Wananchi wa Mbagala wapelekewa huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imeendelea kusogeza huduma zake za kibingwa kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini, ambapo wagonjwa 150 wamehudumiwa katika Hospitali ya Epiphany Mbagala iliyotolewa Machi 31, 2023.
e890f36e-1311-476d-90fb-f67b900123c2.jpg
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Anthony Assey amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuipa kipaumbele Sekta ya Afya, hivyo ni muhimu kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi.

“Tuko hapa Mbagala ambapo tunashirikiana na wenzetu wa hospitali hii kusogeza huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wananchi ili kuwaondolea usumbufu wa kufuata huduma MOI kupitia kwenye huduma yetu ya kliniki jongefu (MOI Mobile Clinic),” alisema Dkt. Assey.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Epiphany, Pharles Yikobela ameishukuru na kuipongeza Taasisi ya MOI kwa kuanzisha huduma ya Kliniki Jongefu (MOI Mobile Clinic) ili kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi.
7e8dd69f-0e5c-4e9c-9d4a-918b2cacc551.jpg

40be4586-8302-4e98-90c5-82f3776a1d16.jpg
“Niwaombe MOI wasiishie tu hapa, waendelee kuja tena na tena kwenye Hospitali yetu ya Epiphany ili wananchi waendelee kunufaika na programu hii ya Kliniki jongefu,” ameisema Yikobela.

Naye, Daktari Bingwa wa Mifupa Dkt. Bryson amewaasa wananchi kuendelea kuchangamkia fursa ya huduma za Kliniki Jongefu ya MOI kwani ni fursa ya kipekee kwa wananchi kupata huduma za kibingwa za MOI bila kulazimika kufika MOI.

fff5ac08-0228-44fb-b1a3-8a14e31896c3.jpg

00954457-691e-43a9-bfd7-ea1727ec86c0.jpg
Mkazi wa Mbagala, Husna Ramadhani ameushukuru uongozi wa MOI pamoja na Epiphany kwa kutusogezea huduma za kibingwa katika eneo la Mbagala kwani imesaidia kuwapunguzia gharama na usumbufu kwa Wananchi kufuata huduma MOI.
 
Back
Top Bottom