benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,517
- 3,174
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa illyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
Mhe. Dkt. Selemani Said Jafo (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Dkt. Jafo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Mhandisi Yahya Ismail Samamba ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara va Madini. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Samamba alikuwa Katibu Mendaji wa Tume ya Madini. Mhandisi Samamba anachukua nafasi ya Bw. Kheri Abdul Mahimbali ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Bw. Yusuph Juma Mwenda ameteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mwenda alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA). Yusuf Mwenda pia aliwahi kuwa diwani wa Mikocheni na Meya wa Kinondoni kuanzia mwaka 2010/ 2015
Bw. Alphayo Japan Kidata ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Ofisi ya Rais - Ikulu. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kidata alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)