Wanajeshi watembeza kipigo kwa raia Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi watembeza kipigo kwa raia Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EMT, Mar 12, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Watu 10 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar baada ya kupigwa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kambi ya Bavuai Migombani kufuatia mke wa askari mmoja kuibiwa pochi na watu wasiojulikana. Mwanamke huyo aliibiwa pochi hiyo huko Jang’ombe katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

  Habari kutoka eneo la tukio zimeeleza askari hao walianza kupiga watu kwa zamu katika mitaa ya Jang’ombe, Urusi na Mpendae majira ya saa 1:00 jioni juzi na kusababisha watu kukimbia ovyo na maduka kufungwa. Msaidizi Katibu Hospitali ya Mnazi Mmoja, Omari Abdalla Ali, alisema majeruhi hao walianza kupokelewa kuanzia saa 2:00 na kulazwa katika wodi namba 1 na 2 na wengine kulazimika kushonwa kutokana na majeraha waliyoyapata katika sehemu za kichwani na mikononi.

  Aliwataja majeruhi hao ambao ni wakazi wa Jang’ombe na Mpendae kuwa ni Juma Issa Mrangi (21), Amini Mwenda Philimon (29), Ali Abrahaman Mwinyi (26), Abeid Ali (18) na Masika Khamisi Ali. Wengine ni Juma Ameir (28), Ali Omar (20), Abrahim Faki Awesu (22), Mussa Phernando (34) na Ali Khamis Mcha (22). Ali alisema majeruhi hao wanaendelea vizuri na matibabu, lakini mgonjwa mmoja amehamishiwa katika Hospitali ya Arhama na wengine waliendelea kulazwa hadi jana katika hospitali hiyo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohammed, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini alisema hadi jana majeruhi waliokuwa wamelazwa ni tisa baada ya mmoja kuruhusiwa baada ya hali yake kuimarika. Hata hivyo, alisema polisi wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha tukio hilo na hawatasita kuchukua hatua za kisheria kwa watu waliohusika kwa sababu tukio hilo ni uhalifu.

  Taarifa kutoka katika eneo la tukio zimeleza kuwa kabla ya askari hao kuvamia na kuanza kupiga wananchi katika mitaa hiyo, mke wa askari mmoja wa JWTZ aliporwa pochi ndani yake kukiwa na simu na Sh. 5,000 katika eneo la Jang’ombe, Urusi.

  Imeelezwa kwamba baada ya mwanamke huyo kuporwa, alifikisha malalamiko kwa mumewe na ndipo askari huyo alipoamua kwenda katika eneo la tukio na kwamba vijana aliowakuta walidai hawahusiki na kumpiga askari huyo kwa jiwe. Hata hivyo, inadaiwa majira saa 1:00 gari la JWTZ aina ya Landrover yenye namba Z997 JW 04 lilifika katika eneo la Jang’ombe Lofi na askari kuanza kushuka kabla ya gari kusimama na kuanza kupiga watu waliokuwa katika eneo hilo.

  “Hali ilikuwa mbaya askari walianza kupiga watu kila waliomkuta njiani au katika baraza ya kahawa na tumeshindwa kutoka majumbani kwenda msikitini kufanya ibada kuhofia kipigo,” alisema Omar Hassan, mkazi wa eneo hilo.

  Alisema askari hao walikuwa wengi na walikuwa wamevaa kiraia na walikuwa wakitumia silaha mbalimbali kama minyororo, mikanda bakora na makwanja ya kukatia nyasi na kusababisha watu kukimbia na kufunga maduka yao.
  Wakizungumza na NIPASHE, baadhi ya majeruhi katika Hospital ya Mnazi Mmoja walisimulia kuhusu tukio hilo.

  Fundi cherahani, Ali Abrahamani Mwinyi, alisema akiwa amefuatana na fundi mwenzake, Tausiri Juma, baada ya kufika Jango’mbe Gengeni waliona mkusanyiko wa watu katika kituo kidogo cha polisi. “Tulikwenda dukani kununua maziwa mara tu baada ya kuteremka katika daladala, tulipokatisha barabara kuelekea nyumbani ghafla watu walituvamia na kuanza kutupiga na sasa nasikia maumivu makali katika sehemu za mbavu,” alisema.

  Alisema aliamua kulala chini na kuficha uso chini ya ardhi, lakini watu hao waliendelea kumpiga na hadi jana alikuwa akigeuka kwa tabu kitandani kutokana na kusikia maumivu makali katika mbavu.

  Kwa upande wake, Omar alisema hadi jana hali yake ilikuwa mbaya kutokana na kipigo hicho. Msemaji wa JWTZ Zanzibar, Luteni Masali, alisema tukio hilo wamelisikia kupitia vyombo vya habari na anaendelea kufuatilia taarifa hizo. Hata hivyo, alisema baada ya kusikia taarifa hizo waliamua kuchunguza kama kuna askari walitoka kambini na kubaini askari wote wakati huo walikuwepo.

  Miongoni mwa watu walioathirika na vurugu hizo ni pamoja na wafanyabiashara wadogo wakiwemo mama lishe baada ya wateja kukimbia vurugu hizo kabla hawajalipa fedha. Mmiliki mmoja wa baa ya Jang’ombe, ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema askari hao waliingia ndani ya baa hiyo na baada ya kuwakuta wateja walianza kuwapa adhabu ikiwemo kuwamwagia maji wakiwa wamelala chini huku wakipigwa na wengine kulazimika kukimbia.

  Wakati huo huo, Chama Cha Wananchi (CUF) kimetoa tamko na kulaani kitendo hicho na kumtaka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dk. Hussen Mwinyi, kuhakikisha askari waliohusika wanachukuliwa hatua za kisheria
  Mkurugenzi wa Uenenzi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Bimani, alisema vyombo vya dola wajibu wake mkubwa ni kulinda misingi ya sheria na sio kuchukua sheria mkononi kama walivyofanya askari hao. “Tunamtaka Mkuu wa Majeshi na Waziri wa Ulinzi kuhakikisha wanachukua hatua za kisheria kwa askari wote waliohusika na kitendo hicho,” alisema.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Tukio kama lilitokea hivi majuzi Dar Es Salaam na mpuuzi mmoja msemaji wa jeshi akawapongeza askari kwa kutemebeza kipigo kwa raia. Kwa huu ni muendelezo wa kauli ya mkuu wao kwamba wanafundishwa kushirikiana. Ni jeshi lisilokuwa na nidhamu ambalo wanajeshi wake wanaweza kufanya upumbavu kama huu na halafu wakasifiwa.

  Pole kwa waliokumbwa na kitendo hiki cha kipumbavu.

  Tiba
   
 3. S

  SeanJR Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo mimi naiyona ni nzur heshma itajengeka kwao! Mtu mkewe kaibiwa anaenda kuuliza kwa heshma mnampiga mawe,aaah,kwa tusidundwe! Sio Tanzania tu,nakumbuka nlipokua Texas Marekani kuna mwanajeshi alivamiwa njiani,wenzanke wakapata habari wakaja ka gari kumi wakawachakaza raia vzuri sana! Tarehe 22'feb'2011 kwa wale wanaofuatilia habar watakua mashahidi mwanajeshi mmoja aliibiwa na kupgwa akiwa njiani mjini Bulhayo Zimbabwe ikatokea revange ya aina yake! Sasa hapa Tz kdgo tu mnalia wakat mmewachokoza,acha mtulizwe! Big up Jwtz...
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  jeshi la tanzania halina nidhamu kabisa hapo ukiuliza watakuambia tulichokozwa kwa nchi nyingine zilizoendelea wanajeshi wanawaheshimu sana raia kuliko polisi
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Inawezekana ni nidhamu kuanza kukosekana ndani ya jeshi...lakini chanzo chake ni nini?
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  chazo ni ufisadi wakubwa wanaangalia nafasi zao zaidi na kulindana kuliko kusimamia majukumu yao na mambo yanapoharibika wakiambiwa wajiuzuru hawataki kisa wanaogopa tu kua pesa watamuachia nani na lingine nchi hii sasa naona watu wameanza kurithisha madaraka kwa watoto wao hii ni kulindana na ni tabia mbaya sana tanzania sio nchi ya kifalme ni nchi ya kidemokrasia mimi lawama zote nazitupa kwa mkulu mwenyewe!
   
 7. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Wanajeshi ndebwedo, raia ndebwedo! Kaazi kwelikweli!
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ikiwa ni haki jeshi kupiga raia eti kwa sababu kapigwa, ni haki pia kwa raia kuwapiga wanajeshi ikiwa watapigwa; vivyo hivyo kwa polisi, mgambo, JKT, JKU, na kadhalika. Kuna ubaya gani anayeibiwa kumpiga mwizi? Kuna ubaya gani ikiwa vibaka watajkusanya kulipiza kisasi kifo cha kibaka mwenzao aliyepigwa na "wananchi wenye hasira"? Mwisho wa habari, kuna maana gani ya kuwa na mahakama ikiwa kila mmoja anaweza kujichukulia hatua mikononi mwake?

  Hivi ndivyo unavyoelewa maana ya demokrasia kuwa "kila mmoja ana haki ya kufanya anavyotaka"?
   
 9. S

  SeanJR Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAMMAMIA,sio demokrasia kila mmoja kufanya anavyotaka! Ila mleta mada katuambia jamaa mke wake kaibiwa,kaenda kuchek inakuaje wanampga namawe..hata ukiangalia kiuhalisia ingekua nimmoja wapo wa hao wa2 knachofuata nikipgo tu wala sio kwamba vbaka nao warevange,c lengo! Lengo nikuwakomesha vibaka na kujenga heshma ukimuona kbaka anazengua mripotishe kunakohusika,ukinyamaza kipgo kikikufikia usilaumu!! Wanajesh na wananch wanapaswa kuwa kitu kmoja,lakin sio kunvizia mlinda nchi wako! 2we na mipaka,ndo maana likfka laku2fka 2nalaumu!
   
Loading...