Wanakijiji wasimulia mkasa wa wazazi waliojiua Tabora baada ya kukosa hela ya matibabu ya mtoto wao

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,327
6,850
Source: https://www.mwananchi.co.tz/habari/...iua-Tabora/1597296-5064562-15iqsdb/index.html

Wanakijiji wasimulia mkasa wa wazazi waliojiua Tabora

Source: https://www.mwananchi.co.tz/habari/...iua-Tabora/1597296-5064562-15iqsdb/index.html

Tabora. Amina Juma na Kanuno Tano wanaweza kuwa wameondokana
na machungu ya kumuona mtoto wao mdogo akiteseka kwa ugonjwa wakati hawana uwezo wa kifedha kwa ajili ya matibabu yake, lakini hatua yao ya kujiondoa uhai ni mwanzo wa matatizo makubwa zaidi kwa
waliowaacha.
Amina (18), alitangulia kujitoa uhai kwa kunywa dawa tofauti baada ya kuona anashindwa kuvumilia kumuona mwanaye akiugua huku akishindwa kumudu fedha za matibabu na mumewe Tano (22), akajinyonga muda mfupi baadaye akisema hawezi kuishi bila ya mkewe.

Marehemu Amina na Tano walizikwa nyuma ya nyumba yao Aprili 6, 2019. Vifo hivyo na sababu zake vimeacha simanzi na maswali mengi, huku wakazi wa Kijiji cha Kigombe wilayani Tabora wakitafakari hatua inayofuata kwa watoto wao wawili, mkubwa akiwa na umri wa miaka minne kutokana na hali yao ya kiuchumi kutokuwa nzuri.

Baadhi wanaona hatua ya wawili hao kujiua imetokana na msongo wa mawazo. “Walikuwa na msongo wa mawazo uliotokana na kukosa zaidi ya Sh2.6 milioni zinazohitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto wao Chiku Kudona,” alisema Adam Kalonga, babu wa Amina wakati alipozungumza na Mwananchi jana.

“Walitakiwa wamrejeshe mtoto wao Hospitali ya (Rufaa) ya Bugando miezi miwili baadaye. Lakini sasa ni miezi mitano imepita.”

Walipokwenda mara ya kwanza kwa ajili ya matibabu ya mtoto wao, wawili hao walitumia zaidi ya Sh320, 000.

“Kukosa fedha za matibabu huku mtoto akiendelea kutaabika kwa maradhi
kuliwaumiza Amina na mumewe Tano. Mara kwa mara Amina alikuwa akilia kila alipomwangalia mtoto wake mgonjwa anavyoteseka,” alisema Kalonga.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Gombe One, Gerson Maganga alisikitika kwa jinsi ambavyo kijiji kilishindwa kuchukua hatua baada ya wawili hao kutoa taarifa ya matibabu ya awali na mahitaji yaliyotakiwa kwa ajili ya kurudi Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.

“Waliporejea kutoka Hospitali ya Bugando, waliujulisha uongozi wa kitongoji mahitaji ya fedha kwa ajili ya matibabu ya mtoto wao, lakini kwa bahati mbaya hawakusaidiwa,” alisema Maganga.

“Hatukujua kama hali ingefikia hapo ilipofika. Tunaomba Mungu atusamehe kwa kushindwa kufanya jambo ambalo pengine lingeokoa maisha ya wanandoa hawa walioamua kujitoa uhai kutokana na ugonjwa wa mtoto wao.

“Tunawaomba Wasamaria wema wajitokeze kusaida matibabu ya mtoto huyu.”
Kuhusu maisha yao, Maganga alisema enzi za uhai wao, ndoa ya Amina na Tano ilikuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi walivyoishi kwa amani na ushikirikiano katika kila jambo.

“Wamedumu kwenye ndoa kwa miaka mitano pekee na walikuwa vijana wadogo,lakini walikuwa miongoni mwa familia za mfano katika kitongoji chetu,” alisema Maganga.

Lakini kazi inayowasubiri ndugu, jamaa na wakazi wengine wa kijiji hicho ni malezi ya watoto hao wawili na matibabu ya Chiku.
Akizungumzia malezi ya watoto hao yatima, Chiku Shaaban ambaye ni mama mzaziwa Amina, aliwaomba wasamaria wema kujitokeza kumsaidia kuwalea nakuwahudumia.

“Tutakuwa na wakati mgumu kuwalea na kuwatunza watoto hawa kutokana na umriwao na ugonjwa wa mtoto mdogo. Tukisaidiwa tutashukuru Mungu,” alisema Chiku.


Source: https://www.jamiiforums.com/threads...aloutoa-ila-huu-ni-ushauru-wangu-pia.1318003/
 
Serikali inayo wajali wanyonge, watoto chini ya umri wa miaka mitani wapatiwe matibabu BURE, hakika kuishi nchi za propaganda ni taabu sawa na kuishi nchi zenye vita live live.
serekali ni watu na watu ni serekali.hata wewe unaweza kuwa serekali ya jamii yako kuwezesha zaidi hiyo serekali kutambua kuwa kuna watu wana uhitaji wa hicho unacho kisema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma uzi na machozi yakinilenga ndani ya macho yangu.
Wa tz tunaroho gani jamani.
Mbona kumbi za starehe tunamwaga sana hela.
Tusaidiane jamani.
Yaani daaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umri wao ni sababu kubwa zaidi ya hayo maradhi,mke miaka 18 kuhimili msongo ni kazi bahati mbaya familia yake si ajabu nao hawakuliona hilo.Hapo ndipo swala la mwenzie linapokuja kuwa na nguvu mmoja lazima awe strong kumshika mkono mwenzie kwenye misukosuko kama hivyo,wameenda halafu mgonjwa kabaki na nani?pengine wazazi wake ndio faraja ya mwisho kwa mtoto!Mungu awasamehe!
 
Serikali iwe na mifuko maalum ya kusaidia wasiojiweza, tofauti kabisa na bima ya afya maana si wote huko vijijini wanauwezo wa kujiunga na bima, au wafanye bima kuwa lazima kwa kila mtz.

Hii inatia uchungu mno jamani, daah...!!!
 
Daaahh kama kuna MTU anajua namna tunaweza wasaidia hao watoto aweke hapa.Japo halingumu lakini tunatofautiana kwakweli,huku Ndugai anaweza tumia zaidi ya billion 5 kwa matibabu yake India,lakini familia hii masikini imekosa 2.6mil na wazazi wakakosa matumaini kabisa mpaka kuamua kuondoa uhai wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jamani c wanasema watoto bure matibabu?
au ndvyo serikali ya wanyonge ilivyo?
 
So sad, si kosa lao, ni walifikia mwisho wa kuhimili changamoto iliyowakumba umri wao pia ukiwa kigezo kikubwa.
Pamoja na kusoma post yote sijaona huyo mtoto alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani, ila yote kwa yote Mungu atoaye faraja ambayo hakuna mwanadamu anaweza toa awatunze hao watoto, wakue vyema, wafurahie maisha kama watoto wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…