Wanajeshi wa Burkina Faso washikiliwa kwa madai ya njama ya mapinduzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875

th

Mamlaka nchini Burkina Faso imetangaza kukamatwa kwa wanajeshi wanane wanaotuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Kanali Mohamed Emmanuel Zoungrana - kamanda maarufu wa zamani wa jeshi ambaye ameripotiwa kuikosoa serikali.

Wizara ya haki Jumanne ilisema uchunguzi kuhusu suala hilo umeanza.

Mapinduzi ya mwisho nchini Burkina Faso yalifanyika miaka saba iliyopita wakati kitengo cha kijeshi chenye utata kinachomtii rais aliyetimuliwa na aliye uhamishoni, Blaise Compaoré, kilipochukua mamlaka.

Kiongozi wa sasa, Roch Marc Christian Kaboré, alifanya mabadiliko makubwa kwa serikali mwezi uliopita wakati akiwa chini ya shinikizo la kukabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara ya wanamgambo wa Kiislamu.

BBC Swahili
 
Back
Top Bottom