jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,412
- 5,013
Wewe Una Askari Jeshi au Una Wasanii Tu! Ukitaka Professional Soldiers Ambao Wapo Very Intelligent, Focused, Courageous, Brave, Committed, Ethical na Very Respectful Nenda Nchini Rwanda. Askari Wa TPDF Wanamengi Sana Na Mno Ya Kujifunza Kutoka Kwa Wenzao Wa RPF........Ukweli Ndiyo Huo MKATAE au MBISHE.
kwanza nadhani ulitaka kusema RDF sio RPF, RPF kwa sasa ni chama tawala sio jeshi.
1. Ripoti ya UN iliyotoka wakati Rwanda ni mwenyekiti wa baraza la usalama iliweka wazi kuwa M23 walikuwa sio tu wanasaidiwa na hiyo RDF, bali walikuwa wamepenyeza mpaka batalioni za RDF humo.. Askari wetu hawa hawa mnaowaita vitambi ndio waliowachapa hao M23 including hao mamluki wa RDF. Mziki wa "vitambi" hao RDF wanaufahamu fika.
2. Hao RDF wameshindwa kuwapiga ex-FAR toka 1994 mpaka leo, wameweza kupindua nchi nzima ya DRC lakini wamewashindwa ex-FAR, mpaka ex-FAR wakajiunga na wakimbizi kutengeneza FDLR mwaka 2000. Tokea muda huo pia mkapa leo wapi! kila wakienda operesheni za kutokomeza FDLR wanachemsha, wanaishia kumalizia hasira zao kwa wakimbizi wa kihutu badala ya kupigana na wanaume wenzao. Hadi saa hivi Rwanda imeamua kuomba collabo za majeshi mengine EAC, kenya, sijui ethiopia kote huko kutaka kupigana na kikundi tu cha ex-FAR wa mwaka 1994? Hivi wangetuomba sie tupambane na FDLR unadhani ingechukua muda gani? Watu wanajiitaje wanajeshi halafu washindwe kupambana na waasi kwa miaka zaidi ya 20? halafu wewe unawafananisha na JW? Hao RDF hawana ubavu wowote wa kulinganishwa na JWTZ, tena kwa upande wa ethics ndio kabisa, saizi yao ni kama panya road kwa atrocities walizofanya DRC (refer to UN mapping report). Real soldiers kama JWTZ hawafanyi hivyo kwa defenseless people, vitambi or no vitambi!