Buswelu
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 1,998
- 343
na Amana Nyembo
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), jana walivamia ofisi za Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam na Pwani (DAWASCO) zilizoko eneo la Ubungo Terminal jijini Dar es Salaam na kutoa kipigo kwa watumishi wa taasisi hiyo ya umma.
Tukio hilo lililosabisha kujeruhiwa kwa wafanyakazi wanne wa Dawasco lilitokea muda mfupi baada ya amri ya wanajeshi hao kutaka mabomba yao ya maji yaliyokatwa yakaunganishwe kukataliwa.
Dawasco ilichukua uamuzi wa kukata maji hayo juzi kama sehemu ya zoezi lake linaloendelea la kuwakatia maji wateja wake wote ambao hawalipii ankara zao. Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa JWTZ ni moja ya wadaiwa sugu wa Dawasco kwani inadaiwa kiasi cha sh milioni 276.
Vurugu hizo zilianza majira ya saa 4:00 asubuhi muda mfupi baada ya wanajeshi watano kufika katika ofisi hizo wakiwa katika gari lao aina ya Land Rover na wakawaamuru wafanyazi wa Dawasco kuondoka nao na kwenda kurejesha maji waliyowakatia juzi.
Akizungumza na Tanzania Daima jana alasiri, Meneja Uhusiano wa Dawasco, Badra Masoud alisema baada ya kuona jitihada hizo zikishindikana, wanajeshi hao waliwachukua kwa nguvu wafanyakazi watatu wa Dawasco katika gari lao na kuondoka nao hadi katika kambi ya Jeshi la Lugalo.
Walipofika Lugalo, wanajeshi hao walianza kuwapa adhabu za kuwaviringisha ardhini drill, na kuwarusha kichura kabla hawajawachukua tena na kuwarejesha katika ofisi zao za Ubungo majira ya saa 8:00 mchana.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wafanyakazi wa Dawasco, Samuel Massawe, ambaye alipata kipigo na kuumia sehemu za uso na mguu wa kulia, alisema kuwa wanajeshi hao walifika katika ofisi zao wakiwaamrisha wafanyakazi hao wawafungulie maji ambayo yalikatwa juzi.
Alisema kuwa, wanajeshi hao walisema wasipowafungulia maji watakwenda kufungua wenyewe katika mtambo wao mkubwa wa Ruvu Juu.
Massawe alisema kuwa baada ya wao kukataa agizo hilo, ndipo askari hao walipoanza kuchukua hatua za kuwapiga huku wakitumia virungu, hali iliyosababisha yeye na wafanyakazi wenzake watatu; Josephina Kombe, Malik Rajabu na Zuhura Salumu kujeruhiwa.
Alisema kuwa wakati wakijaribu kujinusuru kwa kupiga simu Makao Makuu ya Dawasco, wanajeshi hao waliwadhibiti na kuzichukua simu zao, kabla ya kuzirejesha muda mfupi baadaye.
Tukio hili lilisababisha maofisa wa Dawasco makao makuu kuwasili Ubungo majira hayo hayo ya saa 8:00 na muda mfupi baadaye wanajeshi hao wakiwa katika gari lao waliwasili tena hapo na wakaanza kuzozana na Ofisa Biashara wa Dawasco, Raymond Mndolwa.
Mzozo huo uliendelea kwa wanajeshi hao kumkamata Mndolwa na wakaanza kumvuta nje ya eneo kwa lengo la kuondoka naye, jitihada ambazo hata hivyo zilishindikana.
Baada ya kubaini kuwa tukio hili lilikuwa likirekodiwa na wanahabari, wanajeshi hao walimvamia mpiga picha wa gazeti la Mwananchi, Fidelis Felix na wakamnyanganya kamera yake baada ya kupiga picha zilizokuwa zikionyesha jinsi Mndolwa alivyokuwa akizingirwa na askari hao na kumvuta atoke nje ya ofisi.
Muda wote wakati wa mzozo huo, Mndolwa alikuwa akiwalaumu wanajeshi hao kwa kujichukulia sheria mkononi na kuwaumiza wafanyakazi ambao kimsingi hawakuwa na makosa yoyote.
Kama kuhusika na kukata maji ni mimi, na kama wanataka kumpiga mtu wanipige mimi na si nyinyi wafanyakazi na kama kila mtu akichukua sheria mkononi hii itakuwa nchi gani? Nimesikia wanataka kwenda kufungua mtambo wa Ruvu Juu, alisema Mndolwa.
Katika hali inayoonyesha kana kwamba kauli hiyo haikuwafurahisha wanajeshi hao, walimtaka Mndolwa atoke nje ya ofisi wakazungumze naye, hoja ambayo aliikataa.
Hatua hiyo ilisababisha mmoja wa wanajeshi hao kuwaamuru wenzake wamtoe nje kwa nguvu hali iliyosababisha kuanza kuvutana kabla ya hatua hiyo kugonga mwamba.
Kuona hivyo, Mndolwa aliamua kwenda kupanda gari ili aondoke eneo hilo juhudi ambazo hata hivyo zilikwama baada ya wanajeshi hao kukimbilia getini kulifunga wakimzuia kutoka.
Hatua hiyo ya wanajeshi iliyodumu kwa zaidi ya nusu saa ilisababisha watu washindwe kutoka au kuingia katika ofisi hizo kwa muda wote huo, kabla wanajeshi hao hawajaamua kuondoka.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Badra alisema tayari walikuwa wameshafungua faili la malalamiko polisi na kupewa hati ya watuhumiwa hao kukamatwa ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa.
Hata hivyo, katika hatua nyingine, Jeshi la Ulinzi jana lilitoa taarifa likilalamikia uamuzi huo wa Dawasco kulikatia maji jeshi na kutangaza taarifa hizo kupitia katika vyombo vya habari.
Katika taarifa hiyo, jeshi hilo linasema kiasi cha fedha kinachotolewa na serikali kwa ajili ya gharama za maji ni kidogo na kwamba bili zinazotolewa na Dawasco si sahihi na zinapaswa kuhakikiwa.
Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/2/23/habari1.php