Wananchi wamkataa Waziri Karamagi
* Wasema hajatekeleza ahadi zake kwao
Na Stella Ibengwe, Geita
WANANCHI wa wilaya ya Geita mkoani Mwanza, wamemkataa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Nazir Karamagi, kwa madai kuwa yeye ndiye chanzo cha migogoro kati ya wawekezaji na wananchi wa maeneo ya migodi.
Hatua hiyo ya wananchi inafuatia ahadi za Waziri kutotekelezwa kwa muda mrefu na kuwafanya wananchi kuendelea kudhulumiwa haki zao bila kupata muafaka kutoka serikalini, kupitia wizara hiyo.
Wakizungumza jana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kalangalala wilayani humo, wananchi hao waliitaka Kamati ya Kuchunguza Mikataba ya Madini na kupitia sheria za madini chini ya uenyekiti wa Jaji Mark Bomani, kumfikishia taarifa Rais kuwa hawamtaki Waziri Karamagi.
Waliiambia Kamati hiyo kuwa iwapo Rais hatalifanyia kazi suala hilo, kuna matatizo makubwa ambayo yanaweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na wananchi kujichukulia sheria mkononi kutokana na kuchoshwa na ahadi zisizofanyiwa kazi huku wakiendelea kuumia.
Hatumtaki Waziri wa Nishati na Madini Karamagi, alishafika hapa Geita na akaambiwa matatizo yetu akaahidi kuyafanyia kazi, lakini mpaka leo hakuna alichotekeleza, unatarajia tuendelee kuwa na kiongozi wa aina hiyo, hatufai sisi kwani hajali matatizo yetu, tunaiagiza Kamati hii imfikishie taarifa Rais kuwa hatumtaki Waziri huyo, alisema mmoja wa wananchi hao, Bw. Lameck Petro, kwa niaba ya wananchi hao.
Waliitaka Serikali kujali maoni ya wabunge yanayotolewa wakati wa vikao vya Bunge kwani wao ndio wawakilishi wa wananchi na waliwachagua kwa kuwa na imani nao kwamba wanaweza kutetea haki zao katika majimbo wanayotoka.
Aidha, wananchi hao walisema ni aibu kwa nchi kama Tanzania, kwenda kuomba msaada Ulaya, wakati wana utajiri mkubwa wa madini wanaowapa Wazungu kuchimba na kuwaachia mashimo "watoto na wajukuu wetu ambao watakuja kutuuliza haya mashimo ni ya nini sijui tutawajibu nini?".
Walisema viongozi wa Sekta ya Madini hawako makini na ndicho chanzo cha chimbuko la matatizo yote ya migodini na kudai kuwa ukweli wa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, umesababisha kuundwa kwa kamati hiyo huku wakihoji kati ya Serikali na Zitto nani ni mkweli.
Akipokea malalamiko, mapendekezo, maoni na ushauri kutoka kwa wananchi hao, Jaji Bomani alisema pengine matatizo hayo yalikuwa hayamfikii Rais ambapo aliahidi kuyafikisha na kuwahakikishia kuwa yatafanyiwa kazi huku akiwaambia Kamati haikuja kutembea bali kufanya kazi.
Source: Majira