wananchi gani waliomchoka? labda hao ni wale ambao hata hawakumpa kura zao kwahiyo hao hatuwahitaji kwenye takwimu. Mimi kama mwananchi niliyempa kura yangu JK nawalaumu sana wale wapambe wanaokuwa pembeni ya \j\k all the time ambao hatukuwachagua, wanatumia nyadhifa zao kumficha raisi ukweli wa nini kinachoendelea. Pale serikalini watendaji wetu wanaonekana kuwa na makundi na wanaishi na makundi yako na matokeo yake hawafanyi isue zinzowagusa wananchi na hili kundi kubwa ni la wale wanaoteuliwa na rais yaani watendaji ktk wizara.
Katika hali ya kawaida nisingekugongea like, lakini umejaribu kusema jambo fulani pamoja na uwakala wako!
Swala la msingi ni je? Rais anachaguliwa ili awategemee 100% hao wanaosimama pembeni yake na wateule wake? Kama jibu ni ndio...........yeye tunamchagua wa nini sasa!!!
Kama anaowateua wanamfanya katuni, wanakwiba bila woga, wanamkenulia meno nae anasema good job!!...........yeye tulimchagua ili ateue majizi? au tulimchagua asiweze kusimamia hata kitu kimoja???
Kama amechaguliwa na aliowachagua ndo wanamuangusha.................Je, hata wale ambao hajawateua yeye kama wabunge.......wote wa Upinzani na wale wa chama chake wenye nia njema wanapomwambia ....mkuu, wanakudanganya haoooo!!! wezii haooo mkuu!!! kwa nini hasikii??? kwa nini mpaka apate aibu,...aaibishwe na wateule wake ndo anaanza kuhaha kwa kutoa majibu ya vijana wa Form One B shule ya secondary Ilembula?? Rahisi rahisi tu!!
Imagine............eti tatizo la umemem ni la ukame...........Basi, yani tumemchagua na yeye akachagua wasaidizi ile wafanye mambo kwa mzunguko wa dunia na jinsi Mungu na mawingu yatakavyopenda? Mvua za vuli zisiponyesha this year (ofcouse hatutegemei yeye akawe mawingu ili inyeshe!!) TOTAL BLACK OUT!!!
Viongozi wa CCM wanaoipenda nchi hii, ambao hawapo serikalini wako wapi? tuwasikie wakiwakemea wateule wa Kikwete? Wazee wa DSM wakwapi? au kwao umeme unawaka, mafuta ya taa wananua bei gani? Wao hawawezi kumuita Huyu waliyempa kura nyingi na kumwambia......Bwana mkubwa, tunaumia, wanatuumiza, wateule wako wanatukandamiza sisi huku wakineemeka wao!! fanya jambo hima!!
Sio kila siku litokeapo jambo la msingi kwa wananchi, anawaita wazee na kuwapa posho na kuanza kupiga mkwala..........wazee wampige mkwala pia basi!!
Hizi jumuia za wazazi wa CCM, wakina mama ziko wapi? wanafanya nini? au kazi yao ni kukutana kwenye mikutano mikuu na kupeana posho na MIPASHO TU!!!!
Inaniuma sana!!!! this guy need to act.............aanze na kuwa serious kwanza na aache kufikiri WTZ ni mapoyoyo!!!