Grand Canyon
JF-Expert Member
- Jan 2, 2020
- 456
- 924
Ndoa zina mengi.
Mimi nimeoa huu mwaka wa 5 na tuna mtoto mmoja. Tatizo: Mke wangu akinitengea chakula anataka nimalize chote hata nikishiba. Nikibakisha tu nyumbani hapakaliki, ataanza kulia usiku kucha na maneno mara kwahiyo mimi sijui kupika, mara mbona mgahawani huwa hubakishi na maneno mengi
Tatizo mimi si mlaji sana, na nilisha mweleza awe ananitengea kidogo ili nikimaliza aniongezee lakini wapi, huwa anajaza sahani yangu mpaka nasema hiii bagosha huu mlima kilimanjaro nitauweza kweli? Siku zingine najikaza namaliza kwa mbinde ili kuzuia vita lakini sometimes nashindwa.
Sijajua tatizo ni nini, nikibakisha tu naye anazira kula, anaondoka dining namkuta chumbani analia.
Wakuu hili tatizo umewahi kukumbana nalo? ulisovuje?