Kwan jamaa haon hali halis ya maisha ya watu wake mpaka aambiwe na wasaidizi wake? Huyo Njaa Kaya aliwahi kuulizwa na ktuo kimoja kikubwa cha television duniani kuwa kwanini nchi yake ni maskini wakati ina raslimali kibao, mjamaa akasema hajui! Sas kama hajui anagombea urais ili afanye nini kama hajui chanzo cha umaskini wetu? Hawez kufanya kitu kwa kuwa hata hajui kazi inayomfanya awe madarakani!
kaka wewe hapo ulipo kila kinachoendelea una kiona? Rais ni kiongozi wa taifa macho yake ni mawili tu hawezi kuona kila linaloendelea nchi nzima, ndio maana anateua watu wa kumsaidia katika kazi. sasa tatizo la msingi hapa ni uadilifu na uzalendo wa mteuliwa mmoja mmoja kitu ambacho JK hawezi kuwajua wote tabia zao, naamini wengine yeye huletewa majina tu huwa siyo rahisi eti JK wote aliowateuwa anawajua tabia zao, majina hayo yeye huletewa na wale anaohisa ni wasafi kumbe siyo na matokeo yake wanapopangiwa majukum hufanya ubadhirifu mkubwa sana na hujitahidi sana kuficha kupitia report zao. na mbaya zaidi na wale waliopewa mamlaka ya kukagua mazingira yanaonesha huhongeka kiurahisi na kuendelea kuuficha ukweli.