Wanahabari watashabikia CHADEMA dhidi ya Usalama wao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanahabari watashabikia CHADEMA dhidi ya Usalama wao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kageuka, Mar 17, 2013.

 1. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nipo makini kufuatilia mwenendo wa media katika hii kamatakamata ya watuhumiwa wa kutekwa, kuteswa na kuumizwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, na kuteswa wanahabari kwa ujumla wao kwani haijulikani nani atafuatia kung'olewa kucha na jicho baada ya Kibanda.

  Nataka kuwaiti je, wanahabari baadhi wataendeleza ushabiki wao kwa CHADEMA badala ya kuwa objective Kama taaluma inavyowataka? Nimeona udhaifu mkubwa kwao kushabikia zaidi CHADEMA kinyume cha mipaka yao ya kazi. Let's stay tuned.
   
 2. m

  my web JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 23, 2012
  Messages: 1,603
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  media watashobokea wauaji cdm badala ya kutafuta ukweli.wanachadema vilaza kuanzia mkiti hadi mlinzi wa get sasa mmeshikwa masaburi mmetulia kama unaliwa
   
 3. Iwindi_Mbalizi

  Iwindi_Mbalizi Member

  #3
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 1, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mleta mada sijui umelenga nini maana sijui kama hayo ya chadema yaliyoripotiwa yana kasoro zozote kama yana kasoro basi ungeyakosoa.Mi nadhani kama wandishi wana ripoti ukweli si kosa whether ya chadema mengi au mazuri.Ni vyema ukatambua kuwa pengine wakiacha kuripoti hayo ya chadema ndiyo watakuwa hawaripoti ukweli.Nafikiri kama wanakosea kuripoti basi hao wahusika wangechukua hatua za wazi za kisheria kuwapeleka wahusika kunakohusika na si mambo ya gizani wanayoyafanya,maana hayo mabaya yanayofanywa na wahusika gizani yanahalalisha kuwa hao waandishi wameripoti ukweli unaowauma wahusika....
  Big up waandishi wa kweli na Mungu awaondoshee mabalaa yote!!!
   
 4. Makete Kwetu

  Makete Kwetu JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2013
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wenzako wanaumiza vichwa ni jinsi gani watabiliana na Tundu Lisu kwa court wewe unaifurahisha akili yako mgando kuwaita viongozi wa CDM vilaza
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,182
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Wanahabari wanashabikia ukweli hawashahabikii Chadema, chunga kauli mufilisi kama zako!
   
 6. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2013
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 2,040
  Likes Received: 1,135
  Trophy Points: 280
  kuna wash.... wachache wanachelewesha ukombozi wa taifa hili toka kwa manyangau walewale miaka nenda rudi kwasababu tu wao wananufaika mbaf. sana.
   
 7. g

  gayo JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 237
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wewe chichiem uliyetumwa na magamba shindwa na ulegee!Utakuwa mamluki hadi lini?Mungu alikupa kichwa kwaajili ya kufikiria na siyo kufugia nywele..

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 8. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2013
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 19,012
  Likes Received: 11,652
  Trophy Points: 280
  mada zingine bwana..:..........!!!
   
 9. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,434
  Likes Received: 1,359
  Trophy Points: 280
  mkulu yawezekana mtengeneza filamu ya lwakatare mojawapo ya malengo yake ilikuwani kuwachonganisha cdm na vyombo vya habari vinavyo washabikia.
   
 10. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2013
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ni Tanzania tu ambapo polisi wanafanyia kazi ushahidi wa Yutube!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Maboso

  Maboso JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 4,303
  Likes Received: 2,631
  Trophy Points: 280
  Yawezekana unahisi unajua kila kitu kumbe bahati mbaya upo nyuma kabisa na masuala ya usalama. Ni vema wakati mwingine kuweka pembeni masuala ya uchama na kuupa ubongo nafasi ya kudadavua.
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,373
  Likes Received: 13,991
  Trophy Points: 280
  mkuu unaweza kutumika kama itathibitika nikweli pasi na shaka!

  Unakumbuka kibonzo cha kumkashifu mtume? Ilikuwa rahisi kumpata aliyeweka maana ushirikiano ulitolewa kwa youtube!
   
 13. saronga

  saronga JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2013
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 909
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  we unafikiri hao wanahabari ni mambumbumbu kama wewe!? unataka kuwalisha maneno yako ya kimbeambea. wameshawashtukia, mnawatesa halafu mnataka muwatumie kuwapendezesha ili anguko lenu lichelewe. mlianza kwa Stan Katabaro, mkamtesa kubenea, mkamuua mwangosi mkamteka dr ulimboka (rama wa magogoni) sasa kibanda, sijui nani atafuatia. Muda wenu umekwisha, mmeshachakaa kisiasa. Mlango waliotokea KANU ya kenye nyie ndo mtakaotokea, mtabaki kuwa historia. Aibuuuuuuuuu, mimacho kesho itawatoka mahakamani kwa miaibu mtakayoipata.
   
 14. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2013
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Magamba hamna hoja kabisa na mnatumia akili ndogo kwenye masuala mazito.Hivi wale polisi waliomuua mwangosi walitumwa na CHADEMA? Watu waliowahi kumwagia tindikali Saed Kubenea na hatimaye baadae kulifungia gazeti la MwanaHalisi ni CHADEMA? Hivi aliyemshitaki Kibanda kwa 'uchochezi' alipolikosoa jeshi la polisi ni CHADEMA? Hivi Mhe.Bernard Membe aliyekiri ITV kuwa ana waandishi wa habari wawili ana bifu nao na kuahidi kuwashughulikia ni CHADEMA? Tuambie kada wa CCM aliyemtemea mate mwandishi wa habari 2012 kule Mufindi alitumwa na CHADEMA? Na yule aliyewahi kuwa mwandishi/mtangazaji Amina Chifupa aliyetaka kuwaumbua makada wa CCM kabla ya kuawawa kwake,je ni CHADEMA? Kama una akili timamu utagundua huhitaji degree ya metaphysics kujua adui wa mwandishi wa habari ni nani!
   
 15. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2013
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,233
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 135
  Akina Stan Katabalo walitolewa kafara na Chadema?
   
 16. Character X

  Character X JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2013
  Joined: Nov 22, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Naomba nitangulie kusema kwanza nina heshimu observation yako juu ya topic hiyo ya waandishi wa habari, "ushabiki" wao kwa CHADEMA (as you suggest), wimbi la utekaji na yote hayo., Lakini LAZIMA iwe wazi tu kwamba waandishi wahabari wana haki, (pamoja na professional ethics zao zinazo wataka kuwa objective) - ya kueleza/ kuonyesha opinion yao kuhusu chochote kile wazi bila kuhitajika kuficha,. haki hiyo hatuwezi kuwapokonya! niyakwao kwa sheria ya tanzania kama wananchi wa tanzania hii.

  lakini pia lazima tukubaliane kwamba hatutegemei kwenye nchi yenye vyombo vya habari zaidi ya elfu moja na waandishi professionals kwa maelfu yao, WOTE wawe na mtazamo unao fanana, ni wazi wapo watakao kua na mtazamo flani kuhusu jambo flani na wengine watakuwa na mtazamo mwingine tofauti kuhusu jambo lilelile na hii haimfanyi mwandishi mmoja kuamshabiki wa CHADEMA na mwingine wa chama kingine eti kwasababu tu ya mtazamo wake juu ya swala flani. OF COURSE! ni jukumu na wajibu wa mwandishi yeyote kuhakikisha kuwa anaandika habari kwanza yenye UKWELI mtupu (atleast kwa kiwango atakacho jiridhisha nacho), lakini pia Yenye kusikiliza pande zote (objectivity iwepo), yenye ushahidi na vyanzo vya uhakika, na yenye kujenga jamii badala ya kubomoa., lakini mtazamo wao juu ya jambo lolote haupaswi kutafsiriwa kama ushabiki kama hayo niliyo yasema hapo juu yamezingatiwa.

  lakini pia LAZIMA NI SEME HAPA kwamba kama tuta sema "natuone sasa" kama waandishi wataendeleza ushabiki wao kwa CHADEMA atawakiwa wanatekwa na kuteswa TUTAKUA TUNAKOSEA SANA SANA SANA., kwakuwa lugha hii inaonyesha siotu kutokua na kujali, au kutokua na huruma na hawa waandishi wetu lakini kuyafurahia haya yanayoendelea sasa hivi, nakuonyesha WAZI kwamba kumbe kuna watu wa kundi flani ambao wao wangefurahia haya kuwapata waandishi wenye mtazamo positive juu ya CHADEMA na kuonekana vikwazo kwa chama kingine flani,. nahii inatupa mwanga kabisa kwamba huenda watu hao (wanao ona waandishi ni wa shabiki wa CHADEMA) wasi ishie hapo tu ila wakaamua kwenda mbali zaidi na kuanza kuyatekeleza haya tunayo yaona sasa nakisha kupakaza kwa watu wengine ilikuficha ushahidi., Well, nisiende mbali sana, sina nia ya kum convict mtu yeyote hapa, ila ninacho kisema nikwamba sisi kama wana nchi tunao ipenda Tanzania yetu hii tulipaswa kukataa kabisa haya., bila kujali ni chadema, tlp, cuf ama ccm.

  lakini kwa muda sasa inanipashaka kwamba huenda kuna watu wana tumia JF kuendeleza propaganda chafu za vyama vyao. LAKINI HII SIYO SAWA hatakidogo!!.,

  Niombe watanzania wenzangu kwapamoja, tuulinde uhuru wa vyombo vya habari na wana habari wetu., kwakua pasipo hawa ukombozi wa taifa letu ni mgumu sana sana sana., mahali popote pale ukombozi wa taifa ulipo hitajika WANAHABARI ndiyo walio fanya kazi kubwa zaidi ya ukombozi., popote pale.

  South Africa wakati wa Apartheid na utawala wa the Nationalist Party kilicho kua na mitazamo ya kibaguzi haikukombolewa na Nelson Mandela peke yake kwa mikono yake mwenyewe., ukiwa mchunguzi wa haya utagundua wapo waandishi wa habari walio sacrifice wengine zaidi hata ya Mzee Mandela wakati wa Liberation Struggle ya nchi yao. read about Michael Harmel a key figure in the underground communist party, a founding member of the Congress of Democrats and an editor of the magazine liberation.. kulikua na Benjamin Pogrund of the Rand Daily Mail., Patrick Duncan Editor and Publisher of the Contact news paper na wengine wengi., Mandela na wenzake wasinge iweza kazi ile bila hawa!!

  Ninachokisema hapa nikwamba HAWA NDIYO WAKOMBOZI WA TAIFA HILI (Waandishi wa Habari)., pamoja nakwamba tutasimama wote wananchi pamoja na viongozi wa vyama vyetu katika mapambano dhidi ya UFISADI, UBADHILIFU WA FEDHA, na KUTOKUWAJIBIKA KWA SERIKALI ZETU,. lakini hatutaiweza kazi hii ya ukombozi na ulinzi wa rasilimali za taifa LETU bila ya hawa watu,. hawa hatuwezi kuvumilia kuona wakitumiwa vibaya kwa michezo michafu ya kipropaganda alafu tuka kaa eti tukisema "ngoja sasa tuone kama wataendelea kushabikia CHADEMA".,


  Ndugu zangu
  Ni hayo.,

  Asanteni
   
 17. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Bahasha mkuu, hawawezi kuwa objective hata siku moja. Watatumika mpaka wakome
   
 18. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Hata ishu ya juliana shonza waandishi waliichunia baada ya kupewa bahasha mara tu shonza alipomaliza press yake pale maelezo. Njaa mbaya sana
   
 19. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Njaa ni mbaya sana
   
 20. Frank King

  Frank King JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2013
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 1,184
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Daima ukweli ama haki kma haki haiwezi kudhihirika kama haikupitia lang'ata ya uwongo!haki ni ukweli.hakuna aliyeshinda kwa uwongo akadumu basi kwa yaliyomtokea Kibanda hayawahusu wanahabari kwani si wao tu wamekumbwa na huo unyama, ila kazi ni kwao kuufia ukweli au kutokuufia.

  Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
   
Loading...