Hayo mabati jamani yalivyo na kutu yakiporomoka na kuumiza wanafunzi mana yameshachoka mpaka kukatika katika..eeeh kweli kuna watu wanaishi duniani na wengine ulimwenguni!!
hiyo bati ikikugusa ,tetanus yake ni bora ukumbwe na UKIMWI. dah! kidumu chama cha mapinduzi!Hayo mabati jamani yalivyo na kutu yakiporomoka na kuumiza wanafunzi mana yameshachoka mpaka kukatika katika..eeeh kweli kuna watu wanaishi duniani na wengine ulimwenguni!!
hapo upepo mkali tu bati linachinja mwanafunzi.....lakini hawaoni hio hatari.....
kwanini wapinzani wasitumie image kama hizi,hospitali kama temeke kuwaonyesha wananchi CCM ilipotufikisha??
Mimi nadhani hata hao wapinzani ni sawa tu na CCM. Kwanza wengi wao ni wanachama wa zamani wa CCM.
Pili, kwa ujumla na sisi wanachi tunachangia kwa kiasi kikubwa hali kama hizi kwa kuwa tegemezi sana kwa serikali. Hivi unataka kuniambia hapo kwenye hiyo shule wazazi wa watoto wasomao hapo wakijikusanya na kufanya harambee ya kuchangisha fedha za kuboresha mazingira ya shule hiyo watashindwa kweli kupata hela za kutosha? Kwanza usikute wazazi wengi wa hao watoto wanatumia hela nyingi sana ktk starehe zao.
Tuna matatizo mengi sana lakini moja ya nililoliona ni ukosefu wa hamasa na mwamko wa kuupiga vita umaskini kwa vitendo. Tunapenda sana kuupiga vita umaskini kwa maneno. Laiti tungepunguza kuongea na kuongeza kutenda tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
Mimi nadhani hata hao wapinzani ni sawa tu na CCM. Kwanza wengi wao ni wanachama wa zamani wa CCM.
Pili, kwa ujumla na sisi wanachi tunachangia kwa kiasi kikubwa hali kama hizi kwa kuwa tegemezi sana kwa serikali. Hivi unataka kuniambia hapo kwenye hiyo shule wazazi wa watoto wasomao hapo wakijikusanya na kufanya harambee ya kuchangisha fedha za kuboresha mazingira ya shule hiyo watashindwa kweli kupata hela za kutosha? Maana usikute wazazi wengi wa hao watoto wanatumia hela nyingi sana ktk starehe zao.
Tuna matatizo mengi sana lakini moja ya nililoliona ni ukosefu wa hamasa na mwamko wa kuupiga vita umaskini kwa vitendo. Tunapenda sana kuupiga vita umaskini kwa maneno. Laiti tungepunguza kuongea na kuongeza kutenda tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
Hili la kusomea chini mbona ni la kawaida kwa nchi hii.
Wakati huo huo inaletwa timu ya nchi fulani inagharamiwa mabilioni kwa mabilioni.
tukiwa na moyo wa kujitolea kama kwenye maharusi na mambo kama hayo tungeweza kusaidia ku-improve vitu fulani.....lakini serikali inabidi iwe mfano.....ni ngumu mimi kuchangia wakati nalipa kodi na naona kodi hio inanunua LAND CRUISER V8 nyingi na najua bei ya gari hio moja ingetosha kununua madawati mengi sana au kuongeza madarasa......
Sawa, kodi ndio tunalipa. Lakini mchango wa jumuia kwenda kwenye mali za jumuia kama mashule ni mchango ambao ni wa moja kwa moja na ni ninyi wenyewe ndio mtakaosimamia hayo matumizi ya fedha mlizozichanga. Hapo serikali mnaipiga bao na kuionyesha jinsi mambo yanavyopaswa kuwa.
Hivi unadhani huko ughaibuni serikali huwafanyia watu kila kitu? Ikija kwenye mambo ya shule/elimu, bustani za kupumzikia, na sehemu za kuchezea watoto, ni jumuia za wanajamii waishio humo ambazo hukaa chini na kupanga mikakati na mbinu za kutatua matatizo yanayozikabili. Wenzetu huwaga hawasubiri serikali kuwafanyia kila kitu licha ya wao kulipa kodi pia.
Tunaweza kabisa kuwa proactive sema basi tu tuko magoigoi na tusiopenda kujishughulisha kwa kubuni mbinu mpya za kufanya mambo yatakayoleta mabadiliko na ndio maana unaona kila kukicha serikali yetu inapokea misaada kutoka kwa wahisani. Kwa hiyo serikali yetu bila wahisani haitafanya kazi vizuri na sisi wananchi bila msaada wa serikali hakuna tunalolifanya. Shameful
kwanini wapinzani wasitumie image kama hizi,hospitali kama temeke kuwaonyesha wananchi CCM ilipotufikisha??
hapo upepo mkali tu bati linachinja mwanafunzi.....lakini hawaoni hio hatari.....