutakuwa na haja ya mke kumuandalia maji ya kuoga mumewe?
 
Nyumba ina heater mke akamuwashie heater amuwekee na taulo bafuni.
Dining Kuna sink la kunawa na maji yanatoka lkn atataka uje na kijagi na bakuli umnawishe. Pambav kabisa
 
Una kilo ngapi? Labda ndo zinamliza manake raha mwanamme akiwa na kibody flani yummy yummy. 😁😁😁😁🤭🤭
 
Nawe mpe mtihani kuwa hunipendi ndo maana unakula peke yako.Watu wanaopendana wanakula sahani moja sasa itabidi uwe unanisubir tunakula wote.
 
Back
Top Bottom