Trump anazidi kutengwa na kuhusu Iran

Trump anazidi kutengwa na kuhusu Iran

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,698
Reaction score
7,883

l

Maelezo ya picha,John Phelan akiwa na Donald Trump

Katibu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani John Phelan anaondoka katika utawala wa Trump, imetangaza Pentagon siku ya Jumatano.

Kuondoka kwake "ni mara moja," msemaji wa Pentagon Sean Parnell alisema katika chapisho la mitandao ya kijamii.

Parnell aliongeza kuwa, Naibu Katibu Mkuu wa Jeshi la Wanamaji Hung Cao atahudumu kama kaimu katibu.
Phelan ndiye kiongozi wa hivi karibuni wa ngazi ya juu wa kijeshi kuondoka katika utawala huo katika miezi ya hivi karibuni. Kuondoka kwake kunakuja wakati wa vita kati ya Marekani, Israeli na Iran na kuendelea kwa vikwazo vya Marekani kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz.

"Kwa niaba ya Waziri wa Vita na Naibu Waziri wa Vita, tunamshukuru Katibu Phelan kwa utumishi wake katika Jeshi la Wanamaji la Marekani," Parnell aliandika. "Tunamtakia kila la kheri katika maisha yake ya baadaye."
Jeshi la Wanamaji halijatoa sababu ya kuondoka kwa Phelan.

Hii inakuja wiki chache tu baada ya Waziri wa Vita/Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth kumtaka Mkuu wa Majeshi Randy George ajiuzulu kutoka wadhifa wake.
Maafisa wengine wawili wa Jeshi, Jenerali David Hodne na Meja Jenerali William Green, pia wameondolewa katika nyadhifa zao hivi karibuni.

Tangu aingie Pentagon, Hegseth amewafukuza kazi dazeni ya maafisa wakuu wa jeshi, akiwemo mkuu wa operesheni za majini na naibu mkuu wa wafanyakazi wa Jeshi la Anga.

Jukumu la Katibu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani kwa kiasi kikubwa ni la kiutawala na linajumuisha kuunda sera, kuajiri, kutoa mafunzo na kuwapa vifaa Jeshi la Wanamaji, pamoja na kusimamia bajeti na vifaa kama vile ujenzi, na ukarabati wa meli na vifaa vya majini.

Phelan, ambaye hakuwahi kuhudumu jeshini hapo awali, aliapishwa kama Katibu wa Jeshi la Wanamaji Machi 2025 baada ya kuteuliwa na Rais Donald Trump 2024


Source: Reuters
 
Kukiuzulu huko Ulaya na Amerika ni jamno lankawaida. Sasa huwa wanaishije akiacha kazi kiholeoa hivi? Naomba kueleweshwa, maana hata Afrika hata mtu akiua watu milioni moja hataki kuachia madaraka
 
Kukiuzulu huko Ulaya na Amerika ni jamno lankawaida. Sasa huwa wanaishije akiacha kazi kiholeoa hivi? Naomba kueleweshwa, maana hata Afrika hata mtu akiua watu milioni moja hataki kuachia madaraka
Kule kazi ya umma sio ya kitega uchumi,sasa huku kwetu hizo kazi wanazitafuta hata kwa kulala makaburini u
 
Huyo John Phenan amefukuzwa kazi na wala hajajiondokea tu hivyo kama unavyojaribu kupotosha.

Jaribuni kuwa mnaandika habari za ukweli na kuachana na hizi za kuokoteza okoteza toka sijui huko masjid ubwabwa.


 
Kwaiyo kwasasa jukumu lipo kwa katibu Mchina Hung Cao!!

Mkuu wa FBI Muhindi katibu uko Pentagon hung Cao China !!!

bado Marekani ipo kwenye mipango ya kulejea kwenye hatamu za Dunia🧑‍🦯🧑‍🦯🧑‍🦯🧑‍🦯🧑‍🦯🧑‍🦯
 
Back
Top Bottom