Wananchi sasa wamchoka JK

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Ufisadi uliotingisha bunge katika wizara ya Nishati na Madini - Kwa nini hao mawaziri wasijiuzulu?

Inaonekana hawa mawaziri wana nguvu inayowalinda


Licha ya wananchi wa mijini kuchoka migao ya umeme, hali ngumu ya maisha pia Wakulima (wananchi wa vijijini) kutokana na mafuta taa kupanda bei.

Bei kubwa ya mafuta taa imefanya maisha kuwa magumu sana vijijini.

Hata huku mjini, hakuna umeme watu wanategemea mafuta taa, ila bei imepanda maradufu.

Wakati huo huo JK hana habari na shida za watanzania.
 
sasa wananchi wamemchoka vp jk? Bado hoja inaelea mkuu.

Wewe Dazu uko mjini na unatumia Generator, huna shida

Bei ya mafuta taa inawaumiza wananchi wa vijijini, ongezeko la shs 400 kwa lita ni kubwa mno.

Wewe Dazu unaona misitu itapona? Na kama misitu haitapona, je vyanzo vya maji vitapona? na vyanzo vya maji havitapona je, mabwawa yatajaa maji ili Tanesco wazalishe umeme.

Ewura na Ngeleja au Bosi wake labda wanafikiri kwa Tumbo --- Kama Vile Nape na Sam Sitta alivyosema Mbeya kuwa baadhi ya Mawaziri wanafikiri kwa Tumbo.

Huku mjini hakuna umeme, pia watu wanatumia mafuta taa.

Biashara zote zinategemea umeme huku mjini, jee wananchi wanafurahia mgao na bei kubwa ya mafuta???
 
mr kikwete has no guts to be the chief executive of this country, he has failed to deliver his campaign promises, got a divided cabinet, power crisis, a record high national debt.........., mr president there is no substitute to resignation.
 
Ufisadi uliotingisha bunge katika wizara ya Nishati na Madini - Kwa nini hao mawaziri wasijiuzulu?Inaonekana hawa mawaziri wana nguvu inayowalindaLicha ya wananchi wa mijini kuchoka migao ya umeme, hali ngumu ya maisha pia Wakulima (wananchi wa vijijini) kutokana na mafuta taa kupanda bei.Bei kubwa ya mafuta taa imefanya maisha kuwa magumu sana vijijini.Hata huku mjini, hakuna umeme watu wanategemea mafuta taa, ila bei imepanda maradufu.Wakati huo huo JK hana habari na shida za watanzania.
yan wizara ya madini ndo utumbo na wizi mtupu twafanyiwa!Tanzanite peke yake inahudumia chuo kikuu kmoja kuanzia chakula mpaka ada!
 
Magwanda nanyi hamueleweki yani kashifa ya Jairo ndio mawaziri wa Wizara zote wajiuzuru? Mmmmh magwanda kuweni serious!
 
Ufisadi uliotingisha bunge katika wizara ya Nishati na Madini - Kwa nini hao mawaziri wasijiuzulu?Inaonekana hawa mawaziri wana nguvu inayowalindaLicha ya wananchi wa mijini kuchoka migao ya umeme, hali ngumu ya maisha pia Wakulima (wananchi wa vijijini) kutokana na mafuta taa kupanda bei.Bei kubwa ya mafuta taa imefanya maisha kuwa magumu sana vijijini.Hata huku mjini, hakuna umeme watu wanategemea mafuta taa, ila bei imepanda maradufu.Wakati huo huo JK hana habari na shida za watanzania.
wananchi gani waliomchoka? labda hao ni wale ambao hata hawakumpa kura zao kwahiyo hao hatuwahitaji kwenye takwimu. Mimi kama mwananchi niliyempa kura yangu JK nawalaumu sana wale wapambe wanaokuwa pembeni ya \j\k all the time ambao hatukuwachagua, wanatumia nyadhifa zao kumficha raisi ukweli wa nini kinachoendelea. Pale serikalini watendaji wetu wanaonekana kuwa na makundi na wanaishi na makundi yako na matokeo yake hawafanyi isue zinzowagusa wananchi na hili kundi kubwa ni la wale wanaoteuliwa na rais yaani watendaji ktk wizara.
 
wananchi gani waliomchoka? labda hao ni wale ambao hata hawakumpa kura zao kwahiyo hao hatuwahitaji kwenye takwimu. Mimi kama mwananchi niliyempa kura yangu JK nawalaumu sana wale wapambe wanaokuwa pembeni ya \j\k all the time ambao hatukuwachagua, wanatumia nyadhifa zao kumficha raisi ukweli wa nini kinachoendelea. Pale serikalini watendaji wetu wanaonekana kuwa na makundi na wanaishi na makundi yako na matokeo yake hawafanyi isue zinzowagusa wananchi na hili kundi kubwa ni la wale wanaoteuliwa na rais yaani watendaji ktk wizara.

Mkuu mbona unajichanganya sasa. Kama umempa kura Kikwete na bado una-imani naye; mbona ameteua watu bomu (kutokana na mtizamo wako hapo juu). Je hii inakueleza nini kuhusu JK as a leader and the main decision maker? Je kwenye teuzi hizo alikua anaangalia nini kwa watu hao (aliwateua kwa madhumuni yapi hasa) ?
 
this is coz siasa za bongo zina uongo mwingi and lack of accountability.Haiwezekani nchi ipo gizani afu mkuu wa kaya anapeta kwenye ful URANIUM ELECTRICITY ile hali nchi ina taabika
 
wananchi gani waliomchoka? labda hao ni wale ambao hata hawakumpa kura zao kwahiyo hao hatuwahitaji kwenye takwimu. Mimi kama mwananchi niliyempa kura yangu JK nawalaumu sana wale wapambe wanaokuwa pembeni ya \j\k all the time ambao hatukuwachagua, wanatumia nyadhifa zao kumficha raisi ukweli wa nini kinachoendelea. Pale serikalini watendaji wetu wanaonekana kuwa na makundi na wanaishi na makundi yako na matokeo yake hawafanyi isue zinzowagusa wananchi na hili kundi kubwa ni la wale wanaoteuliwa na rais yaani watendaji ktk wizara.
Katika hali ya kawaida nisingekugongea like, lakini umejaribu kusema jambo fulani pamoja na uwakala wako!

Swala la msingi ni je? Rais anachaguliwa ili awategemee 100% hao wanaosimama pembeni yake na wateule wake? Kama jibu ni ndio...........yeye tunamchagua wa nini sasa!!!

Kama anaowateua wanamfanya katuni, wanakwiba bila woga, wanamkenulia meno nae anasema good job!!...........yeye tulimchagua ili ateue majizi? au tulimchagua asiweze kusimamia hata kitu kimoja???

Kama amechaguliwa na aliowachagua ndo wanamuangusha.................Je, hata wale ambao hajawateua yeye kama wabunge.......wote wa Upinzani na wale wa chama chake wenye nia njema wanapomwambia ....mkuu, wanakudanganya haoooo!!! wezii haooo mkuu!!! kwa nini hasikii??? kwa nini mpaka apate aibu,...aaibishwe na wateule wake ndo anaanza kuhaha kwa kutoa majibu ya vijana wa Form One B shule ya secondary Ilembula?? Rahisi rahisi tu!!

Imagine............eti tatizo la umemem ni la ukame...........Basi, yani tumemchagua na yeye akachagua wasaidizi ile wafanye mambo kwa mzunguko wa dunia na jinsi Mungu na mawingu yatakavyopenda? Mvua za vuli zisiponyesha this year (ofcouse hatutegemei yeye akawe mawingu ili inyeshe!!) TOTAL BLACK OUT!!!

Viongozi wa CCM wanaoipenda nchi hii, ambao hawapo serikalini wako wapi? tuwasikie wakiwakemea wateule wa Kikwete? Wazee wa DSM wakwapi? au kwao umeme unawaka, mafuta ya taa wananua bei gani? Wao hawawezi kumuita Huyu waliyempa kura nyingi na kumwambia......Bwana mkubwa, tunaumia, wanatuumiza, wateule wako wanatukandamiza sisi huku wakineemeka wao!! fanya jambo hima!!
Sio kila siku litokeapo jambo la msingi kwa wananchi, anawaita wazee na kuwapa posho na kuanza kupiga mkwala..........wazee wampige mkwala pia basi!!

Hizi jumuia za wazazi wa CCM, wakina mama ziko wapi? wanafanya nini? au kazi yao ni kukutana kwenye mikutano mikuu na kupeana posho na MIPASHO TU!!!!

Inaniuma sana!!!! this guy need to act.............aanze na kuwa serious kwanza na aache kufikiri WTZ ni mapoyoyo!!!
 
Alikwisha kuchokwa siku nyingi ndio maana hata uchaguzi uliopita wote tunajua alivuna nini, tofauti na uchaguzi wa 2005
 
Wapiga kura mapoyoyo, walimchagua poyoyo, akateua mawaziri mapoyoyo wanatenda upoyoyo, hata hizo complement zimefanywa kwa bahati mbaya tuuuuu! yaani ni upoyoyo kwa kwenda mbele.
 
wananchi gani waliomchoka? labda hao ni wale ambao hata hawakumpa kura zao kwahiyo hao hatuwahitaji kwenye takwimu. Mimi kama mwananchi niliyempa kura yangu JK nawalaumu sana wale wapambe wanaokuwa pembeni ya \j\k all the time ambao hatukuwachagua, wanatumia nyadhifa zao kumficha raisi ukweli wa nini kinachoendelea. Pale serikalini watendaji wetu wanaonekana kuwa na makundi na wanaishi na makundi yako na matokeo yake hawafanyi isue zinzowagusa wananchi na hili kundi kubwa ni la wale wanaoteuliwa na rais yaani watendaji ktk wizara.
Kwan jamaa haon hali halis ya maisha ya watu wake mpaka aambiwe na wasaidizi wake? Huyo Njaa Kaya aliwahi kuulizwa na ktuo kimoja kikubwa cha television duniani kuwa kwanini nchi yake ni maskini wakati ina raslimali kibao, mjamaa akasema hajui! Sas kama hajui anagombea urais ili afanye nini kama hajui chanzo cha umaskini wetu? Hawez kufanya kitu kwa kuwa hata hajui kazi inayomfanya awe madarakani!
 
Kama bado unahitaji maelezo juu ya kuchokwa kwa Kikwete basi ndugu yangu wewe ni kilaza sana. Samahani lakini.

Nadhani arekebishe aandike "Wananchi sasa hawamtaki Kikwete", maisha gani haya aliyotuahidi?
 
Watanzania ni wajinga!Inabidi huruma kuwaongoza.Kama Mh Rais angekuwa anawajali kiukweli,then angechukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu.Kama yamemshinda na wasaidizi ni vilaza,aone huruma ajiuzulu.
Na wananchi nao waache domo domo,wao walimpigia kura kwa mara ya pili.So either they shut up or put up wit it!Otherwise waombe huruma imwingie JK.
 
Kwa mara ya kwanza leo hii nimefikiria sana kuhusu mustakabali wa nchi yetu na kujikumbusha maneno ya Obama alipokuwa Accra, Ghana.. katika hotuba yake nitanukuu kipande kimoja cha hotuba yake ambacho kimenikuna zaidi...Obama alisema haya:-

"Kwanza, ni lazima tuziunge mkono serikali zenye demokrasia imara na zilizo endelevu. Kama nilivyosema Cairo, kila taifa linaipa demokrasia uhai katika njia yake ya kipekee, na kwa kuzingatia desturi zake. Lakini historia inatoa uamuzi ulio bayana: serikali ambazo zinaheshimu utashi wa watu wao wenyewe zina ustawi zaidi, ziko imara zaidi, na zinafanikiwa zaidi ya serikali zisizofanya hivyo.

Hii ni zaidi ya kuwa na uchaguzi tu-pia ni juu ya kile kinachotokea kati yao. Kuna aina nyingi za ukandamizaji, na mataifa mengi sana yamekabiliwa na matatizo ambayo yanapelekea raia wake kuwa maskini. Hakuna nchi itakayoumba utajiri ikiwa viongozi wake wanatumia uchumi kujitajirisha wenyewe, au polisi wanaweza kununuliwa na walanguzi wa madawa ya kulevya. Hakuna biashara yoyote inayotaka kuwekeza mahali ambapo serikali inajichukulia asilimia 20 vivi hivi au mkuu wa Mamlaka ya Forodha ni mla rushwa. Hakuna mtu yeyote anayetaka kuishi katika jumuiya ambako utawala wa kisheria unageuzwa kuwa utawala wa ukatili na hongo. Hii si demokrasia, huo ni udhalimu, na sasa ni wakati wake kukoma."
source:- Bofya

Kipande hiki kimenivutia zaidi kwa sababu kinaashiria sisi tuendako na sasa imefikia wakati naogopa na kuchelea kama JK na utawala wa CCM wanaweza kumaliza miaka minne ilobakia wakiwa ktk uongozi. Na maadam kuna uwezekano mkubwa wa CCM kukataa kuachia madaraka basi kuna uwezekano mkubwa wa kutokea maafa. maafa ambayo hakuna Mtanzania anayaombea ingawa sasa hivi dalili zote zipo.

Ni kutokana na hali hii leo hii najiondoa ktk uchama, kuendelea kupingana na JK pamoja na uongozi wa CCM hali bado kuna miaka minne mbele kufikia uchaguzi ujao...muda huu ni mrefu sana kwa wananchi kuendelea kuishi katika shida, adha na mateso makubwa kutokana na makosa ya kuhadaika waloyafanya kuirudisha CCM ktk madaraka.

Natumia maneno ya Mwanakijiji ya kwamba - Katika wakati mgumu, maamuzi magumu hutakiwa - Desperate times calls for desperate measures! na hakuna wakati ambao wananchi wako desperate kama wakati huu ambao tunaona nchi ikididimia utadhani ile meli ya Titanic!..


Nimepitia ushauri wa wengi na kuona bado ushabiki wa vyama unatumika sana ktk kujenga hoja lakini tumeshindwa kutazama WATU na MAZINGIRA ili kutafuta ufumbuzi wa haraka na wenye lengo la kuokoa jahazi hili. na wala Watanzania msidanganyike kwamba JK na CCM ndio watazama na meli hii na nyie mkapona kirahisi, kwa sababu Tanzania inazama KIUCHUMI ktk bahari kuu na hakuna vifaa vya kutosha kutuokoa sote kwa pamoja. Miaka minne ni mbali sana kuweza kuepuka ukweli unaojijenga taratibu kuunda husda kubwa baina ya viongozi kwa viongozi na zaidi ya hapo wananchi na viongozi..Siasa sio tena solution ya matatizo yetu ya Kiuchumi.


Ni katika mazingira haya ya kuwa desperate, ndipo nawatazama Watanzania wataweza vipi kuondokana na janga hili na nimekuja na njia moja pekee ambayo kama rais JK na viongozi wengine wote wataweza kunisikiliza pengine tunaweza kuziba tobo zinazoingiza maji kwa kasi kuizamisha meli hii..

Swala la Umeme ni moja ya matatizo makubwa ya uongozi wa CCM lakini sii mwisho wa matatizo. Mvua mwaka huu zimenyesha kuliko wakati wowote miaka 20 iliyopita lakini tunaambiwa hapakuwa na mvua za kutosha!.. sasa iwe kweli ama isiwe kweli swala ni kutafuta suluhisho la umeme nchini na kikubwa zaidi kuokoa Taifa ktk hali mbaya ya kiuchumi kwani tunazama kwa kasi ya ajabu.

Mtukufu rais na waheshimiwa viongozi wa CCM, waheshimiwa viongozi wa vyama vya Upinzani, wabunge na wawakilishi wetu ktk sekta tofauti nawaomba sana kuweka tofauti zenu pembeni na kuanza kulitazama janga hili kwa uchungu na uzalendo wa kuliokoa taifa kabla hatujaangamia..


Moja ya njia bora ambazo nimezitazama kulingana rasilimali tulokuwa nazo (watuna Mazingira) nimegundua kwamba tunaweza kuifanya kazi hii kwa pamoja. JK akubali kushirikiana na vyama vya Upinzani kuokoa jahazi hili. Ushirikiano mkubwa unatakiwa na rais kwa dharura hiyo achukue maamuzi magumu ya kuachana na siasa za magamba. Siasa za kupakana na kueneza udini, ukabila na kadhalika badala yake ashirikiane na Upinzani (bipartisan) ktk maamuzi ya uongozi wa nchi yetu kutoka ktk janga hili.

Haitakuwa muafaka kama ule wa CCM na CUF, na wala hapatakuwa na mkataba wa aina yeyote zaidi ya rais mwenyewe kuamua kutazama nje ya chama chake ili kuokoa jahazi hili. Na vyama vya Upinzani nao wakubali kushirikiana na JK ktk kutafuta ushauri na mbinu bora za kuliokoa taifa letu bila kujali tofauti za kiitikadi..najua CDM na vyama vyenye msimamo mkali watasema hawawezi kukaa meza moja na shetani lakini ktk hili namtaka shetani asilimu (abatizwe), akubali ujumbe wenye malengo ya kuwaokoa Taifa na wananchi KIUCHUMI, kisha mambo yakikaa vizuri arudi ktk imani yake.

Kwa kuanza na hatua za dharura rais JK amchague Dr.Slaa kuwa waziri mkuu haraka iwezekanavyo. na sii kwa sababu hakuna kiongozi kama Dr.Slaa ndani ya CCM bali hii ni kuondoa uhasama wa kishabiki wa vyama na udini ulokwisha jitokeza ili wananchi wapate kuwa pamoja ktk mtikisiko huu wa kiuchumi.. Na zadi ya hapo hatuna muda wala nafasi ya majadiliano makubwa ila bajeti ya vyama vya Upinzani ilitolewa na mh.Zitto irudishwe bungeni na kupitishwa ama ndiyo itumike kwa sababu ni bora zaidi na yenye nafasi kubwa ya kutuweka ktk hali nzuri kiuchumi.

Itaonekana kama ni wazo la kijinga ikiwa msomaji hatazingatia WATU na katika MAZINGIRA tuliyopo, JK hawezi kuachia ngazi na hakuna mtu atakaye ondoka ktk msemo ule wa tutabanana humuhumu!..Na hatuwezi kuijenga nchi yetu kwa makundi na ushabiki wa kisiasa tena, haya ni matokeo ya ubinafsi wetu kisiasa inatakiwa kurudisha ule msemo wetu wa kijamaa ya kwamba makuzi ya mtoto hutegemea kijiji kizima!..Na kweli mtoto wa kiafrika ni mtoto wa kijiji kizima, hali kwa wazungu jambo hilo haliwezekani kabisa!

Tukumbuke pia kwamba hata mwalimu Nyerere alikubali kuchukua mrengo ambao ktk imani yake hakukubaliana nayo kabisa lakini ilifikia wakati mgumu kiuchumi na maamuzi magumu yalichukuliwa..Nyerere aliachia ngazi, leo nachoweza kumwomba JK ni kubadilisha tu mfumo wa uongozi kwa muda huu ambao CDM wameonyesha uzalendo wa hali ya juu tofauti na ile dhana isemwayo kwamba JK anaangushwa na watendaji kazi wake. na maneno haya yamezungumzwa wakati Pinda akiwa madarakani na hakika nashindwa kuchomoa hata sifa moja ya mazuri alowezesha mh. Pinda. Ni mtu mzuri sana, mstaarabu lakini amekosa nguvu ya kauli ktk kufuatilioa utendaji kazi wa wizara zake.

Nakumbuka wakati wa mwalimu, waziri akiharibu huitwa IKULU kujieleza na huamrishwa palepale kuachia ngazi ama kuffuata maagizo alokabidhiwa tofauti na JK aliyewafuata mawaziri ktk wizara zao na kuwa breifed kana kwamba hakujua kilichokuwa kikiendelea. Na ktk safari zake karibu kila waziri alionekana kaboronga, lakini bado wanapata uetetezi toka kwa waziri mkuu ambaye binafsi naweza kusema ndiye mshauri mkuu wa rais ktk maswala ya utekelezaji..

Mwisho, nitwaomba tena viuongozi wangu, tuache mzaha na siasa za kupakana kwani denokrasia kwa kiasi fulani imetushinda.. Tumejenga Uhasama na uroho wa vyeo kuwa msingi wa maamuzi yetu hali nchi inazidi kudidimia, kesho tutakuja kuchinjana kama wanyama. UTULIVU na AMANI havikupatikana kwa kulaghai watu, ni matunda ya kazi ngumu ya ya ziada walioifanya viongozi waliotangulia tukiwa na chama kimoja...Demokrasia isiwe sababu ya kuvunja utulivu na amani kwa sababu viongozi waliopo madarakani wamekosa uzalendo na ari ya kuliendeleza Taifa ambalo leo hii halina dira sawa na jahazi linalofuata upepo kwa kutumia nyota...

Ni mtazamo wangu binafsi...
 
Mkuu mbona unajichanganya sasa. Kama umempa kura Kikwete na bado una-imani naye; mbona ameteua watu bomu (kutokana na mtizamo wako hapo juu). Je hii inakueleza nini kuhusu JK as a leader and the main decision maker? Je kwenye teuzi hizo alikua anaangalia nini kwa watu hao (aliwateua kwa madhumuni yapi hasa) ?

tatizo kaka ni suala la uadilifu. na uadilifu wa mtu huwezi kuujua mpaka umpe mamlaka. na wengine wakisha pewa mamlaka hujitahidi sana kufanya kama yaliyofanywa na Jairo.
 
Historia inatuhukumu bara la Afrika kutojifunza kutokana na makosa ya nyuma ama yetu wenyewe au ya wenzetu!
 
Back
Top Bottom