Wanafunzi wasomea kwenye vibanda vya nyasi Dodoma

Wanafunzi wasomea kwenye vibanda vya nyasi Dodoma

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,292
Tanzania leo imeadhimisha Siku ya Walimu Duniani ambapo moja ya changamoto wanayokumbana nayo walimu nchini ni mazingira magumu ya kufundisha na kufundishia ikiwemo uhaba wa madarasa kama ambavyo unaikabili shule ya msingi Misrey iliyopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Hali hiyo inawafanya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kulazimika kusomea katika vibanda vya nyasi huku wengi wao wakikaa chini kwenye vumbi kwa kukosa madawati


Screenshot_20181005-161158.png
Screenshot_20181005-161205.png
Screenshot_20181005-161244.png
.
 
Tufanye harambee jamani tuwasaidie hawa watoto. Chaguzi zimetulia pesa nyingi sana kwa ajili ya kutojitambua wakati hizo pesa zingesaidia sana kwenye changamoto kama hizi.
 
Ngoja jiwe aweke sheria ya kutotuma picha za taasisi ya serikali
 
Marudio ya chaguzi tungewezapata shule 1000 kwa kushirikisha nguvu za wananchi.
Tuendelee kuunga tu mkono
 
Tufanye harambee jamani tuwasaidie hawa watoto. Chaguzi zimetulia pesa nyingi sana kwa ajili ya kutojitambua wakati hizo pesa zingesaidia sana kwenye changamoto kama hizi.
Utamaduni huo wanao jamii zilizostaarabika sie bado.
 
Hilo jina la shule walilitoa wapi?
Linasaundi kama la shule binafsi..

Ila duh.. AIBU.. haswa kama ni ndani ya awamu hii na viongozi wa huko hawana time nayo hadi sasa..
 
Serikali yangu ilivyo na mambo ya ajabu; utaona wao wanakazania aliyepost na kupiga hii picha.
 
Pesa za kurudìa uchaguzi zipo tena mabilioni ila zakutengeneza shule na miŕadì muhimu hazipo/zinasuasua. Alafu kiongozi anasimama live kabisa nakusemà anabana matumizi
 
Waliipenda wenyewe,acha waisome namba ,
Wakishapewa yale manguo yao ya kijani wao ni kuchagua tu mbele kwa mbele.
 
Inamaana wanainchi wahapo wanashindwa hata kujenga vyumba viwili tu mpaka magufuli awajengee
 
Waache uvivu na uzembe,jamii nyingi Tanzania tumejenga shule wananchi wenyewe na serikali inasaidia kidogo baada ya sisi kujitolea.Sasa hao wazazi kazi yao ni kuzaa tu eti wanashindwa kujenga vyumba vya madarasa wawekwe mahabusu wazazi wa hicho kijiji kwa kutowajibika!!
 
Msisahau Dodoma ni "kanda ya CCM" toka mkoloni.
 
Back
Top Bottom