Wanajeshi wa Tanzania Wafa Maji Darfur

silao

Member
Apr 1, 2012
24
7
Taarifa ambayo imenifikia muda huu kutoka huko nchini Sudan jimbo la Darfur.Kuwa askari wawili wa jeshi la wananchi wa Tanzania wamekufa kwa kuzolewa na maji wakati wakivuka mto kwa kifaru na gari lingine la kivita. Askari hao kwa ujumla wao walikuwa wanne. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa moja usiku na kwa bahati nzuri mmoja alipatikana akiwa taabani usiku huo. Wengine wawili miili yao imepatikana leo mchana na mwingine mwenye cheo cha Captain bado hajapatikana. Aliyepatikana hai anaendelea vizuri. Helcopter za Umoja wa mataifa bado zinaendelea na kazi ya kumtafuta huyo mmoja ambaye bado ni kitendawili cha aidha yu hai au ameshafariki. Utaratibu wa kusafirisha miili ya hao wawili kuja nyumbani zinafanyika na majinayao yatatangazwa baada ya ndugu na jamaa zao kujulishwa. Mungu alaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMEN.
 
Sasa wameuawa? heading yako vp? Wamekufa maji, result of drowning,kuuawa kunatoka wapi?
 
Badili Heading hawajauwawa....
je haiwezi someka hivi wameuawa kwenye ajali?mbona tunaandika wameuwawa na simba,n.k kwanini isiwe wameuwawa kwa kusombwa na mafuriko?naona mtoa taarifa yupo sahihi!
 
kuna thread iliwahi kuwekwa hapa jf ikieleza manyanyaso wanayopata wanajeshi walioko sudan kwa kupunjwa malipo yao.je kuna uhusiano wowote?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
.
Wameuawa na maji!
R.I.P makamanda wetu.
.

wewe kassim uelewa wako ni mdogo sana sas kama hawakuuwawa na maji wameuwawa na kitu gani? Rudi shule usianze kuangalia upande mmoja tu kuna sentensi zina maana zaidi ya moja, lakini wewe unakwenda moja kwa moja kwenye maana moja tu unayoija " cause of death ni nini? Bila hayo maji wangekufa? :israel:
 
Back
Top Bottom