Wanahitajika vijana 4 haraka!

Wanahitajika vijana 4 haraka!

TheMnyonge

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2022
Posts
738
Reaction score
1,899
Wanahitajika vijana wanne 4, umri miaka 16-22, watakaa kwangu, (baada ya kufahamiana vema na wazazi/walezi wao)

Watakuwa na kazi ya kuuza matunda kwa kutumia matoroli, baada ya mimi kuweka mtaji na kuwapatia vifaa vya kazi,tutakuwa tukigawana faida baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji.

Kama una ndugu, jamaa au rafiki wanaoweza kufanya hii kitu nawakaribisha!

N.b, atakayekuwa tayari, nitafika kwao ili kufahamiana na walezi/wazazi wake.
 
Toa basic information kama location, Phone number, malipo etc
 
Mwamba nipo hapa. Toa details za kutosha niage kabisa hapa nyumbani Namtumbo.
 
Hapo anasubiri awajaze madogo wote wanne chumba kimoja chenye magodoro yaliyolika, na kuwalisha ugali kila siku na kuwatumikisha bila kuangalia upande wao na kujali maslahi tu
Aisée sinaga ukatili wa hivyo mkuu, wote tu tunakula kutoka kwenye meza moja, watakula ninachokula, na watalala sehemu safi kabisa!
 
Vijana wanachopaswa kujua ni kwamba, unapopata kazi mdogo kabisa inakula uzoefu na inakukutanisha na watu wa aina tofauti tofauti, from there unaweza kupata network ambayo ungejifungia kwenu na certificates zako, usingeweza kukutana nazo kamwe!
 
Hapo anasubiri awajaze madogo wote wanne chumba kimoja chenye magodoro yaliyolika, na kuwalisha ugali kila siku na kuwatumikisha bila kuangalia upande wao na kujali maslahi tu
sio wote bro, Ma-boss wanaoamiini katika laissez-faire leadership na huwajali sana wafanyakazi wao. Hiyo hiyo kazi kuna dogo nilikutana naye zenj ana kitoroli cha machungwa kama kighorofa anasema kwa siku kuuza machungwa ya elfu 80 ,90 hadi laki ni kawaida sana,akikosa saaana huwa anauza elfu 30-50...hapo akitoa running cost kwa siku hakosi faida kuanzia 30+(ingawa huko sikumuuliza)....inawezekana jamaa kishausoma mchezo anataka kutumia fursa na sio makosa sababu hata watu ni rasilimali kubwa sana kwenye fursa yoyote.
 
Well said invisible, watu wanapokuwa na negative attitude kwa kila kitu ni tatizo kubwa sana, mimi vijana wote niliowahi kufanya nao kazi huwa tunakula meza moja, kama ni dagaa basi wote tutakula dagaa, kama ni maharage wote tunakula maharage,hivyo yaani
 
Back
Top Bottom