Wanahabari kilimanjaro: Yaliyojiri mkutano feki

STINGER

Member
Oct 18, 2011
41
11
Baada ya mkutano feki wa mecki, wakati wanachama wengine wakiendelea na chakula, viongozi wa mecki waliokuwepo walikuwa na kikao cha dharura na kupitisha maamuzi yafuatayo;

1. Charles ndagula anaedaiwa kamera zaidi ya miaka miwili sasa afuatiliwe kwa nguvu zote airudishena fidia ya shilingi milioni moja la sivyo afikishwe mahakamani

2. Chuwa nae alipe shilingi 140,000/= anazodaiwa kumpa fadhila kamera bila kufuata utaratibu hivyokusababisha uchakavu

3. Uongozi ufanye haraka sana kujibu tuhuma zilizo chini chini ya kuwa nakajumo katibu wa mecki amempa baba yake kamera aitumie bila malipo

kwa nini viongozi hawa wamejenga chuki ya haraka hivi hata kwa mtu waliemtumia kutengeneza katiba yao?

Kwanza wamesahau yakuwa wamekiuka katiba kwa vile ratiba ya mkutano wa marekebisho ya katiba ilikuwa na ajenda moja tu ya marekebisho ya katiba lakini wao kipengele cha kupendekeza tarehe ya kujaza nafasi zilizo wazi wakatumia vibaraka wao kujipatia nafasi hizo kama walivyopanga mwanzo
 
Back
Top Bottom