Wananchi Morogoro walivyoanika udhaifu wa serikali ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Morogoro walivyoanika udhaifu wa serikali ya CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Aug 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akionyeshwa madarasa ya Shule ya Msingi Singisa. Hii ni shule pekee ya katika kijiji hiki ambacho ni makao makuu ya tarafa na kata ya Singisa

  [​IMG]

  Ofisi ya Kijiji na Kata ya SINGISA Jimbo la Morogoro Kusini Katika Taswira.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akionyeshwa sehemu ya vyoo vya wanafunzi wa shule ya SINGISA

  [​IMG]

  Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi akiwa na wanakijiji wa SINGISA jimbo la Morogoro Kusini katika ofisi ya mwalimu wa shule hiyo  Operesheni Sangara zinazoendelea Morogoro bado zimeendelea kuwa chachu ya kuimarisha CHADEMA katika kila vijiji wanavyofikia. Picha hizi ni katika kijiji ambacho hakuna zahanati na kina shule moja tu ya Msingi yenye wanafunzi 398 na Mwalimu mmoja tu!!Wanafunzi wote wanakaa chini.

  Kijiji hiki ifahamike ndicho pia makao makuu ya tarafa na kata ya Singisa.(Kata ya Singisa ina vijiji 7). Makao Makuu ya Kata ndipo pia mwisho wa barabara, hivyo vijiji vingine sita havifikiki na vimetengwa kabisa kimawasiliano.
  Moja ya lalamiko kubwa la wananchi, wamekuwa wakichangishwa michango isiyo na idadi na serikali ya kijii huku wakiwa hawasomewi mapato na matumizi. Baada ya elimu hasa ya uraia na umuhimu wa haki yao hiyo iliyotolewa na CHADEMA, wanakijiji wameapa ndani ya wiki mbili wataitisha mkutano wa kijiji na kuwatimua madarakani viongozi wa kijiji baada ya kuenda kinyume na taratibu za kuendesha serikali ya kijiji.
   
 3. N

  Njele JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Choo cha wanafunzi hata gunia tu la kufunika mlango au kuezeka kwa nyasi mambo yameshindikana. Na hiyo ofisi ya Mwalimu Mkuu imeniacha hoi, nakumbuka siku nilipopita huku Tunduru karibu na kijiji cha Nakapanya na kuona mwalimu amevaa lubega akipuliza filimbi kuashiria wanafunzi kukusanyika kuanza ratiba ya siku ya shule, ofisi hii mwalimu mkuu kuvaa kandambili sitashangaa kwani mazingira yanaashiria hivyo maana kuvaa vizuri ni kwenda kujichafua.
   
 4. T

  THEJEWDA Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hiyo ndo ccm, sasa , vijana tusibaki kupiga kelele bila action, na action ya maana ni kuhakikisha tuna vitambulisho vya kupiga kura ili tuing'oe ccm 2015.
  Jitahidi uwepo kule ulikojiandikisha la sivyo sasisha (update) your voting card. Kwa pale ulipo.
   
 5. sindano butu

  sindano butu JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 478
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  CCM ni chama cha kutetea maslahi ya mapebari lakini CHADEMA ni chama cha wananchi kwasababu wanakubaliana na maombi ya wananchi.NACHUKIA CCM Kama nnavyochukia UCHUZI WA BATA. Chadema ni chama cha wananchi nasi chama cha wachache.MUNGU IBARIKI CHADEMA , MUNGU WABARIKI WATANZANIA.
   
Loading...