Wananchi waridhishwa na huduma za wizara ya ardhi sabasaba

Wizara ya Ardhi

Senior Member
Joined
May 14, 2024
Posts
133
Reaction score
100
Baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) wameonesha kuridhishwa na huduma zinazotolewa na wizara hiyo.

Wakizungumza katika banda la Wizara ya Ardhi tarehe 4 Julai 2025 katika maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Mwl Nyerere Dar es Salaam, wananchi hao wamesema, huduma zinazotolewa ni nzuri na za haraka ukilinganisha na zile zinazotolewa ofisini.

Wametolea mfano wa huduma ya utoaji Hati Milki za Ardhi pamoja na ukadiriaji kodi ya pango la ardhi kuwa, ni moja ya huduma inayopatikana kwa haraka jambo linaloonesha kuwa, wizara imejipanga katika maonesho hayo.

"Tunaomba wizara iendelee kuboresha huduma zake ili kujenga imani kwa wananchi na serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" wamesema.

Katika maonesho hayo yaliyobeba kaulimbiu ya "Fahari ya Tanzania" Wizara ya Ardhi inatoa huduma za Hati Milki za Ardhi, Ubadilishaji jina (Deed poll), Ukadiriaji Kodi ya Pango la Ardhi, ushauri kuhusina na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya pamoja na utatuzi wa changamoto za sekta ya ardhi.

Aidha, huduma za sekta ya Ardhi katika manispaa zote za mkoa wa Dar es salaam za Kinondoni, Ubungo, Kigamboni, Ilala na Temeke zinapatikana

Vile vile, elimu kuhusiana na masula ya sekta ya milki, urasimishaji pamoja na namna ya kujiunga na Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) katika masomo kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada inatolewa na wataalamu sambamba na kutoa fomu za kujiunga na chuo hicho.
 
KUmbe kuna sabasaba?
Anyway poleni
 
Mimi sijaridhika.
Ni huko Sabasaba, sisi huku vijijini
Kijiji cha malamba
Kata ya Ruiwa
Wilaya ya mbarali
Mkoa wa Mbeya.
Tulitapeliwa na Wizara hiyo.
Tulipewa hati miliki za kimila za mashamba.
Lakini cha ajabu serikali ya kijiji ilitugeuka.
Mashamba ni yetu lakini wapangaji wa matumizi ya mashamba ni serikali.
Tunashindwa kuendeleza kilimo endelevu na cha kisasa.
Sababu tukimaliza tu kuvuna serikali inaita wafugaji wa kisukuma na kuwakabidhi mashamba yetu wachungie makundi makubwa ya ng'ombe.
Hatuwezi kupanda matunda
Mihogo kwa ujumla mazao ya kudumu.
Wanasingizia wafugaji hao wanachangia maendeleo ya sekondari.
Ukiwauliza wafugaji kwanini unaingiza ng'ombe mashambani kwa watu.
Wanajibu KIMELIPIA.
Risiti iko wapi na imeandikwa nini, anajibu hakijapewa.
Huku ni pesa mfukoni tu.
 
RITA pia imewakonga moyo
 
Inabidi mboreshe sera zenu kero ninyingi huku mtaani
 
Inasikitisha sana mkuu 😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…