Wananchi, Hivi nchi ni mali ya nani hasa?

Wananchi, Hivi nchi ni mali ya nani hasa?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
478
Reaction score
711
Kama kuna kitabu ningeshauri kila mwananchi akisome kwa sasa ni tamthilia ya "Animal Farm" ya George Orwell (1945)

Hii ni simulizi ya wanyama walioamua kuuasi na kuupindua utawala wa mkulima katili ili waishi maisha ya kijamaa yanayozingatia usawa walioyaita Animalism wakiwa na kauli mbiu ya "All animals are equal."

Baada ya kufanikisha mapinduzi na kuanza kujitawala wakawachagua nguruwe kuwa viongozi wao. Nguruwe waalipotwaa madaraka tu, wakaanzisha propaganda kueleza kuwa nguruwe ni bora kuliko wanyama wengine, mwishowe wakaanza kutenda mambo yale yale mkulima katili aliyokuwa akiwatendea wanyama. Wanyama walipowauliza nguruwe kulikoni, mbona hatuwaelewi? Wakawaeleza "All animals are equal, but some animals are more equal than others." Mwisho hakukuwa na tofauti kati ya mkulima katili na nguruwe.

Hii ni tamthilia yenye mafunzo mengi yanayoakisi hali halisi ya Afrika baada ya madai ya uhuru kutoka kwa wakoloni. Ni tamthilia iliyojaa masomo ya propaganda, power, na political systems. Mwisho inatuasa kuwa waangalifu na madaraka tunayowapa viongozi wetu kwani "Power corrupts, but absolute power corrupts absolutely."

Siku hizi kumeanza kusikika mwananchi mmoja akiwaambia wananchi wenzake kuwa nchi ina wenyewe, au mtatufanya nini, au mtake msitake, au ole wenu! Haya ni maneno yanayofikirisha sana! Hivi ni kweli nchi ni ya wananchi wote? Hivi ni kweli kuna usawa kati ya wanajiita wenyenchi na wanaoitwa wananchi? Au ndio wenye nchi are more equal than wanachi, kama ilivyokuwa kwenye animal farm?

Ni dhana inayokubalika kuwa haitoshi tu kusema tuna haki na usawa, ni muhimu pia haki na usawa kuonekana kwa wazi ikitendeka.

Ubaguzi na uonezi ni jambo la kawaida kama anayeonewa sio wewe wala mtu unayehusika naye, itakapotokea wewe kuwa kwenye kundi la kuonewa na kubaguliwa ndio utakapoiona ladha yake.

Rai yangu tusitoe majibu mepesi kwa maswali magumu yahusuyo ubaguzi, unyanyasaji, ukandamizaji na dhuluma katika nchi zetu. Mambo haya yanaua umoja wa kitaifa. Kama nchi ni yetu sote, ni jukumu letu sote kuona kuwa kila mmoja anapata haki sawa kwa mujibu wa sheria.
 
Kwa wanachotufanyia wazanzibar kwa kutumia ulafi wa wajinga walioko bara naapa ipo siku tutwalipa haya kisasi ni haki ipo siku. Kwamba mnamtoa mzee kibao mnamuua kama nguruwe, mnamuua mdude, Soka na kumkebehi warioba , mnauza bandari zetu, mnanyanyasa masai kisa mnaioga maji ya ikulu tena kwa Kodi zetu. Narudia kwa matendo haya huu muungano wenu sio tu haupo tutawafanyia jambo hamtasahau milele.
 
Kama kuna mwananchi 1 akiwa anatoka ofisini kwake au sehemu yoyote nusu saa kabla hajaondoka barabara zinafungwa na wananchi wote wanasimama hatuwezi kuwa sawa, ina maana viongozi wana haki kuliko wananchi wengine.

Kama wanaweza kuwapangia wananchi wenzao kile wanachoona wao kinafaa bila kuwashirikisha hao wahusika inamaana viongozi ni wa muhimu kuliko wananchi wengine. Hayo ndiyo mawazo yangu.
 
Andiko zuri. Fupi na linaeleweka. Mwandishi alipotumia nguruwe kama awe kiongozi wa wanyama alijua ulafi wa nguruwe.
The same kwa ccm.
 
Back
Top Bottom