Serikali yaahidi kuwaadhibu Wanajeshi walioua Raia 85 'Kimakosa'

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Serikali ya Nigeria, Alhamisi iliahidi kuwaadhibu waliohusika na shambulizi la ndege zisizo na rubani na kuua takriban raia 85 kimakosa huku shutuma na wito wa kufanyika uchunguzi ukiongezeka.

Jeshi limesema wanajeshi walikuwa wakifanya doria za anga Jumapili walipoona kundi la watu kaskazini magharibi mwa Jimbo la Kaduna, na kutafsiri vibaya mtindo wao wa shughuli kuwa sawa na wa wanamgambo.

Ndege isiyo na rubani ilishambulia kijiji cha Tudun Biri, kimakosa wakati wakazi walipokuwa kwenye sherehe. Vyanzo rasmi vimesema takriban watu 85 waliuwawa na wengine 66 kujeruhiwa.

Vikosi vya jeshi la Nigeria, mara nyingi hutegemea mashambulizi ya anga katika vita vyao dhidi ya wanamgambo kaskazini magharibi na kaskazini mashariki mwa nchi, ambapo wanamgambo wenye msimamo mkali wamekuwa wakipigana kwa zaidi ya muongo mmoja.

VOA Swahili
 
Je, kuna ufanano wa mikusanyiko na shughuli kati ya zile za wanamgambo wa Boko Haram na zile za dini yetu?
MK254 njoo utie neno kidogo, maana we unauzoefu kidogo na yaliyofanyika West gate.
 
Nna uhakika zaidi ya 99% kwamba hawakufanya kwakukosea
Nigeria nchi ya hovyo sana na viongozi wao wengi washenzi
 
Back
Top Bottom