Wanaharakati wengi upinzani ni waoga sana

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau,

Utafiti Uliofanyika umethibitisha kuwa "Wanaharakati" Wengi sana hasa wa upinzani hawana sifa za kuwa wanaharakati.

Wengi wao ni waoga sana hata kushindwa kuainisha utambulisho wao. Siyo rahisi hata kujua majina yao halisi au makazi yao au mawasiliano yao au shughuli wanazofanya kuwaingizia kipato.

Wanatofautiana sana na wanaharakati wazalendo ambao muda wote huainisha utambulisho wao bila woga wala hofu na pia ni rahisi hata kuwasiliana nao kwa njia mbalimbali hata kukutana.

Hi ni aibu kubwa Sana kwa "Wanaharakati" hao hewa kutoka Upinzani.

Nawasilisha.
 
Maneno ya uzalendo hutumiwa sana na Madikteta. Huko nyuma ina maana nchi ilikuwa haina watu wanaoipenda nchi yao? wameibuka chini ya utawala huu au mnatafuta mahali pa kujificha kufanya maovu?
 
Huyo ni kibaraka wa watawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna mwanadamu asiye na woga. La sivyo hujakamilika. Ujasiri ni vita ya ndani ya mtu kuushinda woga. Watu wote wana woga isipokuwa wanajitutumua kuushinda na kuitwa majasiri.

Jana nimesikiliza mwanaharakati kenya aliyekuwa anampinga Moi, alipigwa mpaka akapelekwa motuary alipozinduka akakuta maandamano yanaendelea naye akajiunga akaendeza mapambano hadi alichoamini kikatokea. Mwandishi akamuuliza ulikua haogopi.? Akajibu nilikuwa naogopa sana ila nilitamani nione mabadiliko na niliona yamekaribia ndicho kilichonipa moyo.

Kwa hiyo uoga upo na ndio ubinadamu ila kuna kupigana kuushinda ndani yako.

Heko ziende kwa mdude, pamoja na yote hajanyamaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uanaharakati unawafaa watu walio tayari kufumuliwa marinda maana ndio adhabu ya kwanza utakayopewa pindi utakapozingua
 
Back
Top Bottom