Wanajeshi wa Msumbiji wawaokoa raia waliotekwa na Wanamgambo wa Islamic State

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Wanawake 15 na watoto sita waliokuwa wametekwa na Wanamgambo wa Islamic State katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Cabo Delgado nchini Msumbiji wameokolewa na jeshi.

Wengi wao walikuwa wametekwa kutoka katika kisiwa cha Matemo wiki iliyopita, kulingana na mkuu wa polisiBernardino Rafael.

Mapigano ya hivi karibuni yanaonesha kua vikosi vya usalma vilifahamu ni wapi walipokuwa wanamgambo hao, kwa hiyo kwa usaidizi wa helikopta waliweza kuwazingira na kuwatenganisha na watekaji wao, alisema.

Watarejeshwa tenaMatemo, eneo ambalo limezongwa na mashambuliotangu mwezi Oktoba.

Lakini mkuu wa polisi amesema kuwa kisiwa hicho ni salama kwa sasa.

Wanamgambo wa IS, wanaofahamika na wakazi kama al-Shabab, au vijana , wamefanya mashambulio kadhaa katika vijiji na miji katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka mitatu.

Wanamgambo

Hivi karibuni zaidi waliahidi kulitii kundi la IS , na wanafahamika kwa mashambulio ya ukatili, ambayo huwa ni pamoja na kuwakata vichwa wanavijiji na kuchoma moto nyumba.

Mara nyingi huwateka wanawake na watoto ambao hutumiwa kama watumwa wa ngono na kusafirisha bidhaa walizoiba kufuatia mashambulio.

Mwishoni mwa juma, Waziri waulinzi wa Marekani alisema kuwa Anthony Tata, naibu waziri wa mashauri ya kigeni anayehusika na masuala ya sera alitembelea Msumbiji Ijumaa na kufanya mazungumzo na mawaziri juu ya umuhimu wa mpango wa kimkakati wa kuleta utulivu katika jimbo la Cabo Delgado.

Wanamgambo wa Islamic State wanafahamika kwa kukata vichwa na kuchoma nyumba za wanavijiji.

Wanamgambo wa Islamic State wanafahamika kwa kukata vichwa na kuchoma nyumba za wanavijijiImage caption: Wanamgambo wa Islamic State wanafahamika kwa kukata vichwa na kuchoma nyumba za wanavijiji.

Taarifa kutoka ubalozi wa Marekani inasema kuwa Marekani itatoa msaada wa kibinadamu na kiuchumi wa dola milioni 42 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika jimbo hilo lililopo kaskazini mwa nchi.

Juhudi hizi na nyinginezo, kwa mujibu wa balozi Dennis Hearne, ni sehemu ya msaada wa kila mwaka wa dola milioni 500 ambao Marekani hutoa kwa Msumbiji.
 
Wenye wametengeneza tatizo sasa watasema watuma watu wao kuja kulimaliza

Vita ya kiuchumi ni vita ngumu sana
 
Hivi kweli watu wanaoweza kuzingirwa, nini kinashindikana? Kwani kuomba msaada kwa mabeberu kuna tatizo?
 
Hivi kweli watu wanaoweza kuzingirwa, nini kinashindikana? Kwani kuomba msaada kwa mabeberu kuna tatizo?
Kuna wanaodai mabeberu ndio chanzo ili wachimbe mafuta hivyo hawapaswi kuombwa msaada, japo ushahidi wa hilo hawana.

Wengine wanaona kuomba msaada ni kukiri serikali imeshindwa hivyo itajenga picha mbaya kwa raia kwamba serikali yao ni dhaifu hivyo watapoteza kura ukifika uchaguzi.

Wengine wanaogopa masharti watakayopewa na mabeberu ambayo ni ngumu kutekeleza hivyo wanaona bora wasiombe.
 
Tatizo watu wanaishi kwa heresay sana
..upo sahihi..watu wanajazwa ujinga kirahisi sana.

Kila kitu kiovu chanzo chake kinahusishwa na mabeberu tena tunaaminishwa ni wabaya mno na hawatutakii mema.

Ila wakitupa pesa zao tunawaita wafadhili, marafiki na washirika wa maendeleo.
 
Back
Top Bottom