Wanamichezo waenda uchina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanamichezo waenda uchina

Discussion in 'Sports' started by Yona F. Maro, Sep 22, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Watanzania wengi haswa wale wapenzi wa mpira wa miguu haswa kandanda wamekuwa wakijiuliza ni lini wachezaji wetu wataenda kucheza nchi za watu katika ligi mbali mbali za kulipwa ?

  Jibu hilo limeanza kupatikana leo hii baada ya wachezaji wawili nizar khalfan pamoja na waziri mahadhi kuruka na ndege kuelekea uchina kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa huko kwa mkataba wa miaka miwili .

  Wachezaji hawa wamepatikana baada ya muda mrefu wa kunolewa na makocha wao pamoja na wadau wengine wa mchezo huo wa soka , timu watakayoenda kucheza inamilikiwa na Bolton wonderers ya uingereza .

  Vijana hawa wamepelekwa na mradi wa champion ambao kwa asilimia kubwa unafadhiliwa na klabu za uwingereza , mradi huu ulikuwa ukirusha vipindi vyake mara kwa mara katika televisheni ya ITV .

  Watu wengi haswa waandishi wa habari na wapiga picha walikuwa hapa uwanja wa ndege kwa ajili ya kuhojiana na vijana hawa pamoja na wadau wengine wa michezo , wanaamini vijana hawa watafanya maajabu

  Tuwaombee mengi na mafanikio vijana wetu wa kitanzania .
   
Loading...