Kwa pande za Arusha, Majority ya watu wanaifagilia CHADEMA tu. Na hiyo issue ya jana ndio story kila pande. Watu wanaona kama CHADEMA wanaonewa hivyo hasira kwa ccm ndio imezidi. Masela wangu wa porini (mererani) wamenipigia simu kutaka kujua kuhusu ilivyotokea jana ingawa nawajua huwa hawafuatiliagi siasa kabisa. Kwa sasa hivi kuna bonge ya tension na watu wana link hii na yanayotokea misri na tunisia. Mi naona kama atakuja mtu influential akasema watu waingie street, yanayotokea misri itakua cha mtoto kwa comparison. Mimi mwenyewe nawatamani sana hawa wadosi. Wanatukatia umeme karibia daily halafu pande za uzunguni hata hawajui kama kuna mgao.
Halafu kwa hizi siku za karibuni, Landcruiser mkonge za polisi mpya zimekua nyingi hadi zinashindana na daladala kwa wingi. Kila kona ukipita unazikuta. kama wamezileta hizi kutokana na intelijensia yao ilivyowatuma, then, this time wako right! Ingawa kwa sasa polisi washakua mashemeji zetu hivyo hatuwaogopi.