MWANDENDEULE
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 3,996
- 7,087
Inauma sana, watoto waliokwama Dodoma kufuatia kufukuzwa kutoka UDOM waanza uombaomba katika maeneo ya mji viunga vyake hususani Ng'ong'ona, Makulu na maeneo ya Jamatini pamoja na stand ya mabasi.
Pia kwa wale waliojistri kwa jamaa zao wenye magheto pande za makulu na Ng'ong'ona hali si shwari kwani wamelazimika kulala watu zaidi ya wanne kwenye chumba kimoja. Kutoka ghetto moja nililotembelea kujionea hali nimekuta jamaa mwenye ana mke wake wanaishi pamoja lakini kwa kuwahurumia ndugu zake kutoka huko kwao Kigoma kaamua kulala nao pamoja na mkewe kwenye chumba kimoja yaani single room.
Hali ya chakula si rahisi kujua lakini itakuwa mbaya sana bila shaka ikizingatiwa mwenyeji wao ni mwanafunzi pale COED.
Jambo lingine la kusikitisha kuna mabinti waliobeba mimba wakiwa chuoni bila kuwapa taarifa wazazi wao, leo wamebaki wanalia tu katika nyumba walizopanga kwani wanaogopa kurejea makwao wakiwa na mimba au watoto kabisa.