WanaJF, sina mbele wala nyuma… ni mateso tu 💔🥀

WanaJF, sina mbele wala nyuma… ni mateso tu 💔🥀

Nyakati kama hizi humkuta kila mtu hasa wale wanaopambana sana,kusali sana na kujitahidi sana …hizi ni nyakati ambazo ni katikati ya kufanikiwa kwenye jambo lako na kupotea kabisa….! Hizi ni nyakati ambazo ukiendelea kukaza basi unatoboa na ukikata tamaa ndio basi tena! Hizi ni nyakati kama za pale unapokaribia kufika nyumbani halafu umebeba mzigo huwa mzigo unakuwa mzito zaidi!

Hivyo unachotakiwa ni kutrust process unayopitia endelea kukaza kaza nina hakika haitovuka mwaka utakuja kushuhudia hapa, kama una sali/swali kazana zaidi!

Nyakati za kukaribia kufanikiwa huwa ni nyakati za taabu sana zinaumiza na zina katisha tamaa sana na mara nyingi mtu huona ndio mwisho wake…lakini sivyo! Lakini kinachohitajika ni kuvumilia na kukazana zaidi na kutokata tamaa!

Kila anayetaka kufanikiwa au kufanikisha jambo fulani lazima apitie nyakati kama hizi ….zinakuwa za moto sana na mateso na hakuna njia unayo iona…lakini trust me njia utaiona …
Watu wanasahau hta akina Bakhresa kuna matanuri ya moto walipitia ndo wakawa vile...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom