Wananchi wafunga barabara Dar

Wananchi wafunga barabara Dar

...mama watoto wangu Leo nitachelewa kurudi nyumbani, kwa sababu barabara ya kuja kwetu nasikia imefungwa mpaka saa sita usiku!

Hata mimi baba watoto nitachelewa kwa shida hiyo hiyo!
 
sijawahi kusikia wananchi wanaoishi along morogoro road from manzese to fire/kawawa road magomeni to moroko/ali hassan mwinyi upanga to moroko/makumbusho wakiandamana kuwekewa matuta....

kwani ni kipande hicho cha kawe-tegeta?? kuna issue hapa magari yanakimbia sana barabara hio. juzi kati kuna mtu alileta thread hapa kusema ziwekwe taa kupunguza ajali nilisema chanzo cha ajali ni over speeding wala si taa ndio maana watu wanagongwa hovyo mchana kweupe.

kama hamuwezi kujicontrol nyinyi madereva wacha wawawekee matuta....speed camera hatuna tutatumia njia ya kijima matuta.

cc: Nyani Ngabu
 
sijawahi kusikia wananchi wanaoishi along morogoro road from manzese to fire/kawawa road magomeni to moroko/ali hassan mwinyi upanga to moroko/makumbusho wakiandamana kuwekewa matuta....kwani ni kipande hicho cha kawe-tegeta?? kuna issue hapa magari yanakimbia sana barabara hio. juzi kati kuna mtu alileta thread hapa kusema ziwekwe taa kupunguza ajali nilisema chanzo cha ajali ni over speeding wala si taa ndio maana watu wanagongwa hovyo mchana kweupe. kama hamuwezi kujicontrol nyinyi madereva wacha wawawekee matuta....speed camera hatuna tutatumia njia ya kijima matuta.

cc: Nyani Ngabu

Hizi barabara zinaboreshwa ili magari yakimbie zaidi na kuokoa muda. Tatizo ni matumizi ya hovyo kuanzia watembea kwa miguu na waendesha vyombo vya moto.

Tatizo jingine ni hilo la kutokuepo service road. Chukulia mtu anatoka Mwai Kibaki kuingia Bagamoyo road aje IMTU au Tanki bovu,angetumia service road badala ya kuingia ktkt. Jambo jingine lazima Tanroads waweke Zebra crossing maeneo maalum ya vivuko vya miguu. Na watembea kwa miguu waelimishwe kuvuka maeneo ya vivuko badala ya kuvuka hovyo na kuleta kero kwa madereva.
 
Last edited by a moderator:
Kuna mtu kagongwa kafia pale darajani kwa Komba. Wamefunga barabara zote nne. Wanataka matuta.Soon barabara yote itajaa matuta hata kwa makosa ya waenda kwa miguu
Kweli kabisa...........

Subiri Agongwe Mkeo Ndo Utajua Umuhimu Wa Matuta
Huu si uungwana....

Mke wangu ni marehemu siku nyingi.
Pole sana mkuu... Mungu amrehemu alale pema peponi. Amen

Aisee,Pole Sana Ndugu Yangu.
Niwie Radhi Kwa Kadhia Iliyojitokeza
Huu sasa ndo uungwana wa kiume....

Siku zote kusamehe ndio silaha kuu ya wenye 'hekima' mkuu.
Ushauri murua sana huu....

Acha Kujipendeleza Kwa Jamaa Kwa Kuwa Mke Wake Alishafariki. Wewe Ni Mtoto Wa Kiume Halafu Unaleta Ushambenga. Au Unataka Akuoe. Shauri Yako
He!!! Uungwana umeenda wapi tena???

Ulivyomuomba radhi jamaa nikajawa na fikra kwamba wewe ni muungwana.
Ila nimegundua abadani siwezi vijembe nawe.
Naomba nikutakie kheri mkuu.
Mjadala mwema.
Hata mimi nlijua hivyo......

Ahaaaa,Baxi Suluhisho Ni Wewe Dereva Uache Kutumia VIROBA NA MIRUNGI
Oh Gosh..........

Hilo neno hapo kwa blue limenifumbua macho....

Kila la kheri.
 
Tatizo kubwa ni serikali kushindwa kufanya kazi yake vizuri. Madereva wanatakiwa kutii sheria za barabarani, na wale wasiotii dawa yake ni kuwapatia adhabu kali.

Nasema serikali imeshindwa kwa sababu wasimamiaji au wanaotakiwa kukamata madereva wabovu wamejaa pale tegeta na kwenye junctions kubwa. Halafu polisi wenyewe sio wabunifu kwenye kazi yao, wanashindwaje kufanya spot checks kwenye vibao vinavyoelekeza mwendo na zebra crossings.

Kuweka matuta ni ishara ya udhaifu wa serikali na kutokustaarabika kwa madereva walio wengi.

Kama unataka kuendesha speed si ufanye safari ya mbali halafu uridhike. Halafu unakuta dereva anatimua speed kali halafu kumbe wala haendi mbali. Kuongoza Tanzania na watanzania waliowengi katika ngazi zote inataka moyo sana, na tunahitaji Rais ambaye utawala wa sheria humo damuni mwake!!
 
Hizi barabara zinaboreshwa ili magari yakimbie zaidi na kuokoa muda. Tatizo ni matumizi ya hovyo kuanzia watembea kwa miguu na waendesha vyombo vya moto.

Tatizo jingine ni hilo la kutokuepo service road. Chukulia mtu anatoka Mwai Kibaki kuingia Bagamoyo road aje IMTU au Tanki bovu,angetumia service road badala ya kuingia ktkt. Jambo jingine lazima Tanroads waweke Zebra crossing maeneo maalum ya vivuko vya miguu. Na watembea kwa miguu waelimishwe kuvuka maeneo ya vivuko badala ya kuvuka hovyo na kuleta kero kwa madereva.

Mbona hayo ya alama za barabarani yamefanyika, shida ni baadhi ya madereva. Tena wengine akiwa nyuma yako halafu kwenye 50 kph ukapunguza, jamaa anaku-overtake halafu anakumwagia na matusi. Fanya utafiti ndani ya wiki moja halafu uone kama bado utakuwa na mtazamo huu.
 
Nimekuwa naandika siku zote kwamba serikali imeshindwa kulinda barabara kwa kuweka utaratibu wa matumizi ya barabara hasa ktk hizii kubwa kama Bagamoyo,Kilwa,Nyerere,Morogoro,Mandela na Kawawa.

Kila siku natumia barabara ya Bagamoyo,ni kero tupu kuanzia malori mabovu,bajaj nyingine zikiendeshwa na madereva watoto,bodaboda na madereva wanao chat wakidrive vyombo vya moto!

Tatizo jingine la hii barabara ni Tanroads kushindwa kulinda hifadhi ya barabara na kuwaacha watu wakifanya biashara barabarani. Tatizo jingine ni ujenzi wa chini ya kiwango kwasababu barabara hii ingekuwa na service road kama Sam Nujoma magari yote yasingerundikana ktkt ya barabara!
Kuna kitu kinaitwa road management and traffic control, katika idara hii TANROADS inapwaya vibaya.
Wao wanafikiri kazi yao ni kujenga tu, management na traffic control wanafikiri ni kazi ya polisi.
 
Hizi barabara zinaboreshwa ili magari yakimbie zaidi na kuokoa muda. Tatizo ni matumizi ya hovyo kuanzia watembea kwa miguu na waendesha vyombo vya moto.

Tatizo jingine ni hilo la kutokuepo service road. Chukulia mtu anatoka Mwai Kibaki kuingia Bagamoyo road aje IMTU au Tanki bovu,angetumia service road badala ya kuingia ktkt. Jambo jingine lazima Tanroads waweke Zebra crossing maeneo maalum ya vivuko vya miguu. Na watembea kwa miguu waelimishwe kuvuka maeneo ya vivuko badala ya kuvuka hovyo na kuleta kero kwa madereva.

zebra crossing! unaongelea madereva wa bongo au.......zebra crossing zipo kibao ila madereva wanaozingatia ni almost zero %??? hayo mengine yote nakubaliana na wewe.
 
Mbona hayo ya alama za barabarani yamefanyika, shida ni baadhi ya madereva. Tena wengine akiwa nyuma yako halafu kwenye 50 kph ukapunguza, jamaa anaku-overtake halafu anakumwagia na matusi. Fanya utafiti ndani ya wiki moja halafu uone kama bado utakuwa na mtazamo huu.

ajali nchi hii chanzo kikubwa ni madereva....hasa madereva wa dar es salaam ndio hovyo kabisa....hizo alama zipo kibao lakini hamna anaezingatia, sidhani kama ndani ya dar es salaam kuna barabara inaruhusiwa kuendesha zaidi ya 60kph lakini hio ya tegeta watu wanakimbizana over 100kph!!!
 
Kuna kitu kinaitwa road management and traffic control, katika idara hii TANROADS inapwaya vibaya.
Wao wanafikiri kazi yao ni kujenga tu, management na traffic control wanafikiri ni kazi ya polisi.

Sahihi kabisa barabara zetu wameachiwa Polisi wa trafiki badala ya wahusika ktk Wizara ya Uchukuzi,Sumatra na Tamisemi. Na mbaya zaidi nasi tunawalaumu matrafiki badala ya wahusika. Haishangazi solution yao siku zote ni kujenga matuta ambayo yanaharibu barabara na kuongeza msongamano mkubwa.
 
zebra crossing! unaongelea madereva wa bongo au.......zebra crossing zipo kibao ila madereva wanaozingatia ni almost zero %??? hayo mengine yote nakubaliana na wewe.

Jaribu kuangalia Zebra crossings ktk barabara hii zimewekwa wapi,mbele ya vituo ambako Daladala zinaziba kabisa hata hizo Signs,huku shughuli kibao za kibiashara zikiendelea kituoni na ndani ya hifadhi ya barabara!!

Zebra zitaheshimika pale Watembea kwa miguu na madereva watakapo anza kuziheshimu. Na pili adhabu kali zitakapo tolewa kwa madereva watakao sababisha ajali kizembe ktk Zebra crossings!
 
nazungumzia zebra crossing nchi nzima na tabia za madereva wetu....hata zikikaa sehemu sahihi hawa madereva wa tanzania sana sana dar es salaam ni vichaa,hawajui zebra crossing ni nini!!! mtembea kwa miguu ndio anasubiri gari ipite kwenye zebra crossing only in bongo.

kuhusu adhabu kwa madereva wazembe hawa sumatra na trafiki ndio wauwaji wakubwa kwasabbu ndio wanaolea huu ujinga kwa kuendekeza rushwa saaana
 
Subiri Agongwe Mkeo Ndo Utajua Umuhimu Wa Matuta

mkuu matuta sio solution ya watu kugongwa, elimu ya matumizi sahihi ya barabara kwa waendesha magari, pikipiki, baskeli na watembea kwa mguu ni muhimu sana.

Binafsi pamoja na matuta nishamkosakosa mtoto wa shule pale boko magereza, tena alikua na dada mtu mzima kidogo, badala ya kumshika mtoto mkono wavuke wote, yeye kamwacha mwenyewe. mtoto kakurupuka kavuka, kwavile nlikua katika mwendo wa tahadhari niliweza ku control situation nika simamisha gari kando. nashuka namuuliza yule dada kwanini hawi mwangalifu na mtoto, yeye anacheka tu. nikamchapa kibao kimoja tu akarudi kwenye senses zake akaomba msamaha.

believe me ajali nyingi sana barabarani ni results za uzembe wa watumiaji barabara
 
Wananchi wa barabara ya Tegeta wamefunga barabara wakishinikizwa kuwekwa matuta barabarani humo. Hali sasa ni tete kwa wanaotoka au kuelekea Tegeta. Foleni ni kubwa mno.

Chanzo: EA Radio

Maneo ya njia panda ya kawe/bondeni kumekuwa na ajali za mara kwa mara sana
 
Back
Top Bottom