Nyanya mbichi
JF-Expert Member
- Nov 10, 2011
- 3,716
- 2,220
Leo kuna foleni kali hasa kwa magari yatokayo ubungo kwenda buguruni.
Tulivyo vuka daraja la matumbi tukasikia kin'gora kumbe ni Magari ya wana jeshi yamebeba zana za kivita wanatumia barara itokayo buguruni kwenda ubungo wao wamefanya kinyume .
Sasa kuna gari zikawa zinakuja MP wakateremka ili magari yakae kando heee kumbe dereva wa gari ndogo alikua amepaki gari pembeni si mjeshi mmoja akaanza kumtandika hadi basi. Tukio nimeliona vizuri sema picha nilishindwa kuchukua.
No discipline means doing anything arbitrarily!
Leo nilitembelea maeneo ya Tabata kwa mwanangu, wakati narudi kwangu kule Kigamboni , ghafla kufilka pale wanapoita Tabata reli Trafiki Police alisimamisha magari ya upande mmoja ilikuokoa jahazi la magari yanayotoka Buguruni, sasa Gari la mwanajeshi likawa limekumbwa na kizaazaa cha kusimamishwa, mwanajeshi yule ana cheo cha staff sajenti alimvaa Police kwa kejeli na matusi. Trafic akamjibu tuheshimiane lakini mjeshi akaendelea kumtusi askari yule mwenye cheo cha Copro, kama mzaa mwanajeshi akamkwida Uniform , hahahahaaaah Police hakukubali dharau ile, akampiga Mtama mwanajeshi yule, alipoinuka akapigwa Gumi la kuushoto, baada kama ya Dakika 5, MWANAJESHI HOI, ashukuru Mungu jamaa wenye mabucha na askari Police wengine walikuja kuingilia ugomvi ule.
Hakuna dereva wala konda wa daladala alietamani Ugomvi ule uishe, ila jambo lililosisimua na aina ya Ngumi za yuleTrafic dhidi ya Mwanajeshi yule.
atakua aliwaangalia kwa dharau,apigwe tu.Wanajeshi siku zote huwa wana kiburi na kitu kidogo tu huwa wanapiga hawana cha onyo.
Si sawa kupiga raia,wakumbuke raia ndio wanaowalipa wao mishahara kupitia kodi wanazokatwa,pia wao waliamua kuforce kupita njia ambayo siyo yao.Walipaswa wawe wapole na si kujichukulia sheria mkononi,na kwanin wasisafirishe zana zao mida ya usiku wakat hakuna purukushani nyingi.Kama walinzi wetu wanatupiga adui watafanyanyaje? Pia wakumbuke mafunzo yao ni ya hali ya juu na hawakufunzwa kuwapiga raia.NADHANI WAKATI UMEFIKA KWA BAADHI YA WANAJESH KUACHA KUHARIBU SIFA NZURI YA JESH LETU.
Kumbe maskini alikua amepaki pembeni ya barabara kwanini sasa apigwe ?
Ungepiga hata picha eneo la tukio habari ikamilike mkuu!!