Wanamuogopa Mzungu kuliko Mungu, wanajiibia wenyewe kura

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
WANAMUOGOPA MZUNGU KULIKO MUNGU, WANAJIIBIA WENYEWE KURA

Jana nimemsikiliza mama Anna Makinda. Alizungumza jambo la msingi sana. Aliwakumbusha wabunge kuwa mtu yeyote anayedharau au kuombea nchi yake balaa hudharaulika hata kama wanaomsikiliza wanatabasamu! Akatoa mfano wa nchi ya Marekani. Watagombana wee ndani ya Congress na Senate, watashitakiana, watakejeliana na kupingana nchini kwao lakini kamwe hutamuona mmarekani kaenda nchi nyingine kuikashifu au kuitakia mabaya nchi yao. Wakiwa nje utawasikia wakiimba kwa jazba "USA, USA, USA"! Na Ile wako uikashifu nchi yao.

Na kwa hakika hata nchi nyingi za Afrika watazozana ndani lakini nje ya nchi yao hutasikia wakiikashifu nchi yao.
Sasa njoo Tanzania.

Kuna wanasiasa na wanaharakati wa ajabu mno. Wanafunga safari kwa dhamira ya kwenda kuikashifu na kuitakia mabaya nchi yao! Na hawana soni! Wanatangaza kabisa kana kwamba wanaenda kutuletea chakula.

Imekuwa kwao ni sifa! Wanadhani tabasamu za wanaowasikiliza ni ishara kuwa wanatenda jambo la maana sana! Kumbe wanajidharaulisha. Leo hii Trump anashitakiwa lakini hatujamuona mtu yeyote kutoka democratic party akizurura duniani kutaka Marekani inyimwe misaada au kuelezea mabaya ya Marekani.

Nathubutu umkashifu rais wao uone!

Wanasiasa na wanaharakati wetu uchwara wao wanasusa uchaguzi lakini wanapata muda na fedha kwenda kuitukana nchi yao nje! Kwenda kuzuia msaada wa kusomesha watoto wa kitanzania! Na wanajisifuu utadhani watoto wanaocheleweshewa msaada wa elimu ni kutoka nchi nyingine! Ni watoto na wazazi wao haohao ambao mwezi oktoba wapinzani watataka kura zao! Unaenda kumuomba mtu kura ambaye ulikataa asisomeshwe au mwanae asisome kwa kuwa mashoga hawaruhusiwi.

Basi ajabu ni sababu wanazotoa kwa wazungu. Nadhani hata wazungu wenyewe wanawashangaa! Moja ya sababu ni haki za mashoga! Yaani wanaona haki za mashoga ni za maana mno kuliko haki za watoto wa kike wa kitanzania kupata elimu! Masikini sijui wanadhani wazungu woote ni mashoga au mashabiki wa ushoga?

Sababu nyingine ni kuwa eti vyuo vya elimu ni vyuo vya CCM! Hawajui wanaowaambia wengine wamewahi kuishi na kufanya kazi nchini. Wanasahau kuwa benki ina mwakilishi mkazi anayeelewa kwa undani mfumo wa vyuo nchini.

Lakini kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu, hakuna neema kwa chama tawala kama hii. Wapinzani uchwara wanairahisishia CCM kazi mbele ya wapiga kura! Ambacho CCM inatakiwa kufanya ni kuwaeleza wapiga kura jinsi wapinzani wanavyofanya juhudi za kukwamisha maendeleo yao nje ya nchi.

Pia iwaeleze kuwa wapinzani wanafanya hivyo ili kutetea watoto wa kike waruhusiwe kubeba mimba mashuleni na ili ushoga uruhusiwe.

Iwaeleze kwa kifupi tu jinsi wapinzani wanavyomuogopa mzungu kuliko Mungu.

Oktoba njia nyeupe kwa CCM!

NB: Kikao cha benki jumanne wiki hii hakikuahirishwa Kwa kuwa wapinzani waliandika barua bali ni kwa kuwa mjumbe mmoja aliomba kiahirishwe kwa kuwa ana udhuru. Wasipotoshe. Siku moja kabla mwakilishi mkazi alikutana nao na aliwaeleza bayana kuwa benki haioni sababu za msingi za kuzuia mkopo.

Nadhani wapinzani hawa hawajapima. Tukubali mkopo utazuiwa. Je CCM ikiwaeleza wananchi kuwa watoto watakosa elimu kwa kuwa wapinzani wamezuia mkopo ni nini kitafuatia? Halafu watadai wameibiwa kura! Kura wanajiibia wenyewe muda huu!
 
Mnalilia mkopo kama mmekatwa mikono?
Na wapinzani wakiwaambia wananchi kwamba serikali, nasema serikali sii nchi inakusanya kodi zaidi ya trilion moja lakini wanashindwa kuwasomesha watoto wetu mtapata kura?
Mtu muzima mukichwa hutoa kauli kwa kutizana pande zote mbili za shilingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii post mtu akisoma pasipo kuweka uccm wala Upinzani atatoka na kitu.
Waafrika na Waarab wanapelekeshwa sana na wazungu ila sio Iran japo mapandikizi yalishawekwa huko tayari

Huwezi kusema udhaifu wa kwenu kwa majirani eti upate credit.
Wanaharakati, wapinzani uchwara isipokuwa Mbowe na aina zake hao hawatakaa wachukue nchi japo watatumika kuleta machafuko
 
Asante sana mkuu. Umetoa points tupu. Hakuna ulicho kisahau.

Wapinzania wamejipanga vibaya sana sana.
 
Hii post mtu akisoma pasipo kuweka uccm wala Upinzani atatoka na kitu.
Waafrika na Waarab wanapelekeshwa sana na wazungu ila sio Iran japo mapandikizi yalishawekwa huko tayari
Huwezi kusema udhaifu wa kwenu kwa majirani eti upate credit.
Wanaharakati, wapinzani uchwara isipokuwa Mbowe na aina zake hao hawatakaa wachukue nchi japo watatumika kuleta machafuko

Sent using Jamii Forums mobile app
They will never do that!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Mama anafuatilia Trump anavyoi sabotage Marekani nje kwa Putin ili aendelee kuwa rais tu?
 
Umesahau kuandika hivi: huko USA HAKUNA anaezuiwa kufanya mikutano ya siasa wala kubambikizia wapinzani kesi. Huko USA wana tume huru za uchaguzi na matokeo (yakiwemo ya urais) yanapingwa mahakamani (na mahakama zao ni huru kabisa).
Umesahau kuandika kuwa huko USA Rais haabudiwi kama anavyotaka jiwe.

TUNADHARAULIWA ZAIDI kwenye hayo uliyoyakwepa kuliko uliyoyaandika.
 
Kama tunaweza kuwa na Spika ambaye hajui tofauti ya nchi na serikali basi tuna tatizo kubwa sana.
Wakati wakina Lule, Binaisa na kina Museveni waliposikia kilio chao kuhusu Amin kwa nini Nyerere asiwadharau kuwa wanaichukia nchi yao Uganda na kuwapotezea?
Aliamua kuwasaidia hao walioipenda nchi yao na kuichukia serikali ya Amin (kama ilivyo serikali ya CCM) ili kuiondoa madarakani.
Mbona wakati wa JK hakuna aliyekimbilia nje kueleza maovu ya serikali? Ni kwa vile Uhuru wa kujadili mustakabali wa nchi ulikuwepo na haukuwa uadui wa kupigana risasi eti wasaliti, kutekana na kutesana, kuuana na kupotea.
Huu wa WB ni mwanzo mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom