LGE2024 Wananchi hawajajitokeza kujiandikisha ktk daftari

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Watu hawawezi kuendelea kuwa wajinga muda wote.
Haya maneno yako ni mazuri sana hapa.
Natamani wananchi hao hao wasiishie kwenye kususia kujiandikisha kupiga kura. Wakiishia kufanya hivyo maana yake CCM tunayo tena miaka mitano zaidi na pengine zaidi ya hapo.

Kama ujinga umewaondoka wananchi; tutegemee hatua ya ziada itakayo fuata baada ya kukataa kujiandikisha. Hiyo hatua iwe ni ya kuikataa kweli kweli CCM; hata ikitumia mabavu kubaki madarakani, wakatae.
Ikitokea hivyo, hapo nami nitaelewa kuwa wananchi wametoka kwenye ujinga.
 
Uhamasishaji unahitajika
Swali ni nani afanye huo uhamasishaji?

CHADEMA wanapo itisha maandamano kwa sababu halali kabisa wananchi wanashindwa kujitokeza kwa wingi kuunga mkono maandamano hayo.
Hapa tunaweza tusiwalaumu wananchi, kwa sababu ya vitisho vingi vinavyo fanywa na polisi.

Sasa wakati huu wa kujiandisha kuwa wapiga kura, ingetegemewa kwamba CHADEMA na asasi mbalimbali wangefanya juhudi kubwa kuwa elewesha wananchi kwamba hii ndiyo nafasi yao nzuri ya kutumia haki yao na uhuru wao kwa kupiga kura na kuwapata viongozi wanao taka wawaongoze.
Hata kama CCM wakipanga kufanya mizengwe katika uchaguzi; polisi hawataweza kuwaelekezea wananchi mitutu ya bunduki wakati wakienda kupiga kura kwa wingi wao.

Kwa nini fursa hii wananchi hawaambiwi kuwa ipo na wanaweza kuitumia?
Bila shaka mkuu 'Proved' utakuwa umenielewa ni nani hasa wa kulaumiwa.

Kusema kweli inanishangaza sana kwa nini mambo yana kwenda hivi sasa hivi kama yalivyo. Nilitegemea hivi vyama vya upinzani vingekuwa kwenye kazi kubwa sana wakati huu; lakini ni kinyume kabisa, CCM ndio wanao onekana kufanya wanayo taka yafanyike. Ni ajabu sana.
 
Walimu wanatia huruma katika hivyo vituo.
Serikali ijitafakari.

Mwis
Ukiskia watu wamechafukwa mtaani huwezi amini

Leo jilani yangu ananiambia wakitaka nika vote wanipe hela ya kupotezea mda nimeshindwa kumwelewa alikuwa Ana maana gani

Nimejikuta na mwitikia tu eti eeeh?? Akqni jibu hivohivo.,

kikauzu Kama tuna ugomvi
 
Back
Top Bottom