Wananchi wapewa rai kujitokeza kupima kwa hiari VVU

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
WAZIRI MHAGAMA: JITOKEZENI KUPIMA VVU KWA HIYARI

Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea kujitokeza kupima VVU kwa hiari ili kujua hali zao ili kuendelea kuishi kwa kuzingatia matokeo, kwa wale ambao hawatakutwa na maambukizi ni nafasi kwao kuendelea kuishi ili wasiambukizwe na wale ambao watakutwa na maambukizi wana nafasi ya kuendelea kuishi kwa kutumia dawa za kufubaza.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kikao cha pamoja cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima kuhusu kuelekea maandalizi ya siku ya UKIMWI kitaifa kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mhagama amesema tafiti zote za miaka mitano zimeonesha wanaume hawajitokezi kupima, na hawajitokezi kuanza kupata dawa, na hivyo kusumbuliwa sana na magonjwa nyemelezi yanayotokana na virusi vya UKIMWI.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema maandalizi kuelekea wiki ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanaendelea vizuri.

Kauli mbiu kuelekea madhimisho ya siku ya UKIMWI kitaifa inasema "JAMII IONGOZE KUTOKOMZEA UKIMWI" yenye lengo la kuhamaisha jamii yenyewe ndio iongoze mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

28d745362cd8c7b5317bfb2cdea79573.jpg
 
Kama hakuna kampeni za kupima kwa hiari kama miaka ya nyuma zilivyopamba moto wananchi hawatapima mpaka waumwe na kuzidiwa ndio wanapima kujua wanasumbuliwa na nini. Kupima ni zoezi endelevu kwa kuwa wanakutana na wapenzi wapya mara kwa mara na hawawajui afya zao kama wana maambukizi au hawana na kuzidi kuchukua tahadhari
 
Back
Top Bottom