Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Haihitaji kuwa mtabiri kuliona hili jambo kuwa nchi yetu inapitia katika kipindi cha hatari ambacho hakijawahi kupitiwa tokea nchi yetu ipate Uhuru wake mwaka 1961........
Wasomaji wa mada hii mtakuwa na shauku ya kujua kivipi Taifa letu linapitia katika kipindi cha hatari?
Nitafafanua suala hilo kama ifuatavyo:-
Ingawa Taifa letu lina Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama ya nchi yetu, tumeshuhudia tokea Rais wetu wa awamu ya 5 aingie madarakani ni kama vile "ameisuspend" kutumika nchini Katiba ya nchi yetu na matamko yake ya kwenye majukwaa ya kisiasa ameyageuza kuwa ndiyo sheria za nchi hii zinazopaswa kufuatwa!
Hivi ni nani asiyejua kuwa Katiba ys nchi yetu inatamka wazi kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vinapaswa kufanya shughuli zake bila kuingiliwa na chombo chochote?
Sasa tujiulize Rais wetu alitumia mamlaka yapi kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani hususani chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema hadi ifikapo mwaka 2020 wakati yeye na chama chake cha CCM wakiendelea kufanya mikutano ya kisiasa nchi nzima bila kuzuiwa na Polisi?
Na je Jeshi letu la Polisi linapata wapi mamlaka ya kuwakamata viongozi wetu wa vyama vya upinzani wanapotekekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa mujibu wa Katiba kama siyo kutekeleza maagizo "batili" ya Rais wetu?
Tumeshuhudia wabunge almost wote wa Chadema kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikamatwa na Jeshi letu la Polisi kwa ajili tu ya kufanya mikutano ya kisiasa ambayo ni haki yao ya kikatiba lakini serikali hii ya awamu ya 5 na Jeshi letu la Polisi imekuwa ikiichukulia kuwa ni mikutano haramu isiyopaswa kuwepo!
Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake alipokuwa hai aliwahi kusema kuwa Rais wetu tunayemchagua ni lazima aitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu ambayo aliapa kuilinda kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa letu.
Mwalimu akaenda mbali zaidi katika hotuba hiyo kwa kusema kuwa anapotokea Rais ambaye hataki kuitii Katiba ya nchi yetu Rais wa aina hiyo HATUFAI....
Mwalimu akamalizia hotuba hiyo ya hekima kubwa kwa kusema atakapotokea Rais wa aina hiyo wananchi tuna wajibu wa kumwambia Rais wa aina hiyo atuachie Urais wetu na yeye akafanye shughuli zake nyingine kama vile kufunga ng'ombe na kadhalika.....
Inashangaza kuona watanzania tukimuona Rais wetu akiisigina waziwazi Katiba ya nchi yetu na sisi wananchi ambao ndiyo Waajiri wa huyo mwajiriwa wetu (Rais) tunaamua kukaa kimya na kuendelea kumshangilia kwa uvunjifu huo wa wazi wa Katiba ya nchi yetu!
Iwapo kweli sisi wananchi bila kujali itikadi zetu za kisiasa kama kweli tunataka kumuenzi Mwalimu kwa vitendo tunapaswa kupaza sauti zetu kwa nguvu zote kumwambia Rais wetu arejee kwenye mstari na aiongoze nchi yetu kwa mujibu wa Katiba yetu, na kama hatataka kuongoza nchi yetu kwa mujibu wa Katiba yetu, wananchi tunapaswa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo kwa kufuata wosia wake kwa kumwambia Rais wetu kuwa tunakuomba utuachie Urais wetu na wewe nenda kafanye shughuli zako nyinginezo..........
Mungu libariki Taifa letu la Tanzania