Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa ADF waua watu 17 Mashariki mwa DRC

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
1678700359107.png

Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa ADF, jana Machi 12, 2023 waliwauwa takriban watu 17 Mashariki mwa DRC, maafisa wa eneo hilo wamesema, siku chache tu baada ya kundi hilo lenye mafungamano na kundi la kigaidi kufanya mauaji mengine katika eneo hilo lenye machafuko.

Kundi hilo la Allied Democratic Forces (ADF), ambalo kundi la Islamic State linadai kuwa ni mshirika wake wa kati kati mwa Afrika, ni mojawapo ya wanamgambo mashariki mwa Congo, wanaotuhumiwa kuwaua maelfu ya raia.

Shambulizi la hivi karibuni lilitokea asubuhi ya Jumapili huko Kirindera katika Jimbo la Kivu Kaskazini eneo la Beni, kulingana na chifu wa kijiji Katembo Kahongya.

"Tuna watu 17 waliofariki na wanne wamejeruhiwa," aliiambia AFP, akiongeza kuwa wanamgambo hao pia wamechoma majengo.

Walitumia silaha za mapanga na moto kuwaua watu," Kahongya alisema.

Aliyekuwa Gavana wa Kivu Kaskazini, Carly Nzanzu Kasivita pia alitweet kwamba watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa ADF walikuwa wamewaua watu 19 katika kijiji hicho, akibainisha kuwa idadi hiyo ilikuwa ya muda tu.

Mkazi wa Kirindera, Mukondano Kambale alisema wanamgambo hao waliwaua watu katika hoteli na zahanati ya afya kabla ya kufukuzwa.

_______

Daesh-linked ADF group kills 17 in eastern DRC

The attack comes after suspected ADF rebels killed over 40 people in twin attacks on Wednesday.

Suspected ADF militants have killed at least 17 people in the eastern Democratic Republic of the Congo (DRC), local officials said, only days after the Daesh-aligned group conducted another massacre in the troubled region.

The latest attack occurred in the early hours of Sunday at Kirindera in North Kivu province's Beni territory, according to village chief Katembo Kahongya.

"We have 17 dead and four wounded," he told AFP, adding that the militants had also set fire to buildings. "They used bladed weapons and fire to execute the population," Kahongya said.

The Allied Democratic Forces (ADF), which the Daesh terror group claims as its central African affiliate, is one of the deadliest armed militias in eastern DRC, accused of slaughtering thousands of civilians.

Former North Kivu Governor Carly Nzanzu Kasivita also tweeted that suspected ADF fighters had killed 19 people at the village, noting the figure was provisional.

Continuing violence
Kirindera resident Mukondano Kambale said the militants killed people in a hotel and health clinic before being chased away.

"It's fear and desolation in the centre of Kirindera," he said.
The attack comes after suspected ADF rebels killed over 40 people in twin attacks in neighbouring North Kivu villages on Wednesday, according to officials and residents.

A joint Congolese-Ugandan military operation targeting the militia in the eastern DRC has been underway since late 2021, but attacks have nonetheless continued.

Last week, the United States offered a reward of up to $5 million for information concerning ADF leader Seka Musa Baluku.

Source: TRT World
 
Back
Top Bottom