Wananchi wanakula mizizi Kisarawe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wanakula mizizi Kisarawe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Samvulachole, Jan 21, 2012.

 1. S

  Samvulachole JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 22, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Juzi nimeenda Wilaya ya kisarawe nikashangazwa kuona dhiki ilkiyokubuhu kule. Lakini lililonitisha ni kuambiwa kuwa wananchi wako maeneo ya kibuta wana dhiki kiasi cha kuwa hawana hata chakula wameishia kula mizizi

  Hivi kweli miaka 50 baada ya uhuru imekuwaje wilaya ile inaonekana kama vile bado wako enzi za mkoloni mjerumani?

  Hivi jimbo la kisarawe lina mbunge kweli?

  wabunge waliopita ni:

  KIGOMA ALI MALIMA (marehem)

  MZEE JANGUO (alikuwa mkurugenzi THA)


  Jamani kuna siri gani ambayo inafanya viongozi wa serikali na chama na NGO's kulikimbia hili jimbo la kisarawe?

  Nashauri Rais atangaze hali ya dharura ili ijulikane imekuwaje wananchi ambao ni watanzania wanakula mizizi wakati kuna programu za maendeleo, wna wanatengewa fedha za maendeleo na wanakatwa kodi za kila namna
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Hata mihogo, viazi, magimbi, ni mizizi na tunaila mjini kila kukicha.
   
 3. M

  Mamatau Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alae mizizi Kisarawe ni kutokana na uvivu wake kwani ardhi ina rutuba ya kutosha na mvua za kutosha. Nawaasa waache biashara ya kuuuza ardhi na baadaye kubaki hawana kitu. Pia wpunguze muda wa kucheza ngoma na wafanye kazi zaidi!!!! Ajitakiaye shida hapewi pole!!!!!!
   
 4. jakirogo

  jakirogo Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ama kwel ukipenda chongo utaita kengeza!
   
 5. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Sisi tuko bize kutafuta vazi la taifa saa izi.
   
 6. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Serikali serikali serikali serikali! Ni kweli kumekuwa na uzembe katika kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo ambapo kwa kiasi kikubwa lawama tunaelekeza kwa serikali.

  Dhiki iliyoikumba kisarawe(njaa) inawezekana imechangiwa kwa kiasi kikubwa na mambo mawili au matatu, mosi hali ya ukame iliyotokana na mabadiliko ya tabia nchi, pili inawezekana ndugu zangu wa kisarawe hawakubakiza akiba ya chakula walikiuza chote kufanikisha mipango yao, pengine hata mavuno hayakuwa ya kutosha kutokana na hali mbaya ya hewa, na kama ni kweli wanauza ardhi kama ilivyosemwa hili pia sio jema linaweza kuwa na athari kubwa.

  Hoja ya kutangazwa hali ya hatari si rahisi kama inavyofikiriwa, kimsingi dhiki hii itafutiwe ufumbuzi kwa kuahakikisha wananchi wanapewa chakula lakini pia wananchi wanapaswa kuona umuhimu wa kuhifadhi chakula. Lawama kwa serikali wakati mwingine sio ufumbuzi wa tatizo, yeah ni miaka50 ya uhuru, ikumbukwe kuwa kuna maeneo mengi ukame umetamalaki na matokeo yake ni baa la njaa na kero nyingine nyingi. Mnawezajikuta mmetangaza hali ya hatari nchi nzima!

  Poleni sana wanakisarawe Mungu muweza wa yote atafanya jambo.
  Nawasilisha!
   
 7. R

  Radi Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  FF mchawi wako amekufa au????Mbona huna huruma hata kwa ndugu zako,kulikoni? Au mchawi ndio wewe mwenyewe?Lakini yote yana mwisho. Amen
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Mamatau kwenye post #3 kisha jibu vizuri sana.
   
 9. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,135
  Likes Received: 3,327
  Trophy Points: 280
  TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNASONGA MBELe!
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Saa nyingine tuangalie na upande wa wananchi wenyewe wapi wanakosea! Wakazi wa Kisarawe bado wanakumbatia mila na desturi ambazo kwa namna moja au nyingine zinachangia kurudisha nyuma maendeleo yao! Uvivu wa kulima na hata kufanya biashara unachangia; matumizi ya vyakula kwa sherehe za kimila nazo zinachangia. Rutuba wanayo sana tu, wana advantage ya kuwa karibu na soko kuu la vyakula nchini walitumie! Kule kunastawi mihogo kwa sana lakini ni wanhgapi wanalima mihogo kwa biashara? Wangapi wanahudhuria mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa wilayani mwao!?
   
 11. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Asiyefanya kazi na asile!
   
 12. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la njaa kwa watu wanaoishi vijijini kwa kutegemea kilimo kwa maisha yao hilo lipo. Na sio kama wavivu, bali kutokana na
  mabadiliko ya tabia ya hali hewa duniani hiyo ndio imewaathili sana. Mvua hazinyeshi kama inavyokuwa kawaida kutokana na haya
  mabadiliko. Ukame wa ardhi ndio uliosimama sasa hivi, na basi mvua ikinyesha inakuwa ni janga na kuharibu mazao yote
  shambani. Na hata kuharibu chakula chao cha akiba kwa kusombwa na maji ya mvua. Na ukiangalia nchi yetu na za majirani
  zetu hapa Afrika mashariki ndio tulioathirika sana, na ukiangalia ukulima wetu ni bado tupo katika primitive way.
  Serikali za Ulaya, amerika, Canada na Japan zimetoa ruzuku na zinaendelea kutoa kwa nchi masikini zilizoathirika na mabadiliko
  ya tabia ya hewa Duniani. Kwa kuangalia nchi hizo ndizo zimechangia kiasi kikubwa wa haya mabadiliko.
  Sasa cha kujiuliza Serikali ya Tanzania inawasaidia vipi hao waathirika mpaka wanafikia kula Mizizi, au ndio imekuwa zii pesa azijulikani
  zilipokwenda, na kwa ukiangalia mbele hao ndio wanahitajika kusaidiwa kwanza, kabla ya miundo mbinu na vitu vingine.
   
 13. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Na mbunge wa sasa ni Said Jafo, graduate wa Bsc. HE&HN SOKIONE UNIVERSITY, 2001
   
 14. T

  Tinker Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha wale majani

  wakifa wengine wataenda kuchukua ardhi na nafasi kwao
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  UVIVU

  Hakuna mwaka uliokuwa wa NEEMA ya mvua za kutosha kama mwaka jana (2011) kwa ukanda huu wa Kisarawe.

  Mvua za vuli zilizonyesha kuanzia mwezi wa November 2011, wananchi wengi waliolima sasa hivi wanakula na kuuza mahindi mabichi.

  Ni lazima wabadilike, vinginevyo njaa itawateketeza.
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mwaka 2011 nimevuna mpunga, mahindi hadi nikakosa sehemu ya kuhifadhi chakula, uvivu wa hawa watu unajulikana, ukitafuta vibarua kwa ajili ya palizi hawataki, inabidi tuchukue vibarua toka Pugu na Gongo la mboto asubuhi na kuwarudisha jioni.
   
 17. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ana Msc. ya CED (2007) pia!

   
 18. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ccm ilishinda kule kwa asilimia 99
  wanavaa hadi chupi za ccm
  hayo ndo maisha bora yao
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0


  Kwani ni jambo la ajabu sana huko Tanzania.

  Mbona tunasikia kwenye baadhi ya wilaya mikoa ya mara, Singida na shinyanga watu wanapata taabu kuliko hizo?

  Nafikiri ni vizuri uangalia nchi nzima na tatizo la njaa badala ya kuangalia vipande vipande na kushusha tuhuma kwa baadhi ya wabunge.

  Ni vizuri ujue Serikali imechangia nini katika kutaka kuharakisha maendeleo ya wananchi wake.

   
 20. a

  adobe JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  wamezoea kula mizizi kwani hawapendi kufanyakazi.
   
Loading...