Wanahabari watashabikia CHADEMA dhidi ya Usalama wao?

Nipo makini kufuatilia mwenendo wa media katika hii kamatakamata ya watuhumiwa wa kutekwa, kuteswa na kuumizwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, na kuteswa wanahabari kwa ujumla wao kwani haijulikani nani atafuatia kung'olewa kucha na jicho baada ya Kibanda.

Nataka kuwaiti je, wanahabari baadhi wataendeleza ushabiki wao kwa CHADEMA badala ya kuwa objective Kama taaluma inavyowataka? Nimeona udhaifu mkubwa kwao kushabikia zaidi CHADEMA kinyume cha mipaka yao ya kazi. Let's stay tuned.
Hapo penye nyekundu; wewe "stay tuned" na uendelee kucheza ngoma za wauaji akina IGHONDU na Jack Zoka; "stay tuned" ukicheza jinsi afisa usalama wa zamani Maembe aka Joka la mdimu anavyowaelekeza maharamia wa TISS kuishughulikia kambi ya LOWASA na upinzani. "Stay tuned"
 
media watashobokea wauaji cdm badala ya kutafuta ukweli.wanachadema vilaza kuanzia mkiti hadi mlinzi wa get sasa mmeshikwa masaburi mmetulia kama unaliwa

Acha kutukana viongozi wako wa 2015 kuwa nanidhamu humu tupo wakubwa zako.
 
Kaa hivyo hivyo unaefikiri kwa masaburi,kaa na imani eti kuna mtu au chama kinataka kukomboa matatizo ya familia yako,fanya kazi!
Mungu wangu hivi kuna watu wanaishabikia CCM katika karne hii. Ubongo wako umelambwa na NYATI!!
 
Naomba nitangulie kusema kwanza nina heshimu observation yako juu ya topic hiyo ya waandishi wa habari, "ushabiki" wao kwa CHADEMA (as you suggest), wimbi la utekaji na yote hayo., Lakini LAZIMA iwe wazi tu kwamba waandishi wahabari wana haki, (pamoja na professional ethics zao zinazo wataka kuwa objective) - ya kueleza/ kuonyesha opinion yao kuhusu chochote kile wazi bila kuhitajika kuficha,. haki hiyo hatuwezi kuwapokonya! niyakwao kwa sheria ya tanzania kama wananchi wa tanzania hii.

lakini pia lazima tukubaliane kwamba hatutegemei kwenye nchi yenye vyombo vya habari zaidi ya elfu moja na waandishi professionals kwa maelfu yao, WOTE wawe na mtazamo unao fanana, ni wazi wapo watakao kua na mtazamo flani kuhusu jambo flani na wengine watakuwa na mtazamo mwingine tofauti kuhusu jambo lilelile na hii haimfanyi mwandishi mmoja kuamshabiki wa CHADEMA na mwingine wa chama kingine eti kwasababu tu ya mtazamo wake juu ya swala flani. OF COURSE! ni jukumu na wajibu wa mwandishi yeyote kuhakikisha kuwa anaandika habari kwanza yenye UKWELI mtupu (atleast kwa kiwango atakacho jiridhisha nacho), lakini pia Yenye kusikiliza pande zote (objectivity iwepo), yenye ushahidi na vyanzo vya uhakika, na yenye kujenga jamii badala ya kubomoa., lakini mtazamo wao juu ya jambo lolote haupaswi kutafsiriwa kama ushabiki kama hayo niliyo yasema hapo juu yamezingatiwa.

lakini pia LAZIMA NI SEME HAPA kwamba kama tuta sema "natuone sasa" kama waandishi wataendeleza ushabiki wao kwa CHADEMA atawakiwa wanatekwa na kuteswa TUTAKUA TUNAKOSEA SANA SANA SANA., kwakuwa lugha hii inaonyesha siotu kutokua na kujali, au kutokua na huruma na hawa waandishi wetu lakini kuyafurahia haya yanayoendelea sasa hivi, nakuonyesha WAZI kwamba kumbe kuna watu wa kundi flani ambao wao wangefurahia haya kuwapata waandishi wenye mtazamo positive juu ya CHADEMA na kuonekana vikwazo kwa chama kingine flani,. nahii inatupa mwanga kabisa kwamba huenda watu hao (wanao ona waandishi ni wa shabiki wa CHADEMA) wasi ishie hapo tu ila wakaamua kwenda mbali zaidi na kuanza kuyatekeleza haya tunayo yaona sasa nakisha kupakaza kwa watu wengine ilikuficha ushahidi., Well, nisiende mbali sana, sina nia ya kum convict mtu yeyote hapa, ila ninacho kisema nikwamba sisi kama wana nchi tunao ipenda Tanzania yetu hii tulipaswa kukataa kabisa haya., bila kujali ni chadema, tlp, cuf ama ccm.

lakini kwa muda sasa inanipashaka kwamba huenda kuna watu wana tumia JF kuendeleza propaganda chafu za vyama vyao. LAKINI HII SIYO SAWA hatakidogo!!.,

Niombe watanzania wenzangu kwapamoja, tuulinde uhuru wa vyombo vya habari na wana habari wetu., kwakua pasipo hawa ukombozi wa taifa letu ni mgumu sana sana sana., mahali popote pale ukombozi wa taifa ulipo hitajika WANAHABARI ndiyo walio fanya kazi kubwa zaidi ya ukombozi., popote pale.

South Africa wakati wa Apartheid na utawala wa the Nationalist Party kilicho kua na mitazamo ya kibaguzi haikukombolewa na Nelson Mandela peke yake kwa mikono yake mwenyewe., ukiwa mchunguzi wa haya utagundua wapo waandishi wa habari walio sacrifice wengine zaidi hata ya Mzee Mandela wakati wa Liberation Struggle ya nchi yao. read about Michael Harmel a key figure in the underground communist party, a founding member of the Congress of Democrats and an editor of the magazine liberation.. kulikua na Benjamin Pogrund of the Rand Daily Mail., Patrick Duncan Editor and Publisher of the Contact news paper na wengine wengi., Mandela na wenzake wasinge iweza kazi ile bila hawa!!

Ninachokisema hapa nikwamba HAWA NDIYO WAKOMBOZI WA TAIFA HILI (Waandishi wa Habari)., pamoja nakwamba tutasimama wote wananchi pamoja na viongozi wa vyama vyetu katika mapambano dhidi ya UFISADI, UBADHILIFU WA FEDHA, na KUTOKUWAJIBIKA KWA SERIKALI ZETU,. lakini hatutaiweza kazi hii ya ukombozi na ulinzi wa rasilimali za taifa LETU bila ya hawa watu,. hawa hatuwezi kuvumilia kuona wakitumiwa vibaya kwa michezo michafu ya kipropaganda alafu tuka kaa eti tukisema "ngoja sasa tuone kama wataendelea kushabikia CHADEMA".,


Ndugu zangu
Ni hayo.,

Asanteni
mungu akubariki na popote ulipo akuzidishie hekima zaidi ya hizi,na azibariki fikra na akili za uzao wako.
 
Nipo makini kufuatilia mwenendo wa media katika hii kamatakamata ya watuhumiwa wa kutekwa, kuteswa na kuumizwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, na kuteswa wanahabari kwa ujumla wao kwani haijulikani nani atafuatia kung'olewa kucha na jicho baada ya Kibanda.

Nataka kuwaiti je, wanahabari baadhi wataendeleza ushabiki wao kwa CHADEMA badala ya kuwa objective Kama taaluma inavyowataka? Nimeona udhaifu mkubwa kwao kushabikia zaidi CHADEMA kinyume cha mipaka yao ya kazi. Let's stay tuned.

Kumbe lengo lenu lilikuwa kuwachonganisha wanahabari na CHADEMA?
 
Waandishi makanjanja ni shida sana. Aliyepigwa ni mwenyekiti wa jukwaa la wahariri lakini hao wanachama wake wanamshabikia muuaji wao

Hii ishu imekuwa kama ile ya shonza, walikuwa wanaripoti ya chadema tu lakini madai ya shonza hakuna gazeti wala tv iliyoonyesha,,,njaa mbaya sana
Wanahabari si wajinga muwaue harafu wawashabikie, mtabaki na redio Clouds tu redio ya kihuni na Uhuru na Mzalendo magazeti yasiyo na mvuto wowote.
 
Wanahabari si wajinga muwaue harafu wawashabikie, mtabaki na redio Clouds tu redio ya kihuni na Uhuru na Mzalendo magazeti yasiyo na mvuto wowote.

Kwani Lwakatare yupo chama gani bingwa wa kuteka waandishi wa habari.
 
Kwani Lwakatare yupo chama gani bingwa wa kuteka waandishi wa habari.
Jadili mada iliyopo na si kuandika chochote unachowaza kichwani, muwaue waandishi halafu mtegemee wawape coverage kubwa kwani wao wajinga?...wamewagomea..mlitegemea hii itakuwa kete yenu lakini imewarudi.
 
Utaifakwanza, Naona unadhibiti wanaokurupuka humu JF kwa hoja, kweli wewe kamanda. Yaani unanikumbusha pale siku papa anatangazwa kwenye balcony wanaanza kusema kwa kilatini abenus papam ..... We have a new pope.....kwako wewe nasema we have a new commander katika kujibu wanaokurupuka.

TUTEGEMEE nini kama mwanamme "kageuka"????!!!!
 
Haiitaji kuwa msomi saaana kujua walio nyuma ya utesaji huu, hata maigizo yafanywe kiasi gani wengi wetu twajua watesaji ( hata wanaoteswa wanawajua ) hivyo kwa wanahabari ku side na polisi inawaitaji wao kunufaika na either polisi au serikali kama uwaonavyo CLOUDS na bila shaka TBC cuz hawana option hata kama ukweli wanaujua.
 
Jadili mada iliyopo na si kuandika chochote unachowaza kichwani, muwaue waandishi halafu mtegemee wawape coverage kubwa kwani wao wajinga?...wamewagomea..mlitegemea hii itakuwa kete yenu lakini imewarudi.

Mada gani zaidi ya unyama wa Lwakatare dhidi ya waandishi wa habari.
 
Kama ni suala la ushahidi, uliletwa hapa jamii forum ndo poor intelinjensia ikaudaka, maswali ambayo ni ya kuanzia kabisa kabla ya kufika kuchukua hata hii you tube avidence, ni je, kama wanaamini jamii forum kama resourceful centre of information mbona hawakumhoji mwigulu kuhusu kuwa na video ya viongozi wa chadema wakipanga mikakati ya mauaji? Hili lilikuwa la kupuuza? Kweli? Je mbona mpaka leo hawajamhoji Membe kuhusu maadui 11 wawili wakiwa waandishi wa habari, hata kama wangefanya hivo kwa kuweka kumbukumbu in case of anything? Hili nalo ni la kupuuza? kweli? Wakati utaamua.......
Yawezekana unahisi unajua kila kitu kumbe bahati mbaya upo nyuma kabisa na masuala ya usalama. Ni vema wakati mwingine kuweka pembeni masuala ya uchama na kuupa ubongo nafasi ya kudadavua.
 
Siku zote mlaji ndio huchagua ale nini na si mpishi. Sasa wananchi ambao ndio wateja wa habari wanachagua wasome nini, na waandishi wa habari huandika kufuatana na 1. Taaluma yao, 2. Weledi wao na 3. Utashi wa soko. Mwandishi atakaekaa siku nzima akiandika habari za uzuri wa siasa za NAZI za Adolf Hitler kwenye magazeti ya uingereza, hata kama ni kwa lugha tamu kiasi gani, unategemea atapata mafanikio?
Sasa kwa Tanzania CHADEMA ndio habari ya mujini, ukiandika habari zako za kuiponda CHADEMA na kuitukuza CCM, jua gazeti lako hata Nape hatalisoma maana anajua sio kweli. Weka magazeti mawili ya uhuru na mia ya Tanzania daima, pita baada ya masaa mawili, idadi ya magazeti kwenye ubao, uhuru mawili, Tanzania daima hakuna. Kwa wakati tulio nao CDM ndio habari, habari ni CDM.
 
Back
Top Bottom