Wanafunzi wawili wa kike watelekezwa 'guest'

Ni kweli kabisa wala sipingani na wewe Mpwa wangu only one thing kwamba unayaaongea haya ukiwa nje ya tukio, naapa kama nisingekuwa na maadili ningekuwa nimewatafuna; huo ni ukweli but i have been helping them, teaching them this and that, ingawa wakati mwingine wanaonekana kunizidi ......well, nimewasidia sana kisaikolojia ( I am proud of this) ningekuwa na uwezo ningekutuma kwene hio shule ukaulize
Kama mwalim uliye matured ni bora ukaelewa kuwa watoto wanapofikiaumri fulani wanakuwa na mambo mengi ya kuashiria ngono.
Na si vizuri wewe ukajichukulia hiyo nafasi kwa kutokuelewa kwao.
Wengi ni wadogo hawana uwezo wa kupambanua bado wao wanaona dunia tamabalale .

Umri walionao ni mbaya wakudanganyana, kuiga na kujaribu kila jambo.
Eh MUNGU OKOA HILI KIZAZI KISIANGAMIE Maana watoto wengi cku hizi ni yatima wamekosa malezi bora
 
Hapana siko hivyo hebu soma hicho nilichikiandika hapo juu, then judge me accordingly......ningekuwa na uwezo ningekuelekeza uende kwenye shule niliyokuwa nafundisha
watu wenye mawazo kama yako ndio wanaoharibu watoto. Mtoto wa mwenzio mwanao. Alaaaaa!
 
Kwa sababu fulani fulani sitakuelekeza kwenye blog yangu ambayo Mimi ni mmoja wapo ya Campaigner wakubwa (naweza sema hivyo) kuhusu elimu ya watoto wetu.........
Una watoto?ndugu wadogo ..............au wenzio sio wakakwo?sidhani kama angekuwa mtoto/mdogo wako ungeandika hivi.
 
Picha please for evidence



Habari zenu wana JF,
hivi kizazi hiki kinaelekea wapi jamani ?nimekutana na habari hii nikaona niwape mtafakari na nyie.

WANAFUNZI wawili wa kike wa kidato cha pili katika sekondari ya Enyeitu mkoani Arusha, wametelekezwa katika nyumba ya kulala wageni Dar es Salaam kwa mwezi mmoja sasa.

Wasichana hao wakazi wa Mianziani, Arusha, walifika Dar es Salaam Juni 4 wakifuatana na mwanamume anayejulikana kwa jina la Rwaka au Swai.

Mwanamume huyo aliwafikisha katika nyumba hiyo ya Flamingo iliyopo Nzasa A Mbagala katika wilayani Temeke.

Wanafunzi hao Neema Abel (17) anayedai anaishi na mjomba wake, Amos Michael na Tatu Salim (16) aanayeishi na dada yake Aisha Salim, walifika katika nyumba hiyo siku hiyo saa nane usiku na kupokewa na mhudumu Zainabu Abdallah.

Mwandishi wa habari hizi alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni juzi na kuwakuta wanafunzi hao wamekaa nje kama wapo nyumbani tena wakicheza bao na baadaye akazungumza nao.

Awali, mhudumu huyo alidai kuwa mwanamume huyo aliwaandika katika daftari la wageni wanafunzi hao kuwa ni Aisha Salim (Tatu) na Angela Amos (Neema) ambaye alidai mwanamume huyo ni baba yao mdogo na walifika naye jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutembea.

Alisema, baba huyo alikuwa akifika kila siku katika nyumba hiyo na kuwapa fedha za chakula na kulipia gharama ya chumba namba nane walichokuwa wakiishi kwa wiki tatu.

Zainabu alisema, baadaye walishangaa kutomwona huyo mtu na hivyo wasichana hao wakashindwa kulipia chumba na chakula ndipo wakafichua kuwa hakuwa baba yao na amewatelekeza na wanadaiwa Sh 35,000 za chumba.

Mabinti hao wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, walidai kuwa, mwanamume huyo ambaye ni mtu wa makamo, alikutana nao Arusha na kuwa marafiki wa kawaida.

Tatu alisema, baada ya kufunga shule, baba huyo aliwaambia waje Dar es Salaam kuona mji, ndipo naye akamtafuta rafiki yake, Neema, ambaye wanasoma wote shule moja na kutorokea Dar es Salaam.

Alisema, walipofika jijini, mwanamume huyo aliwaambia waseme kuwa ni baba yao mdogo na kuwaacha kwenye nyumba hiyo naye akaenda kwa mkewe, na akawa akifika mara kwa mara akiwa na rafiki yake na kuwaachia matumizi.

Alisema, siku moja alifika na kumtaka kimapenzi alipokataa, ndipo alikawaambia kuanzia siku hiyo watajua wenyewe watalala wapi, kula wapi na hata nauli ya kurudi Arusha.

Alisema, kuanzia siku hiyo wamekuwa wakipika chakula pamoja na wahudumu wa nyumba hiyo, huku bado wakiwa na deni la Sh 35,000 na bila kusema fedha wanazochanga kwa ajili ya chakula wanazipata wapi.

Angela alisema, wanachohitaji sasa ni nauli ya kuwarudisha Arusha, ili kuendelea na masomo, kwa kuwa shule wanayosoma ilifunguliwa jana na wamejifunza kutokana na makosa waliyofanya.

Baadhi ya wafanyakazi wa nyumba hiyo, walidai wasichana hao walisitishiwa huduma baada ya mwanamume huyo kuwakuta wakiwa na vijana wadogo na baada ya kusitishiwa huduma, wamekuwa wakitoka usiku na kwenda kwenye kumbi za starehe ili kupata fedha za kujikimu.

Source:Habari leo 11th JULY 2011

 
Malezi mabaya kutoka kwa wazazi woa yanasababisha haya mambo, wiki jana nimeshuhudi mama anamfokea binti yake under 18 amepata ujauzito cha kushangazi binti naye akamropokea mama yake kuwa mbona yeye mama hajatulia ana wanaume wengi nje.
 
Sikiliza na hii nayo; miezi karibia mitatu iliyopita kabla sijaikimbia hii fani ya chaki; tulimuita binti mmoja (form three) ofisini na kumuelekeza na kumuonya kwa tabia ya kubadilisha mabwana na kuchelewa nyumbani( kama ilivyorpotiwa na Mlezi wake) binafsi nilimuita baadae na kumueleza kuwa yeye ni mwanafunzi mwenye akili na uwezo, aachane na mambo hayo au kama hawezi basi japo apunguze ili uzito uhamie kwenye masomo....tuliongea kwa kirefu sana na tukakubaliana kuwa atabadilika, siku chache baadae ikija kesi nyingine ya kukutwa na mwalimu akiwa amekumbatiwa na mwanaume barabarani paleee maeneo fulani ya Sinza akiwa na uniform (sifa mbaya kwa shule) akaja na mzazi wake this time, mama akalia weee, akaeleza na shida zake na jinsi maisha yao yalivyo ya shida, hilo nalo likaisha, nikamuita tena nikaongea nae, akalia naee akasema mwalimu anamsingizia tu, yakaisha...haaa cha kushangaza wiki iliyofuata ambayo shule ilifungwa kwa mapumziko ya mafupi....yule binti hakurudi kwao ile siku ya ijumaa hadi Mlezi wake anaeishi naye (haishi na mama yake na huyo mlezi wake pia hata hawana undugu) alipokuja kutoa taarifa shuleni, ikabidi taarifa ifike polisi then the following wiki piacha na tangazo likatolewa ITV kipindi cha Jiji letu kuwa amepotea...in short baada ya wiki tatu hivi akarudi na akaja shule, anaulizwa ulikuwa wapi anasema alikuwa kwa ndugu yake.......well hio ndio nature ya watoto wetu, kama mwanafunzi anaishi na mwanaume wewe mwalimu ambaye pengine hata kuoa au kuolewa bado utamfundisha nini akuelewe??
Malezi mabaya kutoka kwa wazazi woa yanasababisha haya mambo, wiki jana nimeshuhudi mama anamfokea binti yake under 18 amepata ujauzito cha kushangazi binti naye akamropokea mama yake kuwa mbona yeye mama hajatulia ana wanaume wengi nje.
 
Ok, hii habari niliisikia pia but mimi nawalaumu hawa watoto kwa kupenda vitu vya cheee, well najua mwaweza kuni-challenge but I have been teaching, I know wanafunzi walivyo, huwa nashangaa hata serikali ikipiga makelele eti walimu wanawapachika mimba wanafunzi......hebu imagine unafundisha mtoto wa kike kakukalia uchi, maziwa nje! Narudia kusema kwamaba naongea kitu ambacho nimekuwa nikikishuhudia kwa macho yangu, well najua wanafunzi wangu watakua wananimisi baada ya kauchana na Ualimu (kuasi taaluma) maaana binti akinikalia uchi nilikua namwambia kabisa kwamba fulani naomba ufunge duka lako.....yes, I did it. Sasa akitokea mtu mwingine ataona ndio nafasi ya kuvitafuna maana katoto ni kazuri mbaya halafu kanakufuata eti kanaomba nauli au umsaidie swali wakati mko wawili tu halafu angalia kanavyrembua na mapozi ya ajabu ajabu.....Namkumbuka sana Baba yangu siku moja alisema hivi: Tusimlaumu Chui peke yake, tumlaumu na Mchunga mbuzi pia.Any comment? nipo tayari kutoa ufafanuzi na experience binafsi kuhusu wanafunzi hasa hawa wa Mjini....challenge me then
according to teaching ethics, The dog should never eat the bone tied around its neck! Akikukalia uchi chapa viboko na sio kumla kondoo!
 
Walitokea wapi wakienda wapi? Wapuuzi wakubwa hawa, hawa ni machungodoa wakubwa hawa, unatakiwa uvikamate uvichapeeee na "fimbo" hadi vikome, ndio vinatuletea tabia chafu mashuleni na vyuoni...pumbaf kabisa, kudanganywa gani huko toka Arusha hadi Dar kama si umalaya ni nini? yaani mtu sio ndugu yako halafu ukubali tu uje tu....No, hawa watoto hiii tabia walikuwa nayo kabla
viranga vayo nao wacha wakome, walifuata nini Guest?
 
Hahahaaaa, sijasema nimevila Mpwa ingawa chances zilikua nyingi ila kweli sometimes unatamani uviltafune......si unasema hivyo kwasababu uko nje ya hali halisi....unatakiwa unisifu bana, leo ni wangapi wanaweza kufanya hivyo? Ngoja nitaku-PM uende pale ukaulize kama nilitafuna hata kamoja zaidi ya kuviumbua tu. Haya
according to teaching ethics, The dog should never eat the bone tied around its neck! Usijifagilie kwa huo upuuzi! Akikukalia uchi chapa viboko na sio kumla kondoo. Bora hata umeiacha kazi cuz ur useles...!
 
Huyo baba ana balaa hasa na hao watoto balehe inawapeleka vibaya maana inaonekana wanategemea zaidi ushauri wa age mates kuliko responsible adults. Inawezekana hata contacts za huyo fataki hawana,hawajui anakoishi wala anakofanya kazi. Wazazi/walimu/walezi tujitahidi kuwafundisha life skills na kujitambua na tuwe karibu na vijana wetu tukiwahimiza kuwa wawazi na kutueleza yanayowasibu. Tuwaonyeshe kuwa tuko kwa ajili ya kuwasaidia na si kuwahukumu.Ulezi kazi jamani ila tukimtanguliza Mungu atatuongoza vema.
 
Hao watoto ni machangudoa wazoefu, Wamevaa uso wa mbuzi na hawana aibu hata chembe, hainiingii akilini vibinti kama hivyo kusema eti vimerubuniwa, ukweli ni kuwa mapenzi vilianza long time na mahala vilipovikia kuvirudisha kwenye mstari ipo kazi.
 
Back
Top Bottom