Wananchi wafunga barabara Dar

Wananchi wafunga barabara Dar

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,143
Kagongwa copy.jpg

Wananchi wa barabara ya Tegeta wamefunga barabara wakishinikizwa kuwekwa matuta barabarani humo. Hali sasa ni tete kwa wanaotoka au kuelekea Tegeta. Foleni ni kubwa mno.

Chanzo: EA Radio
 
Subiri Agongwe Mkeo Ndo Utajua Umuhimu Wa Matuta

Sasa mkuu barabara zote zikijaa matuta kutakuwa na safari kweli!?.
Ni kweli madereva kwa asilimia kubwa huwa wanafanya makosa barabarani,lakini hata watembea kwa miguu nao ni vivyo hivyo.
Mbaya zaidi ikishatokea ajali moja kwa moja lawama zinaenda kwa dereva.
La muhimu ni kuheshimu taratibu na sheria za barabarani kwa watumiaji wote.
 
Mi nadhani serikali iweke msimamo wao, waweke sehemu za kuvuka watu watuachie barabara zetu.
Kwanza hawa nao wamekosa kazi ndo maana wanaenda kukaaa barabarani.
Angalia hata watu wanawashangaa
 
Sasa mkuu barabara zote zikijaa matuta kutakuwa na safari kweli!?.
Ni kweli madereva kwa asilimia kubwa huwa wanafanya makosa barabarani,lakini hata watembea kwa miguu nao ni vivyo hivyo.
Mbaya zaidi ikishatokea ajali moja kwa moja lawama zinaenda kwa dereva.
La muhimu ni kuheshimu taratibu na sheria za barabarani kwa watumiaji wote.

Jamaa mtu wa ajabu sana. Amenitusi lakini namsamehe tu
 
Nchi hii mpaka tatizo litokee ndio tutafute solusheni
 
Kuna mtu kagongwa kafia pale darajani kwa Komba. Wamefunga barabara zote nne. Wanataka matuta.Soon barabara yote itajaa matuta hata kwa makosa ya waenda kwa miguu
Watu wanafikiri barabara ni sitting room na hata polisi wa barabarani hawachukulii hatua yoyote wale wanao tumia vibatya barabara.
Barabara ni kwa magari lakini mikokoteni, guta na baiskeli za mwendo wa 0-5km per hr zinashindana na gari za 60-100km/hr
Huu ni uenda wzzimu
 
Acha Kujipendeleza Kwa Jamaa Kwa Kuwa Mke Wake Alishafariki. Wewe Ni Mtoto Wa Kiume Halafu Unaleta Ushambenga. Au Unataka Akuoe. Shauri Yako

Ulivyomuomba radhi jamaa nikajawa na fikra kwamba wewe ni muungwana.
Ila nimegundua abadani siwezi vijembe nawe.
Naomba nikutakie kheri mkuu.
Mjadala mwema.
 
Watu wanafikiri barabara ni sitting room na hata polisi wa barabarani hawachukulii hatua yoyote wale wanao tumia vibatya barabara.
Barabara ni kwa magari lakini mikokoteni, guta na baiskeli za mwendo wa 0-5km per hr zinashindana na gari za 60-100km/hr
Huu ni uenda wzzimu

Nimekuwa naandika siku zote kwamba serikali imeshindwa kulinda barabara kwa kuweka utaratibu wa matumizi ya barabara hasa ktk hizii kubwa kama Bagamoyo,Kilwa,Nyerere,Morogoro,Mandela na Kawawa.

Kila siku natumia barabara ya Bagamoyo,ni kero tupu kuanzia malori mabovu,bajaj nyingine zikiendeshwa na madereva watoto,bodaboda na madereva wanao chat wakidrive vyombo vya moto!

Tatizo jingine la hii barabara ni Tanroads kushindwa kulinda hifadhi ya barabara na kuwaacha watu wakifanya biashara barabarani. Tatizo jingine ni ujenzi wa chini ya kiwango kwasababu barabara hii ingekuwa na service road kama Sam Nujoma magari yote yasingerundikana ktkt ya barabara!
 
Back
Top Bottom