Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,986
Wakazi wa Mitaa ya Bughudadi, Kizinga na Moringe, Kata ya Mbagala wameilalamikia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wa kutowatimizia mahitaji yao ya maji maeneo yote na kudai kuwa hali hiyo inawalazimu kutumia muwekezaji binafsi kupata huduma hiyo.
Malalamiko hayo yamekuja kutokana na hivi karibuni uongozi wa DAWASA Kata ya Mbagala kutoa notisi ya kumtaka mwekezaji binafsi kusitisha usambazaji wa maji ndani ya siku 30 kwa kuwa anafanya kazi kinyume cha utaratibu.
Sehemu ya malalamiko hayo ambayo Wananchi wameyawasilisha kwa Diwani wa Kata hiyo kwa njia ya maandishi tarehe 24 Oktoba 2022 wamedai kuwa wamesikitishwa na maamuzi hayo kwa kuwa wameshatoa ushauri wao kwa DAWASA lakini haujafanyiwa kazi.
Katika malalamiko hayo wananchi hao wa mitaa hiyo mitatu wameeleza kuwa kabla ya zoezi la kusitishwa kwa huduma ya mwekezaji binafsi waliomba kikao cha DAWASA na Wananchi ili watoe dukuduku lao kuhusu huduma za DAWASA lakini hilo halijafanikiwa.
Pia wameeleza kuwa hofu yao ni kuwa mwekezaji huyo ambaye amekuwa akitoa huduma hiyo ya maji tangu mwaka 2008 hata kabla ya DAWASA kuanza kutoa huduma eneo hilo, amemuwa msaada kwao wakati huu ambao kuna shida ya maji na Serikali imeto tamko juu ya uhaba wa maji.
Alex Mgala, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Bughudadi amesema: "Ni kweli malalamiko yapo kutoka kwa wananchi, tulipata barua kutoka DAWASA na sisi tukawaomba kwa mdomo kukutana nao tushauriane kuhusu uhalisia wa tatizo la maji lakini hawakutupa nafasi hiyo.
"Tumeshapeleka malalamiko yetu kwa Diwani wa Mbagala, Mwenyekiti wetu anashughulikia suala hilo, sisi hatua lengo baya na DAWASa, tunachohitaji ni huduma nzuri ya maji, kumuondoa mwekezaji binafsi wakati wao hawajajipanga ni sawasawa na kurejesha tatizo la maji kwetu."
Akizungumzia kuhusu malalamiko hayo, mmoja wa viongozi wa DAWASA Mbagala alisema: “Mimi siyo msemaji wa DAWASA, lakini kwa ufupi niseme tu hatujapata malalamiko rasmi kutoka kwa wananchi kuhusu sisi kutokidhi mahitaji.
“Tukipata malalamiko yoyote tutayafanyia kazi, kuhusu mwekezaji binafsi wa Bughudadi ni kweli amekuwa akifanya kazi kinyume cha sheria na ameeleweshwa juu ya hilo hata kama amekuwa akiuza maji kwa kusaidia wananchi.
“Tupo naye katika mazungumzo na tunaendelea vizuri.”
Hata hivyo, kutokana na kupungua kwa maji katika Mto Ruvu ambao unatumika kusambaza maji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameshatoa maelekezo kwa kuagiza DAWASA kushirikiana na wenye visima vya maji kutoa huduma hiyo ili kupunguza madhira yanayowapata wakazi wa mikoa hiyo.