Mathias Byabato
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,020
- 691
Wadau.
Hivi una taarifa kuwa kwa sasa kuitwa 'nshomile' ni kama tusi? Je unajua mpaka sasa kuna baadhi ya watu wanagwaya kutumia majina yao ya asili mfano Kagera,Kigoma nk?
Kwa nini? ..wanaosababisha haya wako nje ya Mkoa wa Kagera wakifanya kazi zao na wakitaka kazi ziendelee wao wakiwa huko huko wanasajili NGOs za mfukoni ,au vikundi kisha wanasafiri hadi Bukoba 'eti' kujadili namna ya kusaidia Bukoba na Kagera ,eti wanapanga keleta mapinduzi ya kiuchumi Kagera. Vikundi hivi hufanya kazi hizi katika nyakati za kukaribia uchaguzi ndani ya CCM au uchaguzi Mkuu tu. baada ya hapo hutawaona tena wala kinachoitwa 'foundation'
Si kawaida yangu kuandika humu mara kwa mara baada ya mambo mnavyoyaona nchini hasa uhuru wa habari.
Nasikitika kwa nini vijana tena wasomi wanatumia elimu yao kuharibu Mkoa huu kupitia agenda za 'kijinga' kwa kuandaa matamasha na makongamano ya kutafuta kura za kisiasa na wakisha maliza wanatokomea.Wanatumia title ya 'BUKOBA' eti kujadili fursa za Missenyi,Kyerwa ,Muleba nk.
Naomba upitie hizi link kwanza
'Bukoba Mpya no 1'
'Bukoba Mpya no 2'
'Bukoba Mpya no 3'
Hayo ni makundi ya CCM na CDM kwa kila upande kuandaa matamasha ya malengo ya ya kutafuta namna ya 'kujiuza' kwa wananchi ila baadaye watimize malengo yao.
Waandaaji wengi 'HAWAISHI' au 'SI WAKAZI' wa Bukoba,wengine hawana hata viwanja hapa Bukoba,wanafikia kwa jamaa zao au hotelini,eti wanajadili namna ya kuendeleza Mkoa wa Kagera.
Nimeanza kuhudhuria makongamno haya tangu 2002 hapa hapa Bukoba na agenda huwa ni zile zile tu,wafadhili ni wale nk...
Nasikitika kwamba hadi naandika haya Mkoa wa Kagera unaporomoka kwa kasi kubwa kimaendeleo. Ukifika Bukoba mjini kisha ukawatazama hawa jamaa na tai zao unaweza kushangaa na kusikitika sana.
Nitaendelea....
Byabato
updates:July 2017
Mkuu wa Mkoa Kagera salum katika video hapo chini alikuwa akifungua moja ya komgamano liliandaliwa na kikundi kiitwacho 'Bukoba Mpya' ebu msikilize aliyosema.