Wanafunzi waua Chuo kikuu Mzumbe

Wanafunzi waua Chuo kikuu Mzumbe

Hamjaibiwa ninyi!! Maumivu yake ni makali sana. Usiku raia anasaka nini mabwenini?

Hapa kinachozungumziwa ni kuchukua sheria mikononi huyo waliyemuua wamemkuta na kidhibiti chochote? Hivi Laptop ina thamani sawa na uhai wa mtu? Wewe kweli ni Editor au kanjanja? Unawa-support hao vilaza wa mzumbe kwa upumbavu waliofanya? Mie nishawahi ibiwa vitu vingi vyenye thamani lakini nimechakarika nimenunua vingine lakini siwezi kushiriki kuua mtuhumiwa kisa kapigiwa yowe la mwizi,vilaptop vyenyewe pentium ii.
 
Kijana hajawatoka bali mmemtoa na mkome kusema bwana alitoa na bwana ametwaa ila dhambi ya kuua iko pale pale maana amri ya Mungu ilisema tusiue na haikufafanua kuua kwa vipi. Hapo mseme bwana alitoa na nyie mmetwaa sio bwana ametwaa ila nawapa pole wanakijiji kwa kumpoteza kijana wao kabla hajampokea Yesu kama Bwana na Mokozi wa maisha yake. Kama alipata nafasi ya kutubu kabla hajakata roho ataenda mahali pema peponi.

Bwana ametoa wao wametwaa,swadakta!
 
Inawezekana lengo lao ilikua sio kuuwa ila ikatoka jamaa kafaa, nadhan itakua fundisho kwa vibaka wengine kwan sasa wamegundua kuwa wanafunz nao wamechoshwa na vitendo vyao
 
sasa naona vita imeanza task Kati ya changarawe na wanafunzi, mwisho uswaz ya chini
 
Duh! Mzumbe hiyo! Msalimieni Mecky Nduye mwanakijiji maarufu changalawe.
 
Naona wna MU mnaanza kujuliana hali ni vema sana#kijana kuondolewa ni sawa kwani hali ya kuibiwa ni mbaya sana kama mnakumbuka matukio ya kuibiwa Mara nyingine hutokea kipindicha kuelekea UE na kumfanya mwanafunzi asifanye vizuri kwa sababu ya mawazo#afu naona baadhi wanachangia kwa hasira ya kukosa nafasi kuwa katka chuo pendwa naomba msiwe na hasira kwani kama nyie mlikosa nafasi watoto wenu wanaweza pata nafasi siku moja nao wakalala maria nyerere kinje mkwawa vikenge matola Sophia na bweni pendwa kingo na kibasilaambapo maji hayakatiki.
 
wanafunzi chuo kikuu mzumbe morogoro wamemuua mwanakijiji cha changarawe kijana anaekadiriwa kuwa na miaka 24 kwa tuhuma za wizi, kijana huyo ameuliwa jana majira ya usiku na wanafunzi katika maeneo ya bweni la kimweri na kibasila.

Hii ni mara ya pili ndani ya miezi isiyozidi mitatu kwa wanafunzi hao kuua raia ambao walishukiwa kujihusha na vitendo vya wizi wa mali za wanafunzi.

Ikumbukwe kuwa wanafunzi wa mzumbe baadhi tuko chuoni sasa katika semester yumbishi kutokana na chuo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.

mimi nimesoma mzumbe... Kwa kweli wanakijiji wa pale ni wezi mno.....

Wameshawahi kuniibia nguo zangu zote nilizianika baada ya kufua
 
mimi nimesoma mzumbe... Kwa kweli wanakijiji wa pale ni wezi mno.....

Wameshawahi kuniibia nguo zangu zote nilizianika baada ya kufua

Niliibiwa Mirambo summit. nilikuwa najiandaa kumaliza semester. Mliopo MU msalimieni Komba na Mbano. Pia Paulo Nsimbila.
 
Hapa kinachozungumziwa ni kuchukua sheria mikononi huyo waliyemuua wamemkuta na kidhibiti chochote? Hivi Laptop ina thamani sawa na uhai wa mtu? Wewe kweli ni Editor au kanjanja? Unawa-support hao vilaza wa mzumbe kwa upumbavu waliofanya? Mie nishawahi ibiwa vitu vingi vyenye thamani lakini nimechakarika nimenunua vingine lakini siwezi kushiriki kuua mtuhumiwa kisa kapigiwa yowe la mwizi,vilaptop vyenyewe pentium ii.

Kushiriki kumuua mtu ni jambo baya, lakini ubaya huo unategemeana na hicho kilichofanywa na huyo mtu. Hawa watu wanaovamia na kuiba mali za watu kuna wakati wanafanya matendo ya hovyo sana. Wanabaka, wanafanya udhalilishaji na hata kuua. Kwa hiyo huruma yako inawezekana imejengeka juu ya ukweli kwamba hayajakufika. Siku ukikamatwa mbele ya mama yako, ukaambiwa umwingilie mwanao au dadako, huku wapuuzi hao wakishuhudia, ndipo utakapokoma kuwa na huruma kwa wapuuzi hao! Ukiona mtu anashiriki kumuadhibu mtu wa ina hiyo, ujue, ama yameshawahi kumfika, au hana imani na vyombo vya dola ambavyo kuwaachia watuhumiwa wa aina hiyo ni jambo la kawaida. Wewe laptop unaina kitu kidogo, lakini kwa mwanafunzi ni kitu kikubwa sana. Wanapata shida kuvipata. Wengine ni watoto wa masikini. Wanalima vibarua kupata kitu kama hicho. Shida zote hizo mtu aingie na kujitwalia kirahisi, hawawezi kukubali. Nakuhakikishia ndugu yangu, huwezi kujua uzito wa msiba hadi ukufike kwanza! Sipendi mauaji ya 'watu wenye hasira kali', ;lakini ukweli ni kwamba wananchi wanachoshwa. Rejea matukio ya kijinga ya wizi na ubakaji wanafunzi hata yakasababisha vurugu kule Kigamboni katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
 
Tuwe makini na headline jamani kabla hujapost mjiridhishe. Hizi sentesi zina maana tofauti kabisa. "Wanafunzi waua chuo kikuu mzumbe" "Wanafunzi chuo kikuu mzumbe waua" sentensi ya kwanza inamaana kwamba wanafunzi wamekiuua chuo kikuu cha mzumbe. Sentensi ya pili ina maana kwamba wanafunzi wa chuo kikuu cha mzumbe wameua. Hii inaweza kumaanisha kuwa wamemuua mwenzao. Nirudi sasa kwenye hoja. Natoa pole kwa familia ya marehemu. Ila napata mashaka makubwa na aina ya wasomi wanaochukua sheria mkononi wakati wanajua kuna sheria. Kwanini msingemkamata na kumpeleka polisi. Mnafundisha nini jamii kuhusu utii wa sheria za nchi? Waliohusika wote kwenye hizo bweni mtakamatwa na kuwekwa ndani na upelelezi ukikamilika mtapandishwa kizimbani na masomo ndo basi. Hamuoni kuwa mmejitafutia matatizo?
 
Siungi mkono suala la kujichukulia sharia mikononi na kuua mtu. Ila kama jamaa alikuwa kibaka kweli basi yaliyomkuta ni 'occupational hazard'. Hawa jamaa wameibia sana wanafunzi pale kwenye kile chuo na walifikia hatua ya kupora kabisa hasa wadada! Yaani mtu anayeiba huwa simuelewi kabisa, mali ni yangu halafu unaninyang'ang'anya kinguvu huku unanidhuru? Nikikukuta unapigwa, sitashiriki kukupiga ila pia sitakutetea!

msimamo wako una mwelekeo wa kuridhia kuuwawa vibaka
 
Kwa mazingira ya mzumbe wanafunzi wasipokuwa imara wanaweza kupata shida sana lakini pia sishangai tuna jamii ambayo inaangalia zaidi haki za wakosaji huku wakiacha kuangalia wahalifu namna wanavyorudisha maendeleo ya watu nyuma nimesoma pale miaka mitatu nimeona wanafunzi wakiibiwa na kushindwa kabisa kumiliki tena hizo Mali na unapopeleka case polisi hufanyika maamuzi na hukum za kawaida kabisa mfano Huyu jamaa mpaka alijulikana kama bad boy kwa ajili ya vitendo vya uhalifu na alikuwa anaanza kuogopwa sasa kwa nini kumuachia aendelee kuishi na kuzidi kuwa tishio#adhabu hiyo inafaa kama umepewa nafasi ya kubadilika na hutaki watu wafanyeje.
 
Lakini pia ukiona watu wa jamii fulani hawakemei maovu na wouvu ni kwa sababu wanaamini kuwa kwa wakati Fulani nao watafanya tukio kama hilo hata kama ni katka namna ya tofauti lakini nao watafanya uovu.
 
Back
Top Bottom