Wanakijiji wasimulia mkasa wa wazazi waliojiua Tabora baada ya kukosa hela ya matibabu ya mtoto wao

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,474
2,000
Source: https://www.mwananchi.co.tz/habari/...iua-Tabora/1597296-5064562-15iqsdb/index.html

Wanakijiji wasimulia mkasa wa wazazi waliojiua Tabora

Source: https://www.mwananchi.co.tz/habari/...iua-Tabora/1597296-5064562-15iqsdb/index.html

Tabora. Amina Juma na Kanuno Tano wanaweza kuwa wameondokana
na machungu ya kumuona mtoto wao mdogo akiteseka kwa ugonjwa wakati hawana uwezo wa kifedha kwa ajili ya matibabu yake, lakini hatua yao ya kujiondoa uhai ni mwanzo wa matatizo makubwa zaidi kwa
waliowaacha.
Amina (18), alitangulia kujitoa uhai kwa kunywa dawa tofauti baada ya kuona anashindwa kuvumilia kumuona mwanaye akiugua huku akishindwa kumudu fedha za matibabu na mumewe Tano (22), akajinyonga muda mfupi baadaye akisema hawezi kuishi bila ya mkewe.

Marehemu Amina na Tano walizikwa nyuma ya nyumba yao Aprili 6, 2019. Vifo hivyo na sababu zake vimeacha simanzi na maswali mengi, huku wakazi wa Kijiji cha Kigombe wilayani Tabora wakitafakari hatua inayofuata kwa watoto wao wawili, mkubwa akiwa na umri wa miaka minne kutokana na hali yao ya kiuchumi kutokuwa nzuri.

Baadhi wanaona hatua ya wawili hao kujiua imetokana na msongo wa mawazo. “Walikuwa na msongo wa mawazo uliotokana na kukosa zaidi ya Sh2.6 milioni zinazohitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto wao Chiku Kudona,” alisema Adam Kalonga, babu wa Amina wakati alipozungumza na Mwananchi jana.

“Walitakiwa wamrejeshe mtoto wao Hospitali ya (Rufaa) ya Bugando miezi miwili baadaye. Lakini sasa ni miezi mitano imepita.”

Walipokwenda mara ya kwanza kwa ajili ya matibabu ya mtoto wao, wawili hao walitumia zaidi ya Sh320, 000.

“Kukosa fedha za matibabu huku mtoto akiendelea kutaabika kwa maradhi
kuliwaumiza Amina na mumewe Tano. Mara kwa mara Amina alikuwa akilia kila alipomwangalia mtoto wake mgonjwa anavyoteseka,” alisema Kalonga.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Gombe One, Gerson Maganga alisikitika kwa jinsi ambavyo kijiji kilishindwa kuchukua hatua baada ya wawili hao kutoa taarifa ya matibabu ya awali na mahitaji yaliyotakiwa kwa ajili ya kurudi Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.

“Waliporejea kutoka Hospitali ya Bugando, waliujulisha uongozi wa kitongoji mahitaji ya fedha kwa ajili ya matibabu ya mtoto wao, lakini kwa bahati mbaya hawakusaidiwa,” alisema Maganga.

“Hatukujua kama hali ingefikia hapo ilipofika. Tunaomba Mungu atusamehe kwa kushindwa kufanya jambo ambalo pengine lingeokoa maisha ya wanandoa hawa walioamua kujitoa uhai kutokana na ugonjwa wa mtoto wao.

“Tunawaomba Wasamaria wema wajitokeze kusaida matibabu ya mtoto huyu.”
Kuhusu maisha yao, Maganga alisema enzi za uhai wao, ndoa ya Amina na Tano ilikuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi walivyoishi kwa amani na ushikirikiano katika kila jambo.

“Wamedumu kwenye ndoa kwa miaka mitano pekee na walikuwa vijana wadogo,lakini walikuwa miongoni mwa familia za mfano katika kitongoji chetu,” alisema Maganga.

Lakini kazi inayowasubiri ndugu, jamaa na wakazi wengine wa kijiji hicho ni malezi ya watoto hao wawili na matibabu ya Chiku.
Akizungumzia malezi ya watoto hao yatima, Chiku Shaaban ambaye ni mama mzaziwa Amina, aliwaomba wasamaria wema kujitokeza kumsaidia kuwalea nakuwahudumia.

“Tutakuwa na wakati mgumu kuwalea na kuwatunza watoto hawa kutokana na umriwao na ugonjwa wa mtoto mdogo. Tukisaidiwa tutashukuru Mungu,” alisema Chiku.

Nampongeza sana Mh. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa kwa moyo wa upendo aliouonyesha kwa ndugu yetu huyu anayeitwa Ernest Masenga kwa kumpa jumla ya Shillingi Million Kumi (10,000,000/=) Kwa ajili ya matibabu.

Mbali na hiyo nina wazo pia ambalo ningependa kuwashirikisha watanzania wote kwa ujumla, na Serikali pia kupitia Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu mwenyewe.

Wazo langu linalenga kumudu kabisa gharama za mahitaji ya dharura ya matibabu kwa watu wasiokuwa na uwezo, popote pale walipo nchini Tanzania, NA PIA walio na uwezo lakini wamekumbwa na dharura ya ghafla mno na inayohitaji pesa nyingi sana ya ghafla. Hii hasa nimekuja kuifikiria baada ya kuona kuwa Matibabu ya Ndugu yetu Mh. Tundu Lissu, yamefikia hadi Million mia moja (100,000,000/=). Wazo langu liko hivi katika ushauri:

KAMA KUNA UWEZEKANO TUSEME KWA MFANO:
(i). Wizara ya Afya ipeleke mswaada Bungeni ikiiomba kila Mtanzania aliyeko kwenye PAYROLL ya serikali akatwe kwenye mshahara wake Shs Elfu moja tu (1,000/=) kwa mwezi. (watu wengine na wafanyabiashara wakubwa kama akina Mh. Reginald Mengi, Bakhresa na wengineo wao wanaweza kuombwa washiriki pia kwa namna watakayoona wenyewe, KWA HIARI YAO, na mfanyakazi mwingine yeyote asiyekuwa wa Serikali anaweza kuchangia KWA HIARI YAKE kama anvyoona mwenyewe inafaa


(ii). Pesa inayotokana na makato haya iunde MFUKO MAALUM kwa ajili ya Matibabu ya Dharura kwa watu wasiojiweza, au hata wala wanaojiweza lakini dharura zinazowapata zinahitaji hela nyingi na ya haraka sana kama ilivyotokea kwa mpendwa wetu ndugu yetu Mh. Mbunge Tundu Lissu. Mfuko huu uwekwe chini ya aidha Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu au Wizara ya Afya

Tuseme wafanyakazi Tanzania ni laki tatu (3) tu (300,000/=) sasa angalia takwimu zifuatazo:

  1. Watu hawa 300,000 wakichangia 1,000/= KWA MWEZI, jumla ya Pesa itakayopatikana ni million mia tatu (300,000,000/=) kwa MWEZI MMOJA tu.
  2. Wakichangia 1,000/= KWA MWAKA, jumla ya Pesa itakaypatikana ni million ELFU TATU NA MIA SITA au tuseme Billion tatu nukta sita (3,600,000,000/=) kwa MWAKA MMOJA tu.
Hili wazo tukilifanyia kazi tukaliweka kwenye vitendo, ndani ya mwezi mmoja tu, vipindi kama vile HADUBINI pamoja na MIMI NA TANZAIA, tutavitumia kwa maswala mengine ya kijamii lakini si kwa ajili ya kuomba wasamria wema wajitokeze kwa ajili ya msaada wa matibabu.

Tofauti na hivyo, hatutakuwa na PERMENENT SOLUTION ya hili tatizo, tutakuwa nalo hata baada ya miaka 200 ijayo, halitaisha. Vipindi vya kwenye TV kwa ajili ya kuomba wasamaria watoe msaada, havi-provide PERMANENT SOLUTION. Tutaendelea hivi mpaka lini na hawa watu wapo wengi?

Kwa wazo hili kama ikitokea mfuko umekua, hela hii inaweza hata ikwa inatwanywa kwenye Mahospitali ya Wilaya, kwa ajili ya kutibu wagonjwa walioko huko wenye matatizo special kama nilivyosema hapo awali.

Natamani sana ujumbe wangu huu umfikie kiongozi yeyote yule aliye na mamlaka ya maamuzi serikalin. Natanguliza shukrani zangu!

Source: https://www.jamiiforums.com/threads...aloutoa-ila-huu-ni-ushauru-wangu-pia.1318003/
 

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
3,438
2,000
Serikali inayo wajali wanyonge, watoto chini ya umri wa miaka mitani wapatiwe matibabu BURE, hakika kuishi nchi za propaganda ni taabu sawa na kuishi nchi zenye vita live live.
serekali ni watu na watu ni serekali.hata wewe unaweza kuwa serekali ya jamii yako kuwezesha zaidi hiyo serekali kutambua kuwa kuna watu wana uhitaji wa hicho unacho kisema

Sent using Jamii Forums mobile app
 

vitz14

Senior Member
Dec 27, 2013
112
250
umri wao ni sababu kubwa zaidi ya hayo maradhi,mke miaka 18 kuhimili msongo ni kazi bahati mbaya familia yake si ajabu nao hawakuliona hilo.Hapo ndipo swala la mwenzie linapokuja kuwa na nguvu mmoja lazima awe strong kumshika mkono mwenzie kwenye misukosuko kama hivyo,wameenda halafu mgonjwa kabaki na nani?pengine wazazi wake ndio faraja ya mwisho kwa mtoto!Mungu awasamehe!
 

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
23,384
2,000
Serikali iwe na mifuko maalum ya kusaidia wasiojiweza, tofauti kabisa na bima ya afya maana si wote huko vijijini wanauwezo wa kujiunga na bima, au wafanye bima kuwa lazima kwa kila mtz.

Hii inatia uchungu mno jamani, daah...!!!
 

Tajiri mpole

JF-Expert Member
Apr 15, 2018
1,684
2,000
Daaahh kama kuna MTU anajua namna tunaweza wasaidia hao watoto aweke hapa.Japo halingumu lakini tunatofautiana kwakweli,huku Ndugai anaweza tumia zaidi ya billion 5 kwa matibabu yake India,lakini familia hii masikini imekosa 2.6mil na wazazi wakakosa matumaini kabisa mpaka kuamua kuondoa uhai wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

GEBA2013

JF-Expert Member
Feb 22, 2014
3,758
2,000
jamani c wanasema watoto bure matibabu?
au ndvyo serikali ya wanyonge ilivyo?
 

ISLETS

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
8,144
2,000
So sad, si kosa lao, ni walifikia mwisho wa kuhimili changamoto iliyowakumba umri wao pia ukiwa kigezo kikubwa.
Pamoja na kusoma post yote sijaona huyo mtoto alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani, ila yote kwa yote Mungu atoaye faraja ambayo hakuna mwanadamu anaweza toa awatunze hao watoto, wakue vyema, wafurahie maisha kama watoto wengine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom