PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Mgombea Ubunge jimbo la Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa na mgombea udiwani kata ya Gungu wa chama hicho, walipokuwa wakiomba kura kwa wakazi wa kata hiyo katika soko la masanga, wamekutana na kilio cha wananchi hao juu ya uboreshwaji wa soko hilo.
Mmoja wa wananchi hao alimueleza Zitto kuwa wanajutia kuukataa mpango waliowahi kupewa na Zitto juu ya uboreshaji wa soko hilo akisema "tulikupinga baadae tukajuta"
Jambo hilo limetokea wakati wa kampeni ya nyumba kwa nyumba iliyofanyika katika kata hiyo, mkoani Kigoma, Oktoba 24, 2025.