WanaJF mliochangia uzi wangu kuhusu Ujenzi wa Coco Beach, Rais Magufuli amekisikia kilio chenu kuhusu Sh. 14 Bilioni

Lumumba fursa kila kona siyo hapo Ufipa mnagombania mishahara ya wabunge!!!........ Kazi afanye Sugu posho wagawane akina mrangi wapi na wapi?!!
Koko Beach ulisha jiandaa kukaa mguu Sawa naona

Ova
 
Kwenye ishu ya COCO beach JPM yuko sahihi sana
Ile ni beach ya wanyonge, kwenye sherehe za Iddi na Christmass wanyonge huenda hapo kujiburudisha, sasa ukianza kujenga mistructure ya kuwabana raia wasiingie, au kuwasegregate unakuwa umewadhulumu.
Kwani beach za Miami Costa Rica Hawaii Honolulu zikoje? Tunisia wazungu wanaokuja kupunga upepo Ni zaidi ya watalii was Kenya na Tanzania. We need to think big
 
OK, kwa hiyo kikao cha madiwani kupanga bajeti ya bilioni 14. 5 bashite ndio kawapangia iwe hivyo akiwemo halima mdee

Na ule mradi wa Mto Msimbazi bashite ndio anaukwamisha?

Machinjio ya Vingunguti billion 12.5 nayo amepanga bashite basi madiwani wote wa ukawa ni mizigo
Huyu Kaka na fukwe wapi jamani? Zaidi ya mbegani anajua wapi Tena? Huu mradi angepewa kadogosa mngeona vitu vya maana,
 
Kwani Wa morogoro alitumbuliwa kwa sababu ipi? Makonda, Mkuu Wa wilaya ya ilala na kinondoni pamoja na wakurugenzi wao na ma- DSO wanatakiwa ama kuondolewa au kuhamishwa na kushushwa cheo kwa uhusika wao Wa kadhia ya coco na machinjio ya vingunguti!
Awe fair kwa wote kwani Wa morogoro na wasaidizi wake na RPC wamemwagwa!

Yule ni muhimili kamili uliojichimbia ndani
 
Kuna mshkaji nimewekeana naye dau.

Anasema Makonda hamalizi mwezi, mimi nimemwambia anaumaliza na anabaki hapahapa.
 
Makonda kawa mpole balaa, sasa hivi kashajua mh rais hana utani kwenye kazi na haangalii sura. Alikua anadhani kumsifia sifia rais ndo ataachwa , akae mkao wa kazi.
 
Maajabu ya Magufuli na ubabe wake wote akifika kwa BASHITE anaufyata..! Raha sana!
Nimemzarau mmno!
Hivi hauelewi kabisa sababu za Makonda 'kusevu'?

Ni mambo mawili tu, la kwanza ni ule msingi imara aliojiwekea wa kuanzisha vita vya madawa ya kulevya.

Kisaikolojia Jpm anajizuia kufanya maamuzi kwa sasa, kwa sababu itaoneka matajiri wa unga na ma punda wameshinda vita.

Na Shavu la vita hivyo kwake litaendelea kumsetiri kwa kipindi kirefu mno.

Pili ni kwamba: Jpm anafahamu fika kwamba Makonda hahusiki kwa vyovyote na huo ufisadi wa ujenzi, viongozi wapigaji wanaochelewesha mambo kwa makusudi kwa ajili ya madili yao binafsi wanafahamika kwa majina.

Makonda angelikuwa kalambishwa chochote kwenye kashifa hiyo, angelifukuzwa bila samahani.

Kutajwatajwa huko ni kumtia tu presha ya usimamizi.

Na hapo upele umeota kwa mkunaji, kwanza juzi alifanya kikao cha utendaji na viongozi wote wa mkoa na usiku akaonekana Vingunguti anajenga!

Sasa tuone mambo yatakavyopelekwa!
Tusitabiri chochote, tusubiri kwanza.
 
MUNGU IBARIKI JAMIIFORUMS, MUNGU WABARIKI WOTE WANOTOA MICHANGO YA DHATI YENYE KULETA MABADILIKO CHANYA KATIKA NCHI YETU. MUNGU AWALAANI WALE WOTE WANAOKESHA USIKU NA MCHANA KUIPIGA VITA JAMIIFORUMS WAKATI NA WAO NI WANACHAMA WENZETU. AMEN.
jamii forums haipingwi na watu kama musiba,ila wale kuku waoitumia kutukana wakuu wa mamlaka matusi ya wazi.

wanaiweka kwenye shabaha ya muuaji.hii kichaka itapigwa rpg moja mambo yaharibike kabisa.
 
Back
Top Bottom