Wanajeshi 800 wastaafishwa nchini Rwanda

Wanajeshi 800 wastaafishwa nchini Rwanda

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,312
_96985142_gettyimages-462935969.jpg

Askari jeshi zaidi ya 800 wakiwemo baadhi ya maafisa wakuu katika jeshi la Rwanda wamestaafishwa.

Miongoni mwa waliostaafishwa ni majenerali wawili waliowahi kuongoza idara za upelelezi za nchi hiyo, Jenerali Karenzi Karake na Jenerali Jack Nziza.

Mwaka uliopita majenerali hao walibadilishiwa nyadhifa walizokuwa nazo jeshini, hatua ambayo kwa baadhi waliifasiri kuwa kama kushushwa ngazi.

Kulingana na wizara ya ulinzi ya Rwanda baadhi ya waliostaafishwa wamekamilisha mikataba yao jeshini na wengine ni kutokana na sababu za ugonjwa.

Mwandishi wa BBC aliyepo Kigali Yves Bucyana anasema kwa jumla maafisa waliostaafishwa ni 817.

Luteni jenerali Karenzi Karake kwa muda mrefu aliongoza idara ya upelelezi ya Rwanda na nje ya mipaka ya nchi hii akawa naibu kamanda wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Naye Brigedia jenerali Jacques Nziza alishika nyadhifa mbali mbali katika wizara ya ulinzi ukiwemo wadhifa wa mkuu wa vitengo vya upelelezi.

Mwaka 2015 akiwa mkuu wa upelelezi, jenerali Karenzi alikamatwa mjini London kufuatia waranti ya kimataifa iliyotolewa na nchi ya Uhispania ikimhusisha yeye na maafisa wengine wa jeshi la Rwanda kwa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Rwanda na jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Hata hivyo, baada ya pilka pilka za kidiplomasia Uingereza ilimwachia huru kwa kile ambachoJaji alisema sheria za nchi hizo mbili hazilingani.

Pamoja na hayo, mageuzi ya mwaka uliopita ndani ya jeshi ambapo majenerali hao walibadilishiwa nyadhifa, kwa baadhi yalitafsiriwa kama kushushwa ngazi.

Jenerali Karenzi aliachishwa kazi ya mkuu wa upelelezi na kutangazwa kama mshauri wa rais wa masuala ya kijeshi huku Jacques Nziza akapewa wadhifa wa kuongoza kitengo cha kuratibu shughuli za jeshi na wananchi.

Tangazo la wizara ya ulinzi ya Rwanda, pamoja na kuonyesha picha za karamu iliyoandaliwa kwa ajili ya waliostaafishwa, limeelezea tu kwamba miongoni mwa askari hao, zaidi ya 300 walikuwa mchanganyiko wa maafisa wakuu na maafisa wa dogo, na kwamba baadhi walihitimisha mikataba yao na jeshi la RDF huku wengine 70 wakistaafishwa kwa sababu ya ugonjwa.

Chanzo:
BBC
 
kama hakuna conspiracy kwenye retirement ya hawo 800 soldier is well and fine. Ila kama kuna hila na figisu-figisu, i guess somebody won't go away with it!
 
Hii inafanana fanana na yanayo jili huko Uganda - binafsi nafikiri jamaa hawa wanataka kujenga mazingira ya kutaka kurithisha watoto wao kwenye viti vya Urais - kumbukeni watoto wao wa kiume wana vyeo vikubwa jeshini - I might be wrong lakini dalili zinaonyesha hivyo - na wanaotiliwa mashaka kwamba wanaweza kuzima njama hizo ndio wanaondolewa kiana - maigizo ya kujifanya ni kistafisha emass ili hisionekane wanalenga watu fulani - a very clever ploy ya kuondoa upinzani wa kirithishana Urais kama Ufalme vile - yetu macho lakini mtakuja kuniambia.
 
Siku zote wanaokaa madarakani kwa muda mrefu hawajiamini, wako paranoid na ndo maana hufanya haya.

Vyombo vya dola hubinafsishwa na kutumika kukidhi matakwa yao.
 
Back
Top Bottom