Nimepita hapo leo kama nilivyoahidi jana , Kuna matatizo ya kiuongozi katika
Vijiji hivyo , Wengi wa wanavijiji wanamlaumu kiongozi mmoja wa chama
tawala eneo Kwa kupandisha Bei ya Maji Katika Gari moja ambalo huwa
linasambaza maji katika vijiji hivyo , Yaani maji yanachukuliwa Wami
wanauenda kuwauzia wanavijiji na wauzaji ndio hao viongozi wao , Kwenye
vijiji hivi pia kuna miradi ya maji inayofadhiliwa na NGO zingine lakini
sikuweza Kuwasiliana na NGO hizo kutokana na Muda wangu mchache , Lakini
wanavijiji wameonyesha kuamka na kutaka mabadiliko kwenye Eneo lao .